Nyerere sitakusamehe hata kidogo

Nyerere sitakusamehe hata kidogo

Mimi sintomsamehe huyo mzee kwa jinsi alivyo wakandamiza wananchi kwa UHUJUMU UCHUMI na KUTAIFISHA MALI ZAO na NYUMBA ZAO
 
Yaani ulikua ndani ya utawala kwa muda mrefu Sana tena Kama miaka 22. Tena kipindi chako Chama kilishika hatamu yaani Chama kimoja.

Ulikuwa na madaraka yote na nguvu nyingi za kutenda na kusema lolote na likafanyika
Lkn ona umeondoka na umeacha mkoa wako pamoja na watu wako wakiwa masikini kabisa.

Hakuna uwanja wa ndege wa maana, Hakuna barabara za maana, Hakuna hospital yoyote ya maana, Hakuna huduma ya maji, umeme shida, shule zenyewe zinatosha, yaani nashindwa hata nisemeje.

Tazama mwenzako wa sasa ndani ya miaka Minne tu kijiji chake kilivyo badilika. Nasema kijiji wala sio mkoa

Tayari ana uwanja wa ndege wa kisasa, hotels kubwa kubwa za kufa mtu, mbuga yake ya wanyama tena ya kulazimisha inaendelea kutangazwa kwa nguvu, traffic light za maana hata Kama Hakuna Magari, umeme na maji ya kumwaga, hospital ya rufaa inajengwa, Benki zinafunguliwa kwa fujo duka kubwa LA dawa MSD, shule zinajengwa na Majengo ya kisasa ya kiutawala

Kwa haya yote kweli Nina haja gani ya kukusamehe wewe?

Ulisahau mchezo kwao hutuzwa hadi ukatuacha katika Hali hii dhaifu?

Mungu akurehemu

Mimi kama Mzalendo halisi wa nchi siwezi kukubaliana na huu ushenxx wako na siwezi kukusamehe kwa kumkashifu Baba wa Taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere(RIP).

Kwa bandiko lako hili unataka kutuaminisha kwamba yale anayofanya Magufuli ya kuleta Ubaguzi na Upendeleo wa waziwazi kwa kuona kwa vile amekuwa ni Rais basi eneo analotoka anataka lineemeke kupitia Madaraka waliyompa Watanzania. Kwako wewe na Magufuli wako mnataka kuleta sera za Kibaguzi, upendeleo na kwa maeneo mnayotoka. Mnasahau kwamba Magufuli aliapa kuilinda na kuitetea Katiba ya JMT na KUWATUMIKIA WATANZANIA WOTE BILA YA KUBAGUA WALA KUANGALIA WAPI ALIKOSA KURA au CCM HAWAKUPATA WABUNGE...!!!

Kinachoendelea kwa sasa katika nji hii ni UBAGUZI WA WAZI wa kuhamisha Fedha za walipa KODI toka maeneo au ngome za UPINZANI na kupeleka majimbo ya UPINZANI...Huu ni umajinuni, uhuni, ubaguzi na udikteta wa mchana kweupe na haustahili kuvumiliwa hata kwa sekunde moya.

Kama Baba wa Taifa angelikuwa na akili kama za babako Magufuli basi Butiama, Musoma na Mkoa wa MARA kwa ujumla ingelikuwa mbali sana ya Dar, Mwanza na Arusha na hata Mikoa mingine isingelikuwa na hali ya Kiuchumi iliyo nayo leo.
Mimi ni muumini wa Baba wa Taifa kwa 99% na huwezi kunitoa hapa.
Hivi CCM wanapotamba kwenye Majukwaa kuwa Tanzania ni nchi ya AMANI, UMOJA, MSHIKAMANO na UTENGAMANO na nchi zingine unafikri nani kaleta hayo matunda kama siyo Mwalimu? Tunachoshudia kwa sasa ni kinyume cha hayo yote. AMANI yetu imeanza kupotea, UMOJA wetu uko mashakani, MSHIKAMANO umebakia kwa MafisCCM na UTENGAMANO na nchi zingine umebakia jina tu kwa baadhi ya nchi zinazoongozwa na Sera ambazo Magufuli alikwenda ku- COPY&PASTE(Rwanda, Burundi, Uganda and the like).

