Nyerere na uhuru wa zimbabwe

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,558
25,322
Wakuu magwiji wa historia, nimekutana na ubishi mkubwa sana, kuna mtu amedai kuwa hayati Julius Kambarage Nyerere, aliyekuwa Rais wa jamuhuri wa Tanzania hakuhudhuria sherehe za uhuru wa Zimbabwe, nakualikeni mnaoijua historia mtuondolee utata huu, watu wanaweza kung'oana macho mkichelewa kuleta jibu au hata ikiwezekana kapicha ka mnato.
 
TANZANIA: PRESIDENT NYERERE THANKS BRITAIN FOR ITS | Archive Footage | ITN Source

Siku ya Uhuru Nyerere alituma salamu kutoka mkutano wa hadhara uliofanyika Dar.

Hebu jaribuni ku google kwanza...

Wakuu,
Nawashukuru sana kwa michango yenu, sana zaidi Kiranga, link uliyotoa inamaliza kiu ya swali. Mkuu Mundu umetoa pendekezo murua,

Lakini inaonekana Nyerere aliogopa makaburu ambao kwa zimbabwe alihisi ingekuwa karibu na rahisi makaburu kumdhuru kupitia mamluki. Ama duru zinasemaje! Kulikuwa na majukumu mengine ya kitaifa ama aliamua kusherehekea uhuru ule pamoja na watanzania wenzake kuonyesha mshikamano pamoja nao akizingatia kuwa kuna damu wa watanzania ilimwagika kwa gharama ya uhuru wa zimbabwe!
 
Last edited by a moderator:
jogi, Mundu,

..kuna kipande cha habari toka blog ya Madaraka Nyerere ambacho kina-suggest kwamba Mwalimu alikuwepo Harare siku Zimbabwe inapewa uhuru. fuata link niliyoiweka hapa chini.
From Butiama and beyond...: Visitors to Butiama: Ayoub 'Rasta' Laizer
JokaKuu, habari ya Madaraka Nyerere ni ya kusimuliwa, ushahidi uliowekwa na mkuu Kiranga unajieleza dhahiri kuwa nyerere alisherehekea uhuru wa zimbabwe kwa kuhutubia mkutano wa hadhara jijini dar es salaam. Kama anaweza kutuwekea link ama picture atakuwa kafanya jambo jema.
 
Last edited by a moderator:
jogi,

..huenda Madaraka Nyerere amekosea.

..lakini wewe subiri tu hapa JF ni jungu kubwa utapata jibu la uhakika.

nakala:
Jasusi, Kudi Shauri

Siku ya uhuru wa Zimbabwe Mwalimu alikuwa Dar-es-Salaam. Tanzania siku hiyo ilisherehekea kwa kutangaza siku kuu na Mwalimu alihutubia kwenye sherehe hizo. Mwalimu alienda Zimbabwe baadaye akiwa mgeni wa kwanza rasmi wa serikali ya Zimbabwe baada ya uhuru. Lakini siku ya uhuru alikuwa Dar-es-Salaam. Kiranga you are right on the money.
 
na kuhusu Bob Marley, Madaraka is wrong again. Mwalimu was aware of Marley as early as 1975 alipokwenda state visit Jamaica. Mwalimu may not have been aware of Marley's lyrics for sure lakini wakati wa ziara hiyo msafara wa Mwalimu ulitekwa na wananchi waliosindikiza motorcade ya Mwalimu kutoka airport mpaka Kingston na mbele ya msafara huo alikuwa ni Bob Marley na Wailers. So he was aware of who Bob Marley was.
 
jogi,

..OK, jibu tunalo sasa kwamba kweli Mwalimu hakwenda Harare kwenye sherehe za uhuru.

Jasusi,

..sasa hizi habari za Nyerere na Bob Marley zinatokea wapi?

..wengine wamekwenda mbali mpaka kudai Nyerere alikataa kumpa mkono Bob Marley!!
 
jokaKuu,
Ukishakuwa mtu mashuhuri lazima kuwepo na stori za vijiweni. Ni kama ile stori ya Nyerere kumpa Malkia Elizabeth kifimbo chake badala ya kushika mkono wake. Nina hakika umeshasikia stori nyingi juu ya Kawawa.
 
Siku ya uhuru wa Zimbabwe Mwalimu alikuwa Dar-es-Salaam. Tanzania siku hiyo ilisherehekea kwa kutangaza siku kuu na Mwalimu alihutubia kwenye sherehe hizo. Mwalimu alienda Zimbabwe baadaye akiwa mgeni wa kwanza rasmi wa serikali ya Zimbabwe baada ya uhuru. Lakini siku ya uhuru alikuwa Dar-es-Salaam. Kiranga you are right on the money.

Nyerere hakwenda kwenye uhuru wa Zimbabwe. Alikwenda baadaye ziarani. Nasikia alimwambia Mugabe: 'You have inherited a jewel, keep it that way.'
 
Mkuu wa accurate data...siku zote huwa hakuna wa kuzipinga. Itakuwa vizuri kama utaandika kitabu cha mengi unayoyafahamu kuhusu Tanganyika/Tanzania.

jogi,

..OK, jibu tunalo sasa kwamba kweli Mwalimu hakwenda Harare kwenye sherehe za uhuru.

Jasusi,

..sasa hizi habari za Nyerere na Bob Marley zinatokea wapi?

..wengine wamekwenda mbali mpaka kudai Nyerere alikataa kumpa mkono Bob Marley!!
 
Nyerere hakwenda kwenye uhuru wa Zimbabwe. Alikwenda baadaye ziarani. Nasikia alimwambia Mugabe: 'You have inherited a jewel, keep it that way.'
Kama aliyasema hayo basi ni maneno ya kisiasa kutoka kwa mwanasiasa! hivyo hayana uzito wowote kwangu mimi.
Ningependa kujua sababu zilizomfanya kwa nini asiende Zimbabwe siku ya Uhuru?
 
jokaKuu,
Ukishakuwa mtu mashuhuri lazima kuwepo na stori za vijiweni. Ni kama ile stori ya Nyerere kumpa Malkia Elizabeth kifimbo chake badala ya kushika mkono wake. Nina hakika umeshasikia stori nyingi juu ya Kawawa.

Najua hii utaipiga chenga. Je kwanini JKN alitengana na mama Maria?
 
BAK,

..Thank u.

..I try to be accurate lakini mara nyingine huwa nachemsha.

..In this particular case, kidogo niingie mkenge wa kuanza kubishana na Kiranga.

..namshukuru Jasusi kwa kuni-bail out. LOL!!

NB:

..ila kuna watu wameshatoana ngeu hapa JF kwa kubishana kwamba Mwalimu alikataa kumpa mkono Bob Marley siku ya uhuru wa Zimbabwe.

..sasa imejulikana kwamba habari hiyo ni URONGO kwasababu Mwalimu siku hiyo tajwa alikuwa Dar-Es-Salaam.

..mimi nasema u can lie anywhere else but not at JF.
 
Last edited by a moderator:
Kama aliyasema hayo basi ni maneno ya kisiasa kutoka kwa mwanasiasa! hivyo hayana uzito wowote kwangu mimi.
Ningependa kujua sababu zilizomfanya kwa nini asiende Zimbabwe siku ya Uhuru?

Maneno haya yana uzito mkubwa. Hila kuyazungumza ni kutoka nje ya mada.
 
BAK,

..Thank u.

..I try to be accurate lakini mara nyingine huwa nachemsha.

..In this particular case, kidogo niingie mkenge wa kuanza kubishana na Kiranga.

..namshukuru Jasusi kwa kuni-bail out. LOL!!

NB:

..ila kuna watu wameshatoana ngeu hapa JF kwa kubishana kwamba Mwalimu alikataa kumpa mkono Bob Marley siku ya uhuru wa Zimbabwe.

..sasa imejulikana kwamba habari hiyo ni URONGO kwasababu Mwalimu siku hiyo tajwa alikuwa Dar-Es-Salaam.

..mimi nasema u can lie anywhere else but not at JF.

Baada ya kufa kwa Bob Marley. Kuna kitabu kilitolewa Tanzania kuhusu wasifu wa Bob. Na kuna picha iliyoonyesha Mwalimu na Bob na hiyo ilifanyika Jamaica.

Mwalimu kutokwenda Zimbabwe zilikuwa ni sababu za ki-protocol tu. Alikuwa ni mwenyekiti wa nchi za mstari wa mbele. Na siku aliyofanya ziara Zimbabwe ilikuwa kama sherehe za uhuru.
 
Najua hii utaipiga chenga. Je kwanini JKN alitengana na mama Maria?

Zakumi,
Siyo kuchenga. I honestly do not know why. Nilisikia rumours tu kwamba alimrudisha Mama Maria kwao for a long time mpaka UWT (Umoja wa Wanawake) wakaomba kikao naye kuhusu suala hilo. Lakini sijui kabisa kilichopelekea mkasa huo.
The only person who I know may know is Butiku, but I doubt that he would be willing to talk about it.
 
Its obvious mwalimu hakuwa vasco da gama. Pamoja na sifa zote za uhuru wa zimbabwe still hakwenda kwenye sherehe? Viongozi wa zamani walikuwa na intention tofauti kabisa.
I love the song by marley ya 'zimbabwe'.
 
Back
Top Bottom