Ningependa kujua ni sababu gani iliyomfanya Nyerere ajikite zaidi katika juhudi za ukombozi wa bara la Afrika kiasi cha kumfanya atumie muda mwingi, rasilimali za Taifa na maisha ya Watanzania huku ikijulikana wazi kuwa kama vile ambavyo Tanganyika ilipewa Uhuru pamoja na nchi nyingine kabla yake, hivyohivyo nchi nyingine zilizosalia zingepewa tu Uhuru wao wakati ukifika.
Hivi kulikuwa na haja gani kwa Nyerere kujikita namna ile?
Wakati nchi nyingine zikiona hakuna umuhimu wa kuwekeza nguvu nyingi kwenye ukombozi wa Afrika (mfano Wakenya) na kuwa bize katika kuimarisha Uchumi wao Nyerere alikuwa bize kwenye "ukombozi wa Afrika"!(usishangae sasa ni kwa nini Kenya imeipita Tanzania ambayo ilipata Uhuru kabla ya Kenya).
Swali: hivi kweli Nyerere alikuwa ni mpigania Uhuru wa Bara la Afrika? au kuna vitu vingine nyuma ya pazia kama vile ambavyo inatajwa kuwa alikuwa akitumiwa kuwadhibiti wapigania Uhuru?
Tafadhali wajuvyi wa haya masuali nijuzeni.
======
Moderator:
Tunapendekeza msomaji kusoma matundiko haya:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...m/20575-nyerere-and-africa-end-of-an-era.html
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-with-julius-nyerere-on-anti-colonialism.html
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...g-hero-of-africa-who-made-nelson-mandela.html