Nyoka Mkubwa avuka barabara

Kama unaendesha Pikipiki au Baiskeli unakutana na nyoka mkubwa kama huyu itabidi usimamae apite ndipo na wewe upite kwa usalama wako.

Sasa si atakufanya kitoweo? Hapo ni Kupiga u-turn na kurudi ulikotoka kwa speed ya Hali ya juu Kuokoa nafsi Tena unahairisha safari kabisa maana huenda anafanya timing ukajua katokomea kumbe yupo around.
 
Njia nyingine wanatumia hawa watu wanaokamata nyoka kwa ajili ya masomo na kazi nyingine ,ila unatakiwa uwe mjasiri..Wanatumia kioo kikubwa ,nyoka anagonga kioo akifikiri anakugonga wewe mpaka anachoka.
Hicho kioo lazima kiwe na ubora unaostahili lasivyo tunaweza kula ubwabwa wa matanga....
 
Huyo ni chatu, na anaweza kukua zaidi ya hapo. Aliyemzidi kwa urefu ni anaconda peke yake ambaye hayuko kwetu Africa.
 

Kipo kikawa cha bluu!dah kumbee!
 
Dk 20 au 30 ni cobra!
 
Huyo sio Koboko ni Chatu. Koboko anaweza kuwa mrefu lakini siyo mkubwa kiasi hiki. Huyu ndiye nyoka wa pili kwa ukubwa duniani asiye na sumu wa group la Constrictors ( wa kwanza kwa ukubwa ni Anaconda then chatu au Python).

Chatu anaweza kuwa na urefu hadi mita 6 na katika urefu huo anauwezo wa kummeza adult. Huyo aliyeko pichani ni mkubwa sana akikukuta kwenye mtego wake anakukamata na hautoki labda upate msaada wa haraka.
 

Hivi ni kweli kuwa nyoka haoni vizuri kama sisi tunavyoona usiku na mchana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…