Mashirika mengi ya umma yalikufa enzi za Nyerere...! Na wale waliyo yauwa wakaamishiwa kwenye mashirika mengine.
Tukaanza panga foleni kwenye maduka ya kaya.
Kweli alikuwa shupavu na alijuwa kuwalinda watu wake.
Are you serious mkuu!?Ni kama yapi hayo mashirika yaliyokufa kipindi cha mwalimu Mkuu?
I should ask you if you're serious.Are you serious mkuu!?
X-PASTER......!
mashirika mengi yalikufa kipindi au awamu ipi?
UFI,KIUTA,ELIMU SUPPLY,ZZK,URAFIKI,KAMATA,UDA,KAURU,PRINTPAK,KIBUKU,KAUMU,KAUDO,MWATEX,TACOSHILI,TIPER,ATC,TRC,MAHOTELI(kilimanjaro hotel,new africa hotel,mwanza hotel,moshi hotel,seventy seven hotel,mount meru hotel,...) CO-CABS,N.M.C, NDC,NBC,THB,TIB,TIMU ZA MASHIRIKA(ushirika moshi,nbc mbeya,reli morogoro,rtc kigoma,sigara,bandari mtwara,kurugenzi dodoma,ujenzi rukwa,plisner,ndovu ya arusha/now AFC, ),RANCHES,MUTEX,...........PUGU ROAD ILIKUWA INDUSTRIAL AREA KARIBIA VYOTE VILIKUWA VYA SERIKALI
X-PASTER UNASEMAJE?
ccm oyeee, zidumu fikra za mwalimu.
I should ask you if you're serious.
Sasa wewe unataka kumfananisha Nyerere na nani, Mkapa? Mashirika yote aliyoanzisha yalikufa wakati wa Mwinyi. Nchi ikakosa misimamo na mwelekeo wewe uliza nchi zote zilizoendelea zina misimamo, zinajua kusema 'no' pale ambapo maslahi yao yasipotekelezwa. Wakati wa Nyerere nchi ilikuwa inamalengo na wakubwa wa magharibi walikuwa wanajua hilo ndio maana walihakikisha baadhi ya mambo yake hayakufanikiwa.
We angalia tuu idadi ya wasiojua kusoma na kuandika ilivyoongezeka baada ya yeye kung'atuka. Sasa ni nani unataka kumfananisha na Nyerere katika hao viongozi waliomtangulia? Nyerere alikua binadamu kama mimi na wewe na alikose mengi tuu lakini alikuwa mwadilifu na alitekeleza alichoahidi. Au wewe unafurahi kuona magorofa kariakoo na vijigari vingi ukidhani ndiyo maendeleo, du kweli tuna safari ndefu.
Alikuwa anamwogopa Mungu hawa jamaa tulonao ni kama atheists wala hawaogopi chochote!
Sera zake mbovu alizo siasisi ndio zimeimaliza nchi hii. Aliposhindwa baada ya kutawala zaidi ya miaka ishirini na kushuhudia kila kitu kikishindwa na maji yapo shingoni, yanakaribia kuingia mdomoni, kiujanja ujanja na kiutu uzima akaamua kutoroka uongozi, ndio akamtupia Mwinyi kwa kusingizia kuwa anangatuka mapema...!
Soma Hapa: Natamani Kuishi Tanzania na si Tanganyika