Askari Kanzu
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 4,596
- 1,236
Ni wapi "nimeng'ang'ania" magharibi, bi mdogo. Mbona unazidi kuchanganyikiwa?Ndio maana kwanza nikakupa "link" waone Watanzania wengine wanasemaje kuhusu Nyerere ingawa wewe uling'anga'ania "magharibi" na halafu nikakupa "link" umsikilize mwenyewe anasema nini alipokubali kuwa yeye ni dikteta. Na halafu ndio nikakupa hao wa "magharibi" uliong'ang'ania, nilikuwa na maana yangu. Watu kama wewe nawaelewa sana tu, hamnipi shida.
Sasa chaguwa wewe unaloona linakufaa, anayosema FF, wanayosema Watanzania wengine, anayosema Mwenyewe Nyerere au wanayosema wa "magharibi" uliong'ang'ania kuhusu udikteta wa Nyerere. Unalo? Kumbuka, Sikisii!
Waswahili husema "mtoto umleavyo ndio akuavyo". Nadhani hivyo ndivyo alivyolelewa huyu bi mdogo FaizaFoxy. Yaani malezi ya chuki, uongo, unafiki na uzandiki!Ukimchukia ndugu yako unaweza kumuunga mkono hata shetwani iwapo anazungumza lugha moja na wewe... Lakini kumbuka kuwa kazi unayofanya sasa ina malipo yake.... utalipwa! Nakutakia kazi njema na malipo yake pia uje ufurahie .... alamsiki...
FaizaFoxy,
Endelea kutoa Darsa...hakuna anaekuweza kwa hoja..
Ji habari reeeefu halisomeki, wala sina muda wa kulisoma, kwa kifupi:
Kwanza kabisa mimi sikubaliani na hilo "baba" wa Taifa, huo ni ukatoliki na hutumika kanisani kuwaita wachungaji "baba", kumuita "papa" "baba" mtakatifu.
Hii nchi Nyerere aliikuta ina watu wa imani tofauti na ameondoka ametuwacha watu wa imani tofauti, kwanini mtubambikie vyeo vya kikatoliki na Kikristo? hamuoni kuwa huo ni "udini" wa wazi wazi?
Hakuna "baba" wa Taifa, huo ubaba alipewa na nani na kwa ridhaa ya nani? msitujaze ujinga
Kama kawaida yako, bado hujajibu swali!Una matatizo ya kusahau, na hiyo ni moja ya dalili za uzee.
Umesema kweli, lakini malipo ya mwenye chuki yatakaribiana na yale ya sheitwani ... ole wake yeye mwenye chuki ilopindukiaHakuna ambae atakwepa malipo, si mimi si wewe si Nyerere hata mumpe jina lipi. Malipo lazima.
Tutakutana jukwaa la wakubwa tujadili ngono. Kwa sasa nimechoshwa na pumba zako za kujifanya wewe ni Mwislamu safi wakati hakuna ukweli wowote!Huna swali ambalo hujajibiwa unatafuta pakutokea hupapati. Hapa ni "wrong number".
Nilikuwepo wakati wa nyerere, nilikuwa nimeshaanza shule na kuelewa. Na nilipiga kura wakati wa Mwinyi. Nakumbuka miaka ya sabini ilivyokuwa.
Tena Mwalimu Nyerere angekuwa ameshawataifisha watu kama kina RA zamani.
Nyerere wanted what was best for us.
Ila ngoja nikuache na chuki zako binafsi.
Be careful though: the hate in your heart will consume you too.
It is so sad that in this country we still have people worship a dead dictator ...But I have news for you guys , there is nothing and nothing at all that can clean his legacy.
Police brutality that we see today, is a result of his making...Mwenyezi Mungu, atamuonyesha nani hasa baba wa kweli.
Bi mdogo unaboa!Baada ya kukupa aya za Qur'an, nimekushishia nondo kutoka biblia, tazama post #648 sasa wewe amuwa unaifata ipi? au kama unafata matamanio yako huko jukwaa la wakubwa hayo ni yako, mradi uwe umekidhi vigezo. Hapa ni JF na mimi ni FF aka selebriti namba moja JF. Bye.
Na wewe unajiona great thinker, eh?
