Nyie wanawake vipi, tabia mbaya hiyo!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,650
Utakuta mdada kamuona mume/penzi wa rafiki yake anakula raha na mwanamke wa 'pembeni' au wameingia nyumba ya wageni kufanya mapenzi, basi nongwa. Mwanamke roho inamuuma utadhani labda ndo yeye kafumania. Isitoshe rafiki mwenyewe anayemuonea wivu kumuona mpenzi wake akitoka na mwanamke mwingine sio kusema labda ni wa karibu kiviiiiiiiiiile, wamekutana tu mjini.

Cha ajabu atampigia simu shosti mwenzake aje afanye fumanizi ndiyo iwe furaha yake kuona mwanaume kafumaniwa. Baada ya hapo hakuna la maana atakalopata kutokana na 'umbea' wake zaidi ya ndoa ya shosti wake kuingia kidudu mtu na pengine kuvunjika kabisa.

La kushangaza, kwa wanaume ni tofauti kabisa kwani wengi kabla ya kufanya lolote akikuta demu wa mchizi wake anamegwa, wengi huamua kupotezea. Na hofu kubwa kwa wanaume ni kwamba huenda akichoma utambi lisitokee lolote zaidi ya wahusika kumalizana kwa busara na maisha yao yakaendelea kama kawaida-coz kufumaniana siku hizi ni issue ya kawaida sana miongoni mwa wapenzi.

Mimi nadhani kuna haja ya mtu kuendelea na hamsini zako inapotokea unakutana na issue kama hii, maana wengine sio issue kushare mapenzi na wanawake/wanaume tofauti kutokana na makubaliano yao. Usisahau pia kuwa couple zingine hiyo kwao ni ajira kama ajira nyingine. Mind your business

Wewe unasemaje?
 
I can't even imagine how weak this point of urs is! Kama unaogopa kuvunja ndoa yako, why uzini?? Hahahahaaa wanaume bana!!!
 
Wanaume wa JF Leo tumewakosea nini jamani??? Dah!! Thread almost more than ten zooooooote zimetulenga.....
 
kila uzi 'wanawake', back to the topic, anamwita mke aje kufumania ili achukue hava maradhi mengi, na kuna mijanaume hata matumizi ya ndani ada za watoto hatoi kutwa kutapanya kwa mahawara
 
Naomba wanawake wote tukutane usiku tupange mikakati ya kujibu mashambulizi. Imekuwa too much, kila tukibonyeza new posts lazima ukute mnatusema.

Tatizo hamna simile nyie. Mkikuta tu kamba hata iliyoandikwa maalum kwa vidume lazima muikomalie, lol! Hata hivyo mengi yanayosemwa yanawahusu, kweli au si kkweli?
 
Wanaume wa JF Leo tumewakosea nini jamani??? Dah!! Thread almost more than ten zooooooote zimetulenga.....

Jamani shangazi, leo ni wikiend wengine tunatafuta visa humu. mai wife zetu waone michango yetu, wakasirike then mtu ukifika home unakuta mamsapu kanuna taratibu unasepa kwa kisingizio cha kuepusha shari home. Hapo unakuwa umeshapata sababu ya kutoka alone wkiend bila 'mfuasi' kuwa pembeni yako, hahahahahaaaa!
 
Back
Top Bottom