Baba wa Taifa alikuwa na ndoto ya kujenga USAWA KWA WATANZANIA wote, Miji yote,mikoa yote na hatimaye AFRIKA nzima. Mtu mwenye mawazo, hekima na busara kama hizo kamwe huwezi kumlinganisha na Magufuli Mbaguzi, Dikteta na mtu mwenye Chuki kwa Vyama vingine vya Siasa. Mtu kama huyu hawezi kujenga AMANI na Mshikamano asilani!!
 
Mimi sintomsamehe huyo mzee kwa jinsi alivyo wakandamiza wananchi kwa UHUJUMU UCHUMI na KUTAIFISHA MALI ZAO na NYUMBA ZAO

Hivi anachofanya Magufuli leo kwa Wahujumu Uchumi kina tofauti gani na alichokuwa kifanya Baba wa Taifa?
Acheni unafiki enyi Mapoyoyo na Mabazazi wa CCM...!!!
Mwacheni Baba apumzike kwa amani msije mkazidi kujitafutia Laana bure ambayo tayari ina watafuna!!!
 
Sijui kikwete na mwinyi na wao kwao walifanya Kama mkulu!
 
Yaani ulikua ndani ya utawala kwa muda mrefu Sana tena Kama miaka 22. Tena kipindi chako Chama kilishika hatamu yaani Chama kimoja.

Ulikuwa na madaraka yote na nguvu nyingi za kutenda na kusema lolote na likafanyika
Lkn ona umeondoka na umeacha mkoa wako pamoja na watu wako wakiwa masikini kabisa.

Hakuna uwanja wa ndege wa maana, Hakuna barabara za maana, Hakuna hospital yoyote ya maana, Hakuna huduma ya maji, umeme shida, shule zenyewe zinatosha, yaani nashindwa hata nisemeje.

Tazama mwenzako wa sasa ndani ya miaka Minne tu kijiji chake kilivyo badilika. Nasema kijiji wala sio mkoa

Tayari ana uwanja wa ndege wa kisasa, hotels kubwa kubwa za kufa mtu, mbuga yake ya wanyama tena ya kulazimisha inaendelea kutangazwa kwa nguvu, traffic light za maana hata Kama Hakuna Magari, umeme na maji ya kumwaga, hospital ya rufaa inajengwa, Benki zinafunguliwa kwa fujo duka kubwa LA dawa MSD, shule zinajengwa na Majengo ya kisasa ya kiutawala

Kwa haya yote kweli Nina haja gani ya kukusamehe wewe?

Ulisahau mchezo kwao hutuzwa hadi ukatuacha katika Hali hii dhaifu?

Mungu akurehemu
Ndio maana tunamuombea atangazwe mtakatifu maana hakuwa mbinafsi kwa kujipendelea yeye, familia yake, kijiji au mkoa wake, bali alipenda watu wote sawa kiasi cha kusahau kwao. Huyu wa sasa ni mbinafsi, mchoyo, mpenda sifa na visasi kwa watu kiasi cha kudiriki kutoa uhai wa wakosoaji wake
 
