Kwa kutumia nyenzo za kidigitali zinazokuwezesha kuthibitisha uhalisia wa video, bainisha eneo halisi video hii iliporekodiwa huku ukieleza Nyenzo uliyotumia.
- Tunachokijua
- Wadau mbalimbali wa JamiiCheck kupitia jukwaa lake la JamiiCheck.com pamoja na mitando ya kijamii wameshiriki kuthibitisha ni wapi video hii ilipochukuliwa. Wengi wamebainisha kuwa eneo hilo ni Mafinga Tanzania, Mtaa wa Changarawe
Uhalisia wa video hiyo ni upi?
Kama walivyoeleza wadau wa JamiiCheck, Ufuatiliