kyanyangwe
JF-Expert Member
- Oct 31, 2018
- 1,147
- 2,746
Wakuu kwema?
Nimepata safari ya ghafla ya kwenda Moshi ambapo nilitakiwa kuhudhururia shughuli fulani huko kesho kutwa, cha ajabu nimeenda hapo Ubungo nimekuta mabasi yote yamejaa mpaka tarehe 24 mwezi huu.
Nikajipa matumaini ngoja nikakate ticket ya train, napo nimekuta train iko fully mpaka tarehe 24 mwezi huu, basi nikasema ngoja nivunje kibubu ili walau nichukue mwewe, lakini napo kila nikiangalia Air Tanzania, Precision Air na Auric Air na zenyewe ziko fully hadi tarehe 24.
Hapo ikabidi nikae chini kwanza nitafakari, hawa ndugu zetu Wachaga huko kwao wanaenda kufanya nini kikubwa mpaka usafiri unakuwa wa shida namna hii?
Nikaona nimpigie jamaa yangu fulani hivi kumuulizia kama anaweza kuniunganisha na agent yoyote wa mabasi akaniambia maagent anaowajua wote nao wamesharudi kwao Moshi, basi nikaona nidandie usafiri wowote tu, kwa hiyo sasa hivi niko hapa Rombo Kimara navizia Fuso zinazoelekea huko ili niondoke.
Aisee nyie Wachaga noma sana.