Nyie wanawake vipi, tabia mbaya hiyo!

Utakuta mdada kamuona mume/penzi wa rafiki yake anakula raha na mwanamke wa 'pembeni' au wameingia nyumba ya wageni kufanya mapenzi, basi nongwa. Mwanamke roho inamuuma utadhani labda ndo yeye kafumania. Isitoshe rafiki mwenyewe anayemuonea wivu kumuona mpenzi wake akitoka na mwanamke mwingine sio kusema labda ni wa karibu kiviiiiiiiiiile, wamekutana tu mjini.

Cha ajabu atampigia simu shosti mwenzake aje afanye fumanizi ndiyo iwe furaha yake kuona mwanaume kafumaniwa. Baada ya hapo hakuna la maana atakalopata kutokana na 'umbea' wake zaidi ya ndoa ya shosti wake kuingia kidudu mtu na pengine kuvunjika kabisa.

La kushangaza, kwa wanaume ni tofauti kabisa kwani wengi kabla ya kufanya lolote akikuta demu wa mchizi wake anamegwa, wengi huamua kupotezea. Na hofu kubwa kwa wanaume ni kwamba huenda akichoma utambi lisitokee lolote zaidi ya wahusika kumalizana kwa busara na maisha yao yakaendelea kama kawaida-coz kufumaniana siku hizi ni issue ya kawaida sana miongoni mwa wapenzi.

Mimi nadhani kuna haja ya mtu kuendelea na hamsini zako inapotokea unakutana na issue kama hii, maana wengine sio issue kushare mapenzi na wanawake/wanaume tofauti kutokana na makubaliano yao. Usisahau pia kuwa couple zingine hiyo kwao ni ajira kama ajira nyingine. Mind your business

Wewe unasemaje?

Mi nafikiri wanawake wana ushirikiano kwenye mazuri!! ukitakata upendwe na wenzako fanya mazuri.

Sisi midume ushirikiano wetu ni kwenye mabaya tu!! ukitaka upendwe na wenzako fanya mabaya.
 
Umeona eheeee!!....... off topik........sijakuona ndugu yangu, mzima lakini????


Nimeona best, mengine ni makosa yao kabisa tena wanafanya makusudi na hapa wanatafuta justification tu ya ugoni wao!!! Kama wamejiandaa kwenda kuchakachua weekend hii wao waende tu, ila wakumbuke za mwizi ni arobaini na lazima washikwe tu!!

Mbona kuna mwenzao alianzisha uzi humu jinsi ya kumtonya rafiki yake kuwa gal wake anamsaliti na hawajasema au na yeye kawekwa kwenye kundi la wanawake?? WATUACHE JAMANI, anaeogopa kusemewa na asimsaliti mwenzie!!
 
kipipi ni mlinzi sungusungu sahivi yupo kazini. mi naona kikao kihairishwe. sawa katibu eeh?

Asante kwa kuahirisha kikao ndugu m/kiti, naandaa nondo za ukweli! Na ivi lindo la leo ni taiti, nahifadhi hasira kwa atakae tuchokoza kesho nazuka nae!! Wenye waume au vidate vyao naombeni muwatahadharishe, atakae ingilia kumi na nane zetu, namtwika marungu ya kutosha, sihitaji lawama kwa sababu niko kikazi zaidi!! Salute!!!!
 
Sentenso ya tatu from ur bottom ndyoko (forgive my inglish), unadai wengine ni makubaliano yao kuwa na small house. Sasa kama mlishakubaliana na mwenzio unapanic nini? Unatuyeyusha eeh? Utavuna unachopanda rafiki!
 
Back
Top Bottom