Mwl Nyerere: Hata mimi walinambia using'atuke nchi bado inakutegemea, nikaja jua kumbe nchi ni familia zao, hawana uhakika na ajira zao nikiondoka

eliesikia

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
787
755
Nimekumbuka ujumbe wa Mwl Nyerere kabla ya kung'atuka aliporusha dongo kwa wapambe wake waliomshauri abaki madarakani kwa kuwa ana afya, uwezo na wananchi wanamuhitaji sana kama kiongozi wao mzalendo.

Mwalimu aliwaambia wapambe wake hapana na wasiwe na wasiwasi kwamba akiondoka labda ajae hatawapa madaraka bali wajithamini kama nao wanapaswa kung'atuka kama yeye.

Alirudia tena stori yake mwaka 1992 au 1991 hivi akiongelea ishu ya vyama vingi na uoga wa Chama kushindwa baadae.

Nawasilisha wadau. Kama kuna mtu ana video au gazeti la uhuru wakati huo naomba aweke hapa ili vijana wetu wa sasa nao wafaidike.
 
Hilo ni fundisho tosha kwa huyu wa leo ambaye anajinadi kuwa ni yeye pekee mwenye uwezo wa kuliletea maendeleo Taifa hili na anabainisha kuwa watanzania wasahau suala la maendeleo iwapo yeye ataondoka madarakani!

Huyu jamaa anatengeneza mazingira ya "kuipindua" Katiba yetu ili awe Life Prezidaa wetu!

Kama ulivyosema wapambe wa Mwalimu walipomwambia Nyerere kuwa ni wewe pekee mwenye uwezo wa kuongoza, aliwakatalia.Kata kata......

Swali la msingi linakuja, endapo hawa wafuasi wa "do or die" wa Jiwe watakuja na pendekezo la kumwomba aendelee kuongoza, je atawakatalia??

Nionavyo Mimi ni kuwa atawakubalia na juhudi zishaanza za kina Mkamia+Makonda, kutaka "kuichezea" Katiba yetu, kwa kutaka kuondoa ukomo wa kutawala!
 
Mara pumzi imekata amechoka

Mara anataka kuendelea, hamueleweki.

Magufuli atamaliza miaka yake 10 kikatiba, atakuja mwingine, nayeye mtaanza kusimanga kama kawaida yenu, hamna kazi nyingine mnayoiweza.
 
Mara pumzi imekata amechoka

Mara anataka kuendelea,hamueleweki.

Magufuli atamaliza miaka yake 10 kikatiba,atakuja mwingine,nayeye mtaanza kusimanga kama kawaida yenu,hamna kazi nyingine mnayoiweza.
Katiba ya Nchi haisemi rais atachaguliwa kwa miaka kumi.Katiba ya nchi inasema rais atakaa madarakani miaka mitano,ila imempa Uhuru wa kugombea tena miaka mitano mingine.Na hiyo miaka mitano mingine akishindwa akae pembeni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unafikiri aling'atuka kwa kupenda? Mambo yalishakuwa magumu sana.
Badala ya kujadili hoja aliyoisema Nyerere wewe unamjadili Nyerere kama Nyerere kwa hisia zako tu kama vile upo faragha kwa mpenzi wako! Naona ujinga hauondolewi kwa kuhudhuria darasani

Hiyo chuki yako dhidi ya Nyerere utakufa nayo jinga wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom