Nyerere na maendeleo ya Butiama

Nyerere na maendeleo ya Butiama

mafutamingi

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2011
Posts
2,775
Reaction score
2,198
Mwalimu Julius Nyerere katika kipindi chote cha uongozi wake alikataa kata kata kuigeuza Butiama ionekane kwamba pale ndipo nyyumbani kwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania.

Kwa mfano Mara kwa mara kulikuwa na mipango au hata shinikizo kutoka serikalini kujenga barabara ya lami hadi Butiama. Lakini kila mara suala la barabara ya lami lilipoibuliwa, Mwalimu aliendelea na msimamo wake.

Wakati fulani pendekezo hilo lilipomfikia aliuliza - "mnataka barabara ya lami iende kufuata nini Butiama? Kuna nini huko? Hakuna zao lolote la biashara huko. Hakuna kahawa, pamba, n.k.

Kuna mihogo tu! Sasa barabara ya lami iende kufanya nini!" Kwa hiyo Butiama iliendelea bila kuwa na barabara ya lami hadi alipofariki. Baada ya kifo chaketu Rais Mkapa akaweka lami.

Ifahamike kwamba Butiama iko takribani Km 15 kutoka Kiabakari ambapo barabara kuu itokayo Musoma kwenda Mwanza inapita. Lakini hii isitafsiriwe kwamba Mwalimu hakupenda maendelea ya Butiama.

Alipenda sana maendeleo na ndiyo maana aliweka mradi wa kilimo cha umwagiliaji pale Kyarano - jirani tu na Butiama. Kuna wanaomsifu kwamba alikuwa kielelezo cha kiongozi ambaye hajipendelei.

Lakini pia kuna wanaomlaumu kwamba alisahau nyumbani kwao kwa sababu "charity starts at home"! Kundi hili pia linasema hata Yesu alipowa wanafunzi wake kazi ya kueneza injili aliwaambia waanzie Yerusalemu. Wewe wasemaje kuhusu hili?
 
Kiuchumi, ukiweka lami eneo ambalo lina mazao ya uchumi, uwekezaji huo unaweza kuongeza uchumi na mapato, kiasi cha kukuwezesha kuendelea kuongeza miundombinu mpaka sehemu ambazo hazina mazao ya uchumi.

Kwa hiyo, ingawa sehemu zote zinaweza kuwa zinatakiwa kuletewa maendeleo kama barabara ya lami, lakini sehemu zinazozalisha sana zikipewa kipaumbele, kwa kuwa kipaumbele hicho kitaongeza uzalishaji, utakuwa unarahisisha na unaharakisha maendeleo ya sehemu zote kwa kuanza na sehemu hizi zenye mazao ya uchumi.

Kiswahili tunasema "Kupanga ni kuchagua". Ukianza kuweka barabara ya lami sehemu wanayolima mihogo, badala ya sehemu wanayochimba dhahabu, utashindwa kurahisisha uchimbaji wa dhahabu, ambao utasaidia sana hata kukuwezesha kuweka lami sehemu kumi zinazolima mihogo kwa haraka Zaidi.

Nafikiri ndicho alichokataa Nyerere hicho. Si kwamba alikataa Butiama kusiwe na maendeleo.

Ila, kwa nchi yenye sehemu nyingi zenye uwezekano wa kuwa na mazao yenye kuongeza uchumi sana zaidi ya Butiama, kwa nini aanze kuweka lami Butiama, lami ambayo haitakuwa na uzalishaji wowote, wakati anaweza kuweka lami sehemu nyingine, ikawa na uzalishaji mzuri utakaosaidia kuweka lami sehemu kumi kama Butiama?

Ukisoma kitabu cha maisha ya awali ya Nyerere "Nyerere: The Early Years" cha Dr. Thomas Molony wa Edinburgh aliposomea Nyerere, utasoma mpaka Nyerere alivyokuwa Edinburgh alisoma nini, papers alizoandika zilihusu nini. Mmoja kati ya wanafalsafa ambao Nyerere alimsoma sana na kuandika sana insha juu yake ni John Stuart Mill.

John Stuart Mill alikuwa ni Utilitarianist. Utilitarians wanaamini katika kanuni ya "The greater good for the greater number of people". Yani, ufanye jambo litakaloleta manufaa kwa watu wengi zaidi.

Kwa kanuni hizi za kufanya jambo litakaloleta manufaa kwa watu wengi zaidi, kuanza kuleta maendeleo sehemu zenye kuweza kujenga uchumi zaidi kunafaa watu wengi zaidi ya kujenga sehemu ambazo zina watu wachache na kuzijenga hakuwezi kufaidisha watu wengi zaidi.

Ndiyo maana Nyerere akauliza, ajenge lami Butiama kuna zao gani?
 
Nyerere pamoja na mapungufu yake mengi alikuwa ni kiongozi pekee mzalendo katika taifa hili changa na maskini.

Waliofuata toka awamu ya pili hadi hii ya sasa ni wapiga madili tu.
 
Kwa hiyo Nyerere aliamini kazi ya Lami ni kusafirisha mazao ya biashara pekee?
 
1147481
 
Sasa mm Mambo ya kale nasemaje...

Mzalendo pekee tangu uhuru alikua Nyerere. Mtu ambae hakujenga kwake, watu wake wakabaki nyuma kimaendeleo na familia yake yy mwenyewe hakuwaandalia mazingira ya kumrithi....akaenda kujenga kwa watu (maeneo) wengine wakaendelea kiwazidi wati wake.

Na hii ndo watu wa Musoma wanamlaani huyu mzee. Alikua mtu mpenda nchi yake...aliipenda Tz, hakujimilikisha mali. Akasema watz bado hawana elimu...akawekeza kwenye elimu ilo watu wake wasome waje kutumia mali za Tz kwa maarifa. Lakn maskini alishindwa kulitabiri hili.

Ukiskia mtu mwingine anajiita "Mzalendo" ujue huyo ni muongo, mnafiki, mpenda sifa, na pengine ni wa kupuuzwa.

Wazalendo walishakufa....Nyerere, Nkurumah, Mandela etc.
 
Yani mtoa mada sijui nia yako ni kutaka ku justify nini,hasa unaposema nyerere alipenda maendeleo na kuanzisha mradi wa umwagiliaji kyarano?? Hivi huo mradi wa kyarano nao ulitumia mabilioni ya pesa nje ya budget ya serikali kama ilivyo miradi anayoanzisha magufuli chato au miradi aliyopeleka mkapa na kikwete makwao.
 
Kiuchumi, ukiweka lami eneo ambalo lina mazao ya uchumi, uwekezaji huo unaweza kuongeza uchumi na mapato, kiasi cha kukuwezesha kuendelea kuongeza miundombinu mpaka sehemu ambazo hazina mazao ya uchumi.

Kwa hiyo, ingawa sehemu zote zinaweza kuwa zinatakiwa kuletewa maendeleo kama barabara ya lami, lakini sehemu zinazozalisha sana zikipewa kipaumbele, kwa kuwa kipaumbele hicho kitaongeza uzalishaji, utakuwa unarahisisha na unaharakisha maendeleo ya sehemu zote kwa kuanza na sehemu hizi.

Kiswahili tunasema "Kupanga ni kuchagua". Ukianza kuweka barabara ya lami sehemu wanayolima mihogo, badala ya sehemu wanayochimba dhahabu, utashindwa kurahisisha uchimbaji wa dhahabu, ambao utasaidia sana hata kukuwezesha kuweka lami sehemu kumi zinazolima mihogo kwa haraka Zaidi.

Nafikiri ndicho alichokataa Nyerere hicho. Si kwamba alikataa Butiama kusiwe na maendeleo.

Ila, kwa nchi yenye sehemu nyingi zenye uwezekano wa kuwa na mazao yenye kuongeza uchumi sana Zaidi ya Butiama, kwa nini aanze kuweka lami Butiama, lami ambayo haitakuwa na uzalishaji wowote, wakati anaweza kuweka lami sehemu nyingine, ikawa na uzalishaji mzuri utakaosaidia kuweka lami sehemu kumi kama Butiama?

Ukisoma kitabu cha Maisha ya awali ya Nyerere "Nyerere: The Early Years" cha Dr. Thomas Molony wa Edinburgh aliposomea Nyerere, utasoma mpaka Nyerere alivyokuwa Edinburgh alisoma nini, papers alizoandika zilihusu nini. Mmmoja kati ya wanafalsafa ambao Nyerere alimsoma sana na kuandika sana insha juu yake ni John Stuart Mill.

John Stuart Mill alikuwa ni Utilitarianist. Utilitarians wanaamini katika kanuni ya "The greater good for the greater number of people". Yani, ufanye jambo litakaloleta manufaa kwa watu wengi Zaidi.

Kwa kanuni hizi za kufanya jambo litakaloleta manufaa kwa watu wengi Zaidi, kuanza kuleta maendeleo sehemu zenye kuweza kujenga uchumi Zaidi kunafaa watu wengi Zaidi ya kujenga sehemu ambazo zina watu wachache na kuzijenga hakuwezi kufaidisha watu wengi Zaidi.

Ndiyo maana Nyerere akauliza, ajenge lami Butiama kuna zao gani?
Ninakubalina na wewe korosho ni zao kuu la biashara barabara ya lami ilipaswa kuwa kusini
 
Nyerere wakati huo nchi ilikuwa changa na haina mtoto hata mmoja sasa tz imekua mpaka ina vitukuu , maemdeleo haya vyama ni wivu tu unakusumbua acha magu aitwe magu
 
Sipati picha Magufuli ndiye angekuwa rais mara baada ya Wakoloni kuondoka. Sijui hii Tanzania au Tanganyika kama bado ingekuwepo kama ilivyo.
 
Our times are different from Nyerere's time. Whether we like or not, we need to connect the whole country in such a way that we can have better options, when it comes to tapping the resources and other opportunities.
Nyerere aliisahau kabisa Lindi na Mtwara sababu ya security wakati ule. Leo ni tofauti.
Kama means za kusukuma maendeleo zikisambazwa Tanzania nzima, umaskini utapungua na fursa zitakuwa rahisi kwa kila mwananchi.
Tusifikirie kama tupo kwenye box. Tanzania is evolving like any other country
 
Kiuchumi, ukiweka lami eneo ambalo lina mazao ya uchumi, uwekezaji huo unaweza kuongeza uchumi na mapato, kiasi cha kukuwezesha kuendelea kuongeza miundombinu mpaka sehemu ambazo hazina mazao ya uchumi.

Kwa hiyo, ingawa sehemu zote zinaweza kuwa zinatakiwa kuletewa maendeleo kama barabara ya lami, lakini sehemu zinazozalisha sana zikipewa kipaumbele, kwa kuwa kipaumbele hicho kitaongeza uzalishaji, utakuwa unarahisisha na unaharakisha maendeleo ya sehemu zote kwa kuanza na sehemu hizi.

Kiswahili tunasema "Kupanga ni kuchagua". Ukianza kuweka barabara ya lami sehemu wanayolima mihogo, badala ya sehemu wanayochimba dhahabu, utashindwa kurahisisha uchimbaji wa dhahabu, ambao utasaidia sana hata kukuwezesha kuweka lami sehemu kumi zinazolima mihogo kwa haraka Zaidi.

Nafikiri ndicho alichokataa Nyerere hicho. Si kwamba alikataa Butiama kusiwe na maendeleo.

Ila, kwa nchi yenye sehemu nyingi zenye uwezekano wa kuwa na mazao yenye kuongeza uchumi sana Zaidi ya Butiama, kwa nini aanze kuweka lami Butiama, lami ambayo haitakuwa na uzalishaji wowote, wakati anaweza kuweka lami sehemu nyingine, ikawa na uzalishaji mzuri utakaosaidia kuweka lami sehemu kumi kama Butiama?

Ukisoma kitabu cha Maisha ya awali ya Nyerere "Nyerere: The Early Years" cha Dr. Thomas Molony wa Edinburgh aliposomea Nyerere, utasoma mpaka Nyerere alivyokuwa Edinburgh alisoma nini, papers alizoandika zilihusu nini. Mmmoja kati ya wanafalsafa ambao Nyerere alimsoma sana na kuandika sana insha juu yake ni John Stuart Mill.

John Stuart Mill alikuwa ni Utilitarianist. Utilitarians wanaamini katika kanuni ya "The greater good for the greater number of people". Yani, ufanye jambo litakaloleta manufaa kwa watu wengi Zaidi.

Kwa kanuni hizi za kufanya jambo litakaloleta manufaa kwa watu wengi Zaidi, kuanza kuleta maendeleo sehemu zenye kuweza kujenga uchumi Zaidi kunafaa watu wengi Zaidi ya kujenga sehemu ambazo zina watu wachache na kuzijenga hakuwezi kufaidisha watu wengi Zaidi.

Ndiyo maana Nyerere akauliza, ajenge lami Butiama kuna zao gani?
Ahsante sana kwa uchambuzi mzuri.
 
Our times are different from Nyerere's time. Whether we like or not, we need to connect the whole country in such a way that we can have better options, when it comes to tapping the resources and other opportunities.
Nyerere aliisahau kabisa Lindi na Mtwara sababu ya security wakati ule. Leo ni tofauti.
Kama means za kusukuma maendeleo zikisambazwa Tanzania nzima, umaskini utapungua na fursa zitakuwa rahisi kwa kila mwananchi.
Tusifikirie kama tupo kwenye box. Tanzania is evolving like any other country

But it will remain the standing ruins when his time is over.
 
Hapo tunafunzwa tusiwe watu wa kujipendelea na kujiangalia sisi kama sisi (tusiwe na ubinafsi)!!

Wapendelee wengine kwanza ndio baadae uje kwako mwishoni!!!
 
Back
Top Bottom