Nyoka hupigwa kichwani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyoka hupigwa kichwani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kidatu, Dec 3, 2008.

 1. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ndugu wanabodi,
  Napenda kutoa zangu shukrani kwa jitihada zenu za michango ya mawazo kwa lengo la kuijenga na kuitetea Tanzania.

  Kuna kitu kinanikera na naomba kukitoa wazi hapa JF.

  Vita ya kupambana na mafisadi katika nchi yetu sioni kama imeanza pamoja na kelele zote za wananchi kwa serikali husika. Serikali imeanza kuwakamata watu na kuwapeleka mahakamani tokana na EPA pamoja na makosa mengine.

  Lakini kwa upande wangu naona kwamba wanaokamatwa na kufikishwa mahakamani pamoja na kwamba kwa njia moja ama nyingine walihusika katika kulileta hasara Taifa bado wahusika wakubwa hawajaguswa.

  Ningeomba serikali isione haya kuwaonea haya wahusika wakubwa kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

  Mramba na Yona walikuwa mawaziri chini ya Mkapa, bila shaka walichofanya kilipata baraka za Mkapa, sasa kwanini Mkapa hakamatwi?.

  Mkapa ndiye chanzo cha wizi wote na matatizo yote yanayojitokeza sasa, kwanini tuone haya kumwonea haya mtu kama huyo?. Naelewa kwamba Mkapa kama Raisi mstaafu anakinga ya kupelekwa mahakamani, lakini kinga hiyo inakubalika katika makosa aliyoyafanya kama Raisi na si katika makosa aliyoyafanya kama Benjamini William Mkapa.

  Mkapa alikula kiapo cha kuilinda katiba ya nchi, kuilinda nchi, wananchi na mali za nchi kwa akili yake yote, moyo wake wote na nguvu zake zote. Kwa kuitumia ikulu kwa kujinufaisha yeye na genge lake katika kuiba mali za nchi na wananchi tayari amekiuka katiba hivyo anapaswa kufikishwa mahakamani.

  Hii kamatakamata ya vijifisadi inayoendelea haileti maana kama majifisadi yenyewe hayakamatwi hivyo ni bora kuwaachia wote huru. Ni kichekesho kuwakamata Mramba na Yona kumwacha Mkapa. HAPA NI SAWA NA KULIPIGA JOKA MKIANI KUMBE JOKA LINATAKIWA KUPIGWA KICHWANI.
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Dec 3, 2008
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280

  Mimi naona bado inabidi waendelee kukamatwa hawa hawa wadogo.

  1. Fundisho kwa wale wadogo wote popote walipo mnapotumika katika ufisadi, nyie ndiyo mtakaokamatwa?

  2. Dhana nzima ya uisadi hatuelezi wakubwa tu bali na wadogo wote kuanzia ngazi ya wafagizina mamesenja kila idara ofisi n.k

  3. Kama kuna waziri ambaye aliona anakerwa na ufisadi wa serikali ya mkapa angejiuzuru mapema sana, kwa sababu hiyo walikubaliana naye

  4. DHANA YA KIKWETE KUMKAMATA MKAPA NI KUJIDANGANYA KAMA CCM WALIZITUMIA KATIKA UCHAGUZI WOTE LAO MOJA!!!! FUMBUKA MACHO HAWA WENGINE WATANYANYASWA NA MAKOSA YA UFISADI WAO BINAFSI AMBAO HAUKUGUSA CCM YOTE WALA MKAPA.

  HIVYO BASI ISSHU YA YA MRAMBA NA YONA 'WANGEKULA' WOTE USINGEWAONA KEKO


  SO JUA:

  1. KUNA 'DILI' ALICHEZA MKAPA NA WATU WAKE WACHACHE.

  2.ALICHEZA YEYE MWENYEWE

  3. ALICHEZA NA CCM YOTE

  4. MAWAZIRI ;KUNA DILI WALICHEZA WAO WENYEWE BILA MKAPA KUJUA.


  KWA HIYO YONA NA MRAMBA WAKO GROUP LA NNE>>>> WACHA WAKOME

  IKIJA ZAMU YA NAMBA 2 , ACHA IJE ISIZUIE YA NAMBA NNE SASA!!!!!!!!!!!!

  waberoya
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Dec 3, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - For the record, hivi karibuni Ngasongwa, amesikika mahali kwenye masanga akisema kua deal la Yona na Mramba, ni la cabinet nzima, na b included na muungwana alipokuwa minister.
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Dec 3, 2008
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  Ndiyo maana naona, swala hili dawa yake ni CCM yote iodnoke madarakani, au CCM iingiliwe na damu mpaya kabisa with no impurities za wat hawa wa sasa, kitu ambacho ni kigumu sana!

  Ikulu patamu ati!!, haya yote ni maandalizi ya 2010.
   
