Nyerere fit to be a saint - Museveni


Why do you think that I didn't take my time: kuelewa wengine wanachoongea ?
 
mazee ustaarabu hauuzwi dukani. Unaharibu mjadala kwa kutuletea maelezo mareeeefu yasiyohusiana na mada na bado unaongezea komentsi zako zenye matege.

Jaribu kutumia akili na busara kidogo.

ha ha ha! You nailed him!!! Ha ha ha!
 
Kati ya Ukristo/ Uislamu upande mmoja na kutoamini ukristo/uislamu kipi kimeazimwa kwa "mijitu mieupe"? You are just exposing your racist disposition.

Naona mada inaanza kupiga kona kuelekea "kusikojulikana".
Hivi kati ya hizo dini mbili ni ipi ndo waafrika wameazima kutoka kwa "mijitu mieupe".
 
I'm not an authority to create versions mazee.

You don't have to create a version to have a version, you don't have to be a windows programming guru to have a version of windows XP. I need to know the version you are using in order to understand better your thinking.

Sasa kama unaadvocate sheria ambazo huwezi kuzi articulate unashindwa hata ku communicate, utaweza kuniconvince ni ishi kwa "sheria ya dhahabu"?

Acha kuchekesha.
 
Naona mada inaanza kupiga kona kuelekea "kusikojulikana".
Hivi kati ya hizo dini mbili ni ipi ndo waafrika wameazima kutoka kwa "mijitu mieupe".

Umeshindwa kuona contrast si ukristo/uislam bali ni Ukristo/Uislam on one hand na kutoamini Ukristo/Uislam on the other.

Kuhusu ipi waafrika wameazima kutoka kwa "mijitu mieupe" inategemea definition yako ya "mijitu mieupe" ni nini.
 
Acha kuchekesha.

Wewe ndio unayechekesha..How can you ask me to provide my own version of Pythagoras theorem ... Hivi unaelewa maana ya version weye?

Nadhani una matatizo ya msingi kuliko nilivyofikiria hapo awali.
 
Penye ukweli uongo hujitenga.Hawakubaliki na Kanisa TZ ila Uganda ruksa kuimba? Ninini tena hiki? Au ni personal vendetta za baadhi ya wahusika kwenye sakata la maombi?
 
Kati ya Ukristo/ Uislamu upande mmoja na kutoamini ukristo/uislamu kipi kimeazimwa kwa "mijitu mieupe"? You are just exposing your racist disposition.

Ahaa!
Sijataja hizo dini! wewe wasema. Mie kwangu kama wanadamu (hapa hasa watanzania) undugu, kuishi pamoja,kusaidiana na mambo kama hayo ndilo la msingi,...mtu yeyote anaeleta imani yake inayotaka kututenganisha undugu wetu,kuheshimiana kwetu nk kwangu mimi anastahili kuitwa jitu (tena jitu ovu)!
 

Collectivism at its best! What do you think we are, some borgs?
 
Collectivism at its best! What do you think we are, some borgs?

Enheehee!! hili lilugha la wakoloni wakati mwingine linanisumbua mkuu.
Kwanini usitumie tu lugha yetu ili watu wa kada zote waliomo humu waelewe umesema nini na mie najibu nini!? tusiwabague, tafadhari Bw Bluray!
 
Enheehee!! hili lilugha la wakoloni wakati mwingine linanisumbua mkuu.
Kwanini usitumie tu lugha yetu ili watu wa kada zote waliomo humu waelewe umesema nini na mie najibu nini!? tusiwabague, tafadhari Bw Bluray!

Mazee kama una muda wa ziada, nenda kakamate laga na nyamachoma. Hapa naona hoja zimeisha vimebaki vioja.
 

Mkuu Mwanafalsafa,
Kuna giza totoro la ufahamu wa kiroho katika kanisa katoliki. Biblia hawaifuati wao wameamua kufanya kama waonavyo kuwa ni vyema machoni pao. Ndo maana YESU anasema;

Marko 7: 6-8
6Akawaambia (YESU), watu hawa huniheshimu kwa midomo, ila mioyo yao iko mbali nami 7Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu, 8 Ninyi mwaiacha amri ya MUNGU, na kuyashika mapokeo ya wanadamu.

Kuhusu kuombewa na waliokufa Bibilia inasemaje?

Mhubiri 9:5-6
5Kwa sababu waliohai wanajua ya kwamba watakufa, lakini wafu hawajui neno lolote, wala hawana ijara tena, maana kumbukumbu lao limesahauliwa. 6Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao imepotea yote pamoja, wala hawana sehemu tena katika jambo lolote linalofanyika chini ya jua

Nani mwombezi wetu?

Waebrania 7:25
25Naye (YESU) kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai siku zote ili awaombee

Je zaidi ya YESU kutuombea tunahitaji intermediate person called saint? The answer is no.

Waebrania 10:19-22
19Basi ndugu kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, 20 njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani mwili wake, 21na kuwa na kuhani mkuu juu ya nyumba ya MUNGU 22na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya; tumeoshwa miili kwa maji safi.

MUNGU awasaidie macho yao ya rohoni yatiwe nuru wapate kuona.
 
..mwalimu angechukia sana huu upumbavu,wana muda wa kupoteza sana hawa!
 

Una jua mimi sielewi kabisa mtu ana pewaje utakatifu na binadamu wenzake. Mungu si ndiyo anaye jua nani mwenye haki na nani asiye na haki kutokana na maandishi? Sasa iweje binadamu wenzie waji pangie kumpa utakatifu. Una mpa utakatifu kumbe kwa Mungu siyo mtakatifu. Huku ndiyo kufanyana miungu mtu. Mi nakubaliana na wewe, kama haya ndiyo mawazo yao basi kunatatizo. utamuombaje binadamu mwenzio akuombee rehema au msamaha kwa mwenyezi Mungu? Hata hii ya kumuabudu bikira Maria sielewi kabisa. Sema haya bwana ngoja tuwaachie wenyewe, ukisema sana utaambiwa una ingilia imani za wengine.
 

Mazee imani ya kanisa na mafundisho yake, watu huwa wanakaa chini wanafundwa na kufuhitimu. Iwe seminari au parokiani watu husoma katekisimu na mafunzo mengine.

Wewe na mwenzako hapo juu inaonesha si waumini na hamna mafunzo ya dini ya kikatoliki. Ungefanya vyema hoja zako ukaziweka in terms of maswali, badala ya in terms of conclusion kama ulivyofanya. Matokeo yake ni kuwakosea wengine adabu, kudhihiridha rigidity ya akili yako, na kuingilia imani za wengine na kujitia ujuaji wa mambo usiyoyaelewa.

Mambo kama haya ndiyo yanayoleta mafarakano ya kidini mazee.
 

Ndiyo maana nikasema imani yao tuwaachie wenyewe kwa vile sina mamlaka ya kuihoji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…