Mkulungwa01
JF-Expert Member
- Jul 14, 2021
- 3,977
- 5,352
Salam nyie wanachuo mnaokuja huku Dar, ushamba wenu wa mikoani muuache Ubungo, wengi mnakuja na ulimbukeni na ushamba mnaishia kupigwa hela na makahaba wa mjini, take care. Soma, fanya vitu vya msingi tulia.
Huku kuna malaya wanajua kuita majina yote mazuri ila inawindwa pochi yako tu, umetoka Busere sere au Moshi vijijini huko, unakuja Dar unajikuta Dar nzima yako, warembo wote wako, shauri yako utalia kilio cha mbwa mwizi.
Wazazi wanahangaika kupika na kuuza mbege, wanauza mashamba ili usome, ila wewe ukifika na jina unabadili unajifanya ni mzaliwa wa Dar, mshua. Be real, soma, fanya vitu smart. Ni hayo tu, msije mkadanganyika nyie mnaotoka mikoani, hii ni DSM. Shauri yenu!!!!!