Tumia nyenzo za kidigitali kubainisha eneo halisi ilipopigwa picha hii amba mdau aliuliza "hii ni sehemu gani bongo?" Je, umetumia nyenzo gani kujua eneo halisi?
- Tunachokijua
- Je, wajua? Uhakiki na uthibitishaji wa picha ni muhimu ili kudhibiti upotoshaji unaoweza kufanyika kupitia maudhui hayo. Hivyo ni muhimu kujifunza namna ya kutumia nyenzo za kidijitali zinazotuwezesha kubaini uhalisia wa picha.
Uthibitishaji Picha kwa kutumia Google Reverse Image Search ni njia muhimu ya kubaini asili au maelezo zaidi kuhusu picha fulani.
JamiiCheck imekuandalia utaratibu wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kutumia Nyenzo hii kufanya uhakiki wa picha. Rejea kiungo hiki kufuata hatua zote.
Mfano tutumie picha hii ambayo mdau ametaka kufahamu ilipigwa wapi. Picha hiyo inaonesha majengo yaliyopo pembezoni mwa fukwe huku upande wa nyuma kukiwa na safu ya mlima mrefu. Je, ilipigwa wapi na lini?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck
Ufuatiliaji wa JamiiCheck kwa kutumia Google reverse image search umebaini picha hiyo ilichapishwa Machi 05, 2013 na ukurasa wa Matema Beach Festival katika mtandao wa Facebook huku baadhi ya maoni katika chapisho hilo yanabainisha kuwa eneo hilo ni Kyela Mbeya, Tanzania.
Aidha tovuti ya Tripadvisor ilichapisha picha inayoonesha mandhari ya eneo hilo ambapo inaeleza kuwa ni kijiji cha Matema wilayani Kyela.
JamiiCheck ilienda mbali zaidi na kutaka kufahamu uhalisia wa eneo hilo kama ndipo ilipopigwa picha hiyo ambapo kupitia Google map inabainisha muonekano wa video unaofanana na picha husika, ambapo inabainishwa kuwa ni Matema pembezoni mwa fukwe za ziwa Nyasa mkoani Mbeya.
Na huu ni muonekano wa moja ya jengo kati ya majengo mawili yanaoonekana katika picha hiyo.