Nakubaliana na wewe kabisa na hakika Mwalimu ndiye baba wa Taifa wasiokubaliana na hilo wameze wembe...Lakini Nyerere sii baba wa Taifa la kisasa maana Taifa la kisasa lilikuja mwaka 1992 baada ya kuacha kuvunja utawala wa chama kimoja, kufuta Azimio la Arusha na kuondoa miiko na maadili ya uongozi tulipoingia Azimio la Zanzibar. Nchi sii tena ya Wakulima na Wafanyakazi na no one is responsible or accountable - ni RUKSA - Hili ndilo Taifa la kisasa...Mkandara
Inawezekana mnaongea kitu kimoja lakini kwa vipindi tofauti; wakati Mwl. Nyerere anachukua uongozi wa kuliongoza Taifa hili alifanya mabadiliko makubwa ya mwelekeo wa Taifa hili; na alipoachia madaraka viongozi waliofuatia nao waliamua kuendesha nchi kwa mitazamo yao; yapo mambo ya msingi lazima yafanyike ili Taifa liwe na hiyo sifa ya modern nation kuanzia uchumi, kisiasa, kiutamaduni na kidini; ukichulia maana ya modern nation; Tanzania ya wakati wa Mwl. Nyerere ileta maana halisi; hivi sasa Tanzania tunaelekea kwenye Fallen state.
Chama
Gongo la Mboto DSM
Uzuri wako FaizaFoxy una Nyerere wako mwenyewe mbali na huyu tunaemfahamu. Endelea tu dada kutoa maoni yako kwa uhuru mpana kabisa wa JF. Tunaomfahamu Mwalimu hatuna tatizo nawe ati. Jana ulikwenda kuchangia TV IMANI?Unafikiri wote wanataifishika? kwani hao kina RA hawakuwepo wakati huo? uliza kama huelewi.
Ukimaliza uliza kisa cha LONRHO au Tiny Rowlands na Nyerere. Si wote wanataifishika, alijidai kumtaifisha Tiny Rowlands, mwenyewe akarudisha baada ya kuona mnhhhh hapa pagumu. Si kila mtu aliweza kumchezea anavyotaka. Alisema nikigeuka nyuma ntageuka jiwe, Tiny akamfanya alambe matapishi yake.
Hakuna chuki binafsi kuna ukweli tu hapa, kama una mbadala tueleze. Nyinyi ndio wale mna macho lakini hamuoni, mna masikio lakini hayasikii. Mmejazwa ujinga na mnaukubali bila kutazama upande mwingine, kwangu hilo ni NO.
Na kama huna hoja za kupingana na niliyoyasema bora ujinyamazie tu. Kwani nna uhakika huwezi kuufuta ukweli, ukweli upo na utazidi kuonekana kila siku zinavyokwenda. Sana sana utaanza FaizaFoxy hivi FaizaFoxy vile kama wenzio wengine. Si unawaona hapa?
kwanza, lazima nikiri kwamba hoja yangu ya msingi kuhusu heshima ya baba wa taifa kutambulika kwa mujibu wa sheria, ilikuwa dominated zaidi na passion and feelings, with minimum facts, kwani sikueleza bayana sheria ipi inamtambua mwalimu kama baba wa taifa. Mniwie radhi kwa hilo. All that being said, majibu ya wana historia hapo juu ni ishara kwamba, kwa mtu mzalendo wa taifa hili, hana haja ya kutumia akili ya ziada kuhoji facts, au kupitia utafiti unaohitaji a certain methodology kufikia conclusion kwamba mwalimu nyerere anatambulika na bunge, kwa mujibu wa sheria (tafadhali rejea jibu la nne, tano, na sita la historian hapo juu).
bwana mchambuzi, kwanza naomba nikupongeze kwa kuwa muungwana, kwa kukiri pale ulipokosea, hivi ndivyo kijiwe chetu cha jf kinavyotakiwa kiwe!. Ni vyema next time ukaja na facts badala ya passion na emotion, wengi tunamkubali mwalimu lakini tunataka ifahamike wazi kwamba historia ya tanzania nyuma yake wapo watu wengi na wala siyo one man show.
Hata hivyo, kutamkwa kwa jina "baba" wa taifa ndani ya bunge bila kipingamizi haimaanishi nguvu ya kisheria ya jina hilo, au jambo hilo!. Bungeni kuna taratibu mbalimbali za kufuata ili kulipa jambo nguvu za kikanuni/kisheria.