Wadau naomba tuwe wa kweli, kwanza chato siyo kijiji kama tunavyo dramatize (kutia chumvi), pili Chato ni sehemu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania hivyo inayo haki ya kuendelezwa kiuchumi na kijamii kama sehemu zingine ikiwemo kupata uwanja wa ndege , benki, shule, hospitali nk, tatu viwanja vya ndege vikubwa havijaanzia wilaya ya Chato vipo wilaya nyingine kama Hai (KIA), Ilemela (Mwanza), Songwe (Songwe), Ilala (JNIA), tano siyo Busara kufunga machimbo mjini Geita na kuanzisha ujenzi wa uwanja wa ndege nk bali kujenga mahali popote ndani ya mkoa husika, sita mbuga ya Burigi na kisiwa cha Rubondo siyo ya Mhe. Magufuli, ilikuwepo , ipo na itaendelea kuwepo, saba Utalii ni jambo la msingi katika awamu hii, sidhani kama channel ya Safari Tanzania inatanganza mbuga hiyo tu , huo ni ubaguzi. Tanzania ni moja.
Kuna shida gani haya yakifanyika huko Chato? Au ulitaka yafanyike Marangu? Sielewi watanzania wanavyolalamika maendeleo chato, kama ni maendeleo chato nayo ina deserve maendeleo, sioni shida ya huo uwanja, sababu tayari utatumika strategically kama uwanja wa mkoa wa geita pia
 
Umenisoma vizuri sio kuwa namlaumu Nyerere Bali nilitaka kuonyesha utofauti wa uongozi kwa ajili ya watu na uongozi kwa ajili ya mtu mbinafsi
Kwa hiyo wa sasa barabara , maji, viwanja vya ndege, shule , miradi na huduma zote za kiuchumi na kijamii hapeleki sehemu zingine za Tanzania?! Je maraisi wengine kwao hawakufanya lolote?! Barabara ya Kwa Mwinyi Dovya ilifuata nini?, Barabara ya Msoga, umeme nk vilifuata nini huko? Lami ya kwanza kuiona mimi ni ya Mwanza Musoma ilifuata nini huko?! Tusiwachimbe viongozi wetu, hakuna aliyemkamilifu na maeneo yao pia yanastahili kupata huduma kama sehemu nyingine za Nchi yetu kabla ,wakati na baada ya viongozi hao kutoka madarakani!
 
Hivi anachofanya Magufuli leo kwa Wahujumu Uchumi kina tofauti gani na alichokuwa kifanya Baba wa Taifa?
Acheni unafiki enyi Mapoyoyo na Mabazazi wa CCM...!!!
Mwacheni Baba apumzike kwa amani msije mkazidi kujitafutia Laana bure ambayo tayari ina watafuna!!!

Poyoyo ni wewe enzi zake huyo wewe ulikua unanyonya maziwa huku sisi kaka zako tukitembea viatu vya makata mbuga,mara elf ya jiwe kuliko hicho kichuguu,kilichokua kikiwaweka watu kizuizini hovyo tu
 
Sijui kikwete na mwinyi na wao kwao walifanya Kama mkulu!

Mzee Mwinyi ni mojawapo ya Marais waliokuwa na hekima na busara sana(Mzee Ruksa). Mzee wa Msoga aliingia kwenye Urahisi akiwa amebakiza ka-imini kadogo sana kalikobakia kutoka kwa Baba wa Taifa. Baadaye alijichanganya na kuzidiwa kete na Mahafidhina wa CCM na akapoteza mwelekeo kabisa....!!

Lakini bado huwezi kuwalinganisha na huyu bazazi Magufuli ambaye anaitawala Tanzania kama vile ni familia ya nyumbani kwake......Ninashangaa sana Rais aliyeapa kuilinda na kuitetea Katiba ya JMT leo anaikanyaga kwa kisigino kwa kupindisha Sheria ili kukidhi matamanio yake huku akizidi kuwaumiza na kuwatesa Watanzania wenzake kwa vile tu ati wako vyama pinzani...Hii ni akili ya matope ambayo inapashwa isafishwe na itakatishwe kwa moto wa chuma cha pua..!!
 
