siku mapigo yangu ya moyo yatapofuta
nuru itazima mfano wa nyota inapodondoka
stoweza kuamka tena macho yangu yatapofumba
safari imewadia naenda kwa baba muumba
maasela nawaachia usia
waambie ndugu na jamaa wapunguze kulia
sote tutakwenda bali mimi ninatangulia
duniani sio makazi yangu tena
niombeeni kwa mola nilazwe peponi pema
hamtoniona tena mileelee
nawaachieni majonzi teelee
buriani naagana nakata kauli
roho yangu inatolewa na izraelii
yowee la uchungu litasikika
pale roho yangu itakapokuwa inatoka
masela wangu saana nitakuwa nimefikwa
nipo kwenye jeneza tayari kwenda kuzikwa
mauti pindi yataponikabili
ni nani atakaeliziba pengo hili
kaditamati mzunguko wa damu umesimama
BURIANI NAAGA MASELAA, KWAHERINI NDUGU JAMAA NA MASELA, ZE FINEST MASELAAA, ASPIRIN MASELAA, LIZZY, AFRODENZI MASELAA, PEARL INVIZIBO MASELAAA, UPOROTO, MTM MASELAAA, NYANI NGABU MASELAAA, HUSNINYO MASELAAA, MICHELLE, BISHANGA MASELAAA, MBU, BJ MASELAAA, NYAMAYAO MASELAAA, WISELADY FIGGANIGGA MASELAAA, NAKADHALIKA MASELAAA.
BURIANI NAWAAGA MI KLOROKWINI, ALAZWE PEMA PEPONI KLOROKWINI, ALAZWE PEMA PEPONI KLOROKWINIII
itakuwa huzuni kwa ndugu na masela, safari yangu itapofika kwenda ahera
pata burudani