 5. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #5
  Dec 3, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Wakijisafisha kama wanavyofanya sasa, sio mbaya kupewa a second chance!
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Dec 3, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wanabodi,
  Kwanza ningependa kuelewa uhusiano wa hawa jamaa Yona na Mramba kila tunapozungumzia swala la EPA.
  Pili inaonyesha wazi kila hoja humu JF kuhusu inamhusisha Kikwete ktk maamuzi ya kuwafikisha mahakamani Yona na Mramba...hii taarifa imetoka wapi?..
  Je, haiwezekani kuwa ni vyombo vya sheria ndivyo vimewafikisha mahakamani na sio shinikizo toka kwa Kikwete!..Sote tunafahamu kuwa EPA Kikwete amehusika lakini hili la Yona na Mramba sikumbuki kusikia kuwa Kikwete ameagiza uchunguzi wa watu hawa.
  Ndugu zangu subra, subra ndio tatizo kubwa la watu maskini (sisi sote) na kutokana na kutokuwa na subra ndio maana hata maendeleo hayapatikani..
  Binafsi naamini kabisa kuwa Yona na Mramba sio samaki wadogo hata kidogo, sioni kiongozi fisadi ambaye anaweza kuwa daraja moja na hawa watu tukiondoa Mkapa..Na ni kupitia hawa watu tunaweza kupata ushahidi wa kumhusisha Mkapa!..
  Kama mnakumbuka hata deal la Richmond, Lowasssa hakuwepo ktk hesabu za uchunguzi pamoja na kwamba tunajua alihusika, mwisho wa hadithi alikuja ibuliwa na hao samaki wadogo Mabangusilo!
   
 7. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #7
  Dec 3, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kidatu umetoa wazo zuri, lakini ukumbuke kuwa tukiua joka hili mara moja tunaweza kujistukia kuwa tunakufa wenyewe. Au tukipiga kichwa unaweza ukashangaa kuwa, mikono, miguu na viungo vingine vyote vitafanya kila vinavyoweza kuhakikisha kichwa hakipigwi, kwa hiyo naona approach hii ya kupiga wadogo kwanza kwenye issue hii ni nzuri. Lakini hata mimi nashangaa, kwenye orodha ya makosa walioyosomewa hawa waheshimiwa yanahusu kufanya maamuzi ya kulitia hasara taifa, na sio wizi wa fedha za umma. Hapa nona kama ni tiktak ambayo tunataka kufungwa goli. Ina maana wa EPA wamekwisha au? Maana at the moment mzizi mkuu uko kwenye EPA na makampuni yake na wamiliki wake, (waliotajwa hadharani na waliojificha). Labda ni mimi niliyepitwa na habari.
   
 8. L

  Lorah JF-Expert Member

  #8
  Dec 3, 2008
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  wanavyofanya yapi bado mpaka dk ya mwisho either wameachiwa au wametudai fidia ndo tuseme wamefanya mambo mazuri sasa hivi walaaaa bado
   
 9. K

  Kinto Senior Member

  #9
  Dec 3, 2008
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 109
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wenzetu Thailand wameshinikiza hadi mahakama imekifuta chama tawala na waziri mkuu aliyekuwa amegoma kujiuzulu ni lazima sasa ajiuzulu (hii ndiyo maana ya mpaka kieleweke). Hakuna kuaminiana kirahisi hivi katika masuala haya, ni lazima tubanane kila mtu atimize wajibu wake kwa uadilifu. Mpaka ifikie hatua kama CCM nzima walihusika chama kizima kiwajibishwe kwa kukosa sifa ya kuongoza nchi. Hakuna kusubiri hukumu ya wapiga kura wakati ni dhahiri kuwa wamekengeuka na kujiingiza kwenye ufisadi.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Dec 3, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  NI wakati gani Rais hawi Rais akishakula kiapo, na kabla hajaondoka rasmi au asipoweze kutimiziza kazi zake kwa mujibu wa Katiba? Rais anakuwa Rais anapotia sahihi makaratasi ya kazi lakini akienda kula chakula cha mchana anakula kama mtu binafsi? Rais akiondoka Ikulu kwenda kumtembelea ndugu yake Chalinze anakuwa bado Rais au Urais unabakia Ikulu?
   
 11. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #11
  Dec 3, 2008
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  mkuu wa medani umesema masanga ??!!!

  Tafadhari rekebisha kidogo maana hii italeta kutokuaminika kwa ulichosema hasa pale wanaomfahamu huyu alhaj, rekebisha venue mkuu ukitaka tu buy hii record.
   
 12. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #12
  Dec 3, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280


  Haya yote yangewezekana kama kusingekuwa na kile kitu kwenye Katiba ya nchi Ibara ya 46 kina chosema na nanukuu:

  Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais kutokana na masharti ya ibara ya 46A(10), itakuwa ni marufuku kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa Katiba hii.


  Hapa walijiwekea kinga kwua wasishtakiwe kwa makosa waliyoyafanya wakiwa madarakani ili kuweka kujikinga maana wanajua wakiwa madarakani wanafanya mambo yao ya kipuuzi

  Hadi hapo Bunge litakapokaa na hatpa inategemea Bunge lenye nia hasa ndio linaweza kwa maamuzi ya Theluthi Tatu ya Wajumbe wa Bunge hilo baada ya hoja binasfi kuwasilishwa bungeni na kuungwa mkono hapo wanaweza kumuondolea kinga hiyo rais ambaye hayuko madarakani kuweza kushtakiwa.

  Je tuna Bunge la namna hiyo hapa kwetu ambalo linaweza kumuondolea kinga hiyo rais
   
 13. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #13
  Dec 3, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Kuwa kwenye masanga au maeneo ya msanga si lazima na wewe ushiriki masanga, huwa kuna soda, maji, juce, totozzzzzz! na vinginee vingi tuuuuuu. Sasa inategemeana muheshimiwa alifuata nini pale na likuwa na nani!! Hlafu pia kila kitu kina mwanzo!
   
Loading...