Kwa mantiki hiyo basi, nasema kwamba tanzania tuna "mababa"/ mama wa taifa wengi, mwalimu akiwa mmojawapo, wengine miongoni mwao ni kama mzee karume, kawawa, wale 17 aliowataja jk, na wale waadilifu waliofanya kazi ya kusimika misingi ya taifa letu kama sokoine etc.
Hawa ndiyo founding fathers/ fathers of the nation.
Hata hivyo, kutamkwa kwa jina "baba" wa taifa ndani ya bunge bila kipingamizi haimaanishi nguvu ya kisheria ya jina hilo, au jambo hilo!. Bungeni kuna taratibu mbalimbali za kufuata ili kulipa jambo nguvu za kikanuni/kisheria.
Public Holidays Act.bwana mchambuzi, kwanza naomba nikupongeze kwa kuwa muungwana, kwa kukiri pale ulipokosea, hivi ndivyo kijiwe chetu cha jf kinavyotakiwa kiwe!. Ni vyema next time ukaja na facts badala ya passion na emotion, wengi tunamkubali mwalimu lakini tunataka ifahamike wazi kwamba historia ya tanzania nyuma yake wapo watu wengi na wala siyo one man show.
Hata hivyo, kutamkwa kwa jina "baba" wa taifa ndani ya bunge bila kipingamizi haimaanishi nguvu ya kisheria ya jina hilo, au jambo hilo!. Bungeni kuna taratibu mbalimbali za kufuata ili kulipa jambo nguvu za kikanuni/kisheria.
Kwa mantiki hiyo basi, nasema kwamba tanzania tuna "mababa"/ mama wa taifa wengi, mwalimu akiwa mmojawapo, wengine miongoni mwao ni kama mzee karume, kawawa, wale 17 aliowataja jk, na wale waadilifu waliofanya kazi ya kusimika misingi ya taifa letu kama sokoine etc.
Hawa ndiyo founding fathers/ fathers of the nation.
Baada ya kukupa aya za Qur'an, nimekushishia nondo kutoka biblia, tazama post #648 sasa wewe amuwa unaifata ipi? au kama unafata matamanio yako huko jukwaa la wakubwa hayo ni yako, mradi uwe umekidhi vigezo. Hapa ni JF na mimi ni FF aka selebriti namba moja JF. Bye.
Kipande hiki nimekipenda sana na hakika nitachangia kwa wale wasiojua mahesabu ili wapate kujua kama kweli tulishindwa ama kulichangiwa sababu nyingine kabisa..Ndugu zetu mnaomkejeli Mwalimu, hoja zenu kwamba Ujamaa umetupotezea muda, Je wenzetu hapo juu wameutumiaje muda huo? Je, hii haitoshi kuwaonyesha kwamba kuna mdudu hapa ambae ni common kwetu sote ambae anatufana, bila ya kujali Ujamaa au Soko Huru? Ndio maana Mwalimu anabakia kuwa Rais Bora wa Tanzania mbali ya kuwa baba wa taifa kwa sababu alithubutu kujaribu geuza madudu haya, kwa kulipa taifa letu a self determination chini ya Ujamaa na Kujitegemea. Kilichomshinda Mwalimu ni uchanga wan chi kuweza kuzalisha kwa wingi na wakati huo huo kutimiza ahadi za uhuru – ajira kwa wote, huduma bora kwa wote. Angalau alishindwa lakini hakuwasaliti na ahadi zake za wakati wa uhuru. Mbali ya hili na pia utekelezaji mbaya wa sera, sababu za kushindwa pia ni kutokana na unduminakwili wa baadhi ya watendaji wake ambao walikuwa wanashirikiana na mabepari wa nje, na hatimaye kumshinda nguvu. Nyerere bado ni Rais bora kutokana na ukweli kwamba alishindwa kwa sababu za maadui (ukiachilia utekelezaji mbovu wa sera); Bado Nyerere ni Rais bora kwani hata nchi za nje zilimpa heshima ya kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kusini – South Commision, hata baada ya Ujamaa kushindwa, kwa kutambua kwamba ana uwezo wa kuziletea nchi zote maskini mwongozo wa jinsi gani ya kupambana na mfumo wa uchumi wa kimataifa usio wa haki.