Na uhuru ulipatikana kwa katiba ipi.
Tatizo ninyi kizazi cha sasa ni kufikiri kila kitu kinaenda katiba.
Hisia na uhamasishaji ndio msingi wa siasa zote, katiba ni matokeo.
Mkuu kwani ungeamua kukaa kimya ungepata hasara gani?Maana inaonekana unadhani katiba ni kitabu tu.Mkuu tusipokuwa na sheria nzuri na institutions za kuhakikisha hizo sheria zinafuatwa na kuheshimiwa na kila mtu tunajidanganya wenyewe.Hata maandiko matakatifu yanatuambia amelaaniwa mtu yule anaemtegemea mwanadamu.hakuna nchi iliyowahi kumtegemea mti na ikawa na sustainable development, Ya Libya umeshaona,ya Tanzania unayajua na ya Rwanda utayaona just wait
 
Mzee Mwinyi ni mojawapo ya Marais waliokuwa na hekima na busara sana(Mzee Ruksa). Mzee wa Msoga aliingia kwenye Urahisi akiwa amebakiza ka-imini kadogo sana kalikobakia kutoka kwa Baba wa Taifa. Baadaye alijichanganya na kuzidiwa kete na Mahafidhina wa CCM na akapoteza mwelekeo kabisa....!!

Lakini bado huwezi kuwalinganisha na huyu bazazi Magufuli ambaye anaitawala Tanzania kama vile ni familia ya nyumbani kwake......Ninashangaa sana Rais aliyeapa kuilinda na kuitetea Katiba ya JMT leo anaikanyaga kwa kisigino kwa kupindisha Sheria ili kukidhi matamanio yake huku akizidi kuwaumiza na kuwatesa Watanzania wenzake kwa vile tu ati wako vyama pinzani...Hii ni akili ya matope ambayo inapashwa isafishwe na itakatishwe kwa moto wa chuma cha pua..!!
Wakati huo huo watanzania milioni 55 ambao ndo wenye katiba yao wakiwa either wamelala usingizi mzito au wamekufa kabisa
 
Poyoyo ni wewe enzi zake huyo wewe ulikua unanyonya maziwa huku sisi kaka zako tukitembea viatu vya makata mbuga,mara elf ya jiwe kuliko hicho kichuguu,kilichokua kikiwaweka watu kizuizini hovyo tu

Upoyoyo wa CCM uko dhahiri na kila Mtanzania na Dunia yote inaona mnayowafanyia Watz. Nani asiyejua kinachoendelea Bungeni, Serikalini na Mihimili mingine kama Mahakama?? Bado unaendelea kudhihirisha UPOYOYO wako hapa kwa kujaribu kuaminisha mapoyoyo wenzio kuwa THAMANI YA KATA MBUGA inaweza kulinganishwa na THAMANI ya AMANI, UPENDO na MSHIKAMANO alio turithisha Baba wa Taifa(rip).

Kata mbuga mbona ni vazi la kawaida tu na hate leo hii bado watu wanavaa kata Mbuga tena kwa hiari bila ya kulazimishwa na Magufuli wako?Nenda kwa WAMAASAI uone kama wanavaa raba mtoni leo..!! Ficha na tuondolee upoyoyo wako hapa. Pambaf!
 
Mkuu kwani ungeamua kukaa kimya tungepata hasara gani?Maana inaonekana unadhani katiba ni kitabu tu.Mkuu tusipokuwa na sheria nzuri na institutions za kuhakikisha hizo sheria zinafuatwa na kuheshimiwa na kila mtu tunajidanganya wenyewe.Hata maandiko matakatifu yanatuambia amelaaniwa mtu yule anaemtegemea mwanadamu na ikawa na sustainable development, Ya Libya umeshaona,ya Tanzania unayajua na ya Rwanda utayaona just wait

Sijijui,
Mimi nakuita unajijua,
Hoja yako hapa inaonesha wewe ni mtu unayejijua na kujitambua. Tunahitaji akili kuntu kama hizi ili kuleta mabadiliko katika nji hii ambayo Magufuli na genge lake la CCM wanazidi kuitokomeza gizani badala ya kuirudisha kwene nuru...!!
 
