Nyerere hakukosea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyerere hakukosea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ustaadh, Nov 8, 2009.

 1. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2009
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  "Inawezekana tatizo la paka kwa panya lingekwisha kama paka angefungiwa kengele shingoni: taabu ni kumpata panya wa kuifanya kazi hiyo. Na panya watakuwa wajinga sana wakidhani kuwa paka watajifunga au watafungana kengele shingoni" - Mwl. J. K. Nyerere

  MWALIMU NYERERE ALIKUWA SAHIHI, TUSITARAJIE KUWA CCM WATAONDOKA MADARAKANI KWA KWA HIARI YAO WENYEWE. NI LAZIMA TUKUBALI GHARAMA YA "PANYA KUMFUNGA PAKA KENGELE". MABADILIKO LAZIMA YATOKEE KWA GHARAMA YOYOTE ILE ILI KUINUSURU NCHI YETU VINGINEVYO TUTAENDELEA KULIA NA KUSAGA MENO!
   
 2. S

  Shamu JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nyerere ndiye aliyesababisha hii CCM itawale milele. Ni makosa kumtumia Nyerere as an example leader.
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Shamu,
  Lakini CCM ya leo si ile aliyoiasis JKN. Hawana uadilifu, hawana upendo wa watu, hawana mwelekeo.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Wewew ni Fisadi wa Mawazo , na una chuki binafsi na wivu!

  Mtu yeyote mwenye akili za kawaida anaona wazi utofauti wa uongozi kati ya enzi hizo mbili...wewe unaishi wapi?

  Nyerere alisababisha vp CCm itawale milele?

  Au huwa anakuja siku ya kura kama jinamizi na
  kukulazimisha uipigie kura sisiemu?...Tueleze mwenzetu inakuwakuwaje!
   
 5. O

  Ogah JF-Expert Member

  #5
  Nov 8, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  si "mapaka" tena bali ni "mambwa".......kaaazi kweli kweli
   
 6. S

  Shamu JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Why he chose to change the constitution in order to benefit one party? Tofauti kubwa ya Nyerere na viongozi wa sasa hivi ni kwamba, now we live on open society, democracy, freedom, and freedom of press. There were a lot of bad things that happened when Nyerere was a leader. Hakuna mtu au kiongozi aliyethubutu kuripoti, au kuzungumza jambo lolote baya linalohusu CCM.
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Nov 8, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Shamu,
  Nani alikushika mdomo wakati huo? Mbona wengine tulikuwa tunazungumza na bado tunadunda?
   
 8. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #8
  Nov 8, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  Jasusi,

  Nyerere alichangia kwa kiasi kidogo yote yaliyopo sasa hivi. Aliwaamini mbwa mwitu.. angewachnguza kidogo angebaini.... uwezo alikuwa nao.
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Nov 9, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  FairPlayer,
  Ningekubaliana na wewe kama sote tungejua mapema kuwa Mkapa angebadilika na kuwa fisadi. Watu wengi waliokuwa karibu na Mwalimu, including Salim, ni wanafiki. Walijua Mwalimu hapendi hiki hapendi kile kwa hiyo nao wakapretendkuwa hawako hivi hawako vile. Lowassa alikuwa fisadi tangu utotoni. Lakini alijua kuficha makucha yake. Hawa mbwa mwitu wa CCM wote walijua kuficha makucha yao. Ndo maana niliondoka CCM baada ya Mwalimu kufariki.
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Nov 9, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  CCM ya Nyerere (CCM-NY) sio ya Mwinyi (CCM-MW), Mkapa (CCM-MK) wala Kikwete (CCM-KI)! Ile ya Nyerere iliongozwa na Azimio la Arusha lililokuwa na Miiko ya Uongozi! Kwenye CCM-NY hakuna aliyethubutu kujilimbikizia mali isivyo halali! Mwenye mali hakuruhusiwa kugombea uongozi wa CCM-NY! CCM-MW ilifuta Azimio la Arusha, madirisha yasiyo na nyavu ya kiuchumi yalifunguliwa! Kwa hiyo upepo "mzuri" wa kiuchumi uliruhusiwa lakini kwa kuwa hakukuwa na nyavu pia mbu, vumbi, wadudu wa bidhaa feki na bei rahisi walimaliza kabisa viwanda vyetu ambavyo havijanyanyuka hadi leo! Mpaka sasa we are consuming what we don't produce and we are producing what we don't consume! CCM-MW ilimzaa CCM-MK ambaye iliendekeza mno wezi ambao walipewa jina "zuri" la wawekezaji! Ukiongea jambo baya juu ya mwekezaji unaonekana wewe sio mzalendo! Wizi huu ulizaa ufisadi! CCM-MK iliwalea mno mafisadi na ukiongea vibaya juu ya mafisadi unaambiwa wewe ni "mvivu wa kufikiri" au "una wivu wa kike!" CCM-KI inaendeshwa kisanii: hakuna mipango yoyote zaidi ya ile iliyokuwapo ya kuingia Ikulu! Baada ya kuingia hawajajua wafanye nini! Usanii unaendelea kila nyanja: kwenye mapambano dhidi ya ufisadi wengine wanatakiwa wapumzike, wakati baadhi wanashtakiwa! Wengine wanapewa muda wa kurudisha hela walizoiba, wengine wanafunguliwa mashtaka bila kupewa huo muda! CCM-KI ni nyepesi mno kuona matatizo lakini ni nzito mno kuchukua hatua, imejaa woga na kuoneana haya! CCM hii inaonekana haina central command, kila mtu ni msemaji! Migawanyiko, vijembe, matusi, kukashfiana ili kutafuta cheap popularity kila kona! Usipokuwa na vijisenti kwenye CCM-KI sahau kabisa kuchukua fomu ya kugombea uongozi, utaaibika! CCM-KI si Chama cha Wakulima na Wafanyakazi: Ni Chama Cha Wafanyabiashara! Ukiambiwa CCM ina wenyewe, they always mean what they say, and say what they mean!
   
 11. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #11
  Nov 9, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyerere alionyesha sana wasiwasi kwa Lowasa na akawaaminisha Watanzania wakatambua hilo. Lakini tokea Lowasa aanze kujijenga kuingia kwenye Uwaziri mpaka alikofikia angalia sasa yanayotokea mpaka inafikia ni sisi wenyewe wa kujilaumu.
   
 12. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #12
  Nov 9, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Jamani kila karne na zama zake. sasa hatuwezi kulinganisha chumvi na sukari. Enzi za JKN kulikuwa chama kimoja na sasa vyama vingi. Hivyo ni bora tubadilike kulingana na mazingira.
   
 13. kilema

  kilema Member

  #13
  Nov 9, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wote mafisadi wa Mawazo. wizi mtupu. hamna hoja. labdamnieleze namna ya kwenda mbele na nione daliliza kwenda mbele. Maneno tupu na mnajifanya mnajua sana. kwendeni zenu.Kazi kupanga mipango ya kwendA NYUMA.
   
Loading...