Mkuu kwani ungeamua kukaa kimya tungepata hasara gani?Maana inaonekana unadhani katiba ni kitabu tu.Mkuu tusipokuwa na sheria nzuri na institutions za kuhakikisha hizo sheria zinafuatwa na kuheshimiwa na kila mtu tunajidanganya wenyewe.Hata maandiko matakatifu yanatuambia amelaaniwa mtu yule anaemtegemea mwanadamu na ikawa na sustainable development, Ya Libya umeshaona,ya Tanzania unayajua na ya Rwanda utayaona just wait
Msiojua misingi ya kulianzisha Taifa hili mtaweweseka sana.

Katiba ni muhimu lakini bila kuelewa inapatikana vipi mtahangaika sana.

Hata leo nenda pale Kariakoo muimbie mmachinga juu ya katiba, kama atakuelewa una bahati.

Miaka ya 70s wakati wa Mwalimu ni wasomi wachache sana waliohamasika kumpinga Mwalimu, sembuse katiba.
Na chama kilikuwa kimoja TANU/CCM.

Ni watu wachache zaidi , kama James Mapalala, waliodiriki kuongea juu ya mageuzi ya kisiasa kwa ujumla.

Leo wasomi ni wengi na vyama ni vingi , na vyama vingi vilikuja kwa ruhusa ya Mwalimu.

Mazingira ya leo ukiongelea katiba na mageuzi yake, watu watakuelewa.
 
Kila muwamba ngoma huvutia kwake

Nyerere yeye kipaombele chake ilikua kuikomboa afrika
 
Haya maelezo yako ni ya uongo sana, eti kila Rais, hivi hizo barabara za lami zinazojengwa kila kona ya nchi hii kuna marais na huko? Mtwara iringa wanajenga uwanja mkubwa tu wa ndege, katavi wamejenga kwann chato ambayo ipo mkoa wa geita wasijenge? Utasema wangejenga geita, geita hamna eneo pale ni milima tu, labda wangejenga kuelekea Mwanza ndio unaweza pata eneo la kujenga uwanja wa ndege, sababu ndio utapata maeneo tambalale. Suala la katiba hilo nakuunga mkono , nyerere hapo alichemka.
Aaaaah Geita yote ni milima...aaaaaahaaah
 
Msiojua misingi ya kulianzisha Taifa hili mtaweweseka sana.

Katiba ni muhimu lakini bila kuelewa inapatikana vipi mtahangaika sana.

Hata leo nenda pale Kariakoo muimbie mmachinga juu ya katiba, kama atakuelewa una bahati.

Miaka ya 70s wakati wa Mwalimu ni wasomi wachache sana waliohamasika kumpinga Mwalimu, sembuse katiba.
Na chama kilikuwa kimoja TANU/CCM.

Ni watu wachache zaidi , kama James Mapalala, waliodiriki kuongea juu ya mageuzi ya kisiasa kwa ujumla.

Leo wasomi ni wengi na vyama ni vingi , na vyama vingi vilikuja kwa ruhusa ya Mwalimu.

Mazingira ya leo ukiongelea katiba na mageuzi yake, watu watakuelewa.
Mkuu hapa unataka kuongea nini? kwamba ujinga wa watanzania tulio wengi ndo misingi ya taifa letu au Tanzania ni mali ya nyerere na chama chake? By the way taifa ni nini na taifa la Tanzania lilianzishwa lini na nani?ujinga wetu na uendawazimu wa wachumia tumbo wa ccm usikufanye uone katiba si muhimu.Nchi nyingi zilizopiga hatua kimaendeleo na zenye sustainable development ni zile zilizowekeza kwenye katiba bora yenye institutions imara na independent za kuhakikisha inafuatwa ukilinganisha na shithole zinazotegemea fikra za watu.Hata home kwako kama hauna formula ya maisha na ukakubali kuifuata kwa dhati lazima ufe rofa
 
Back
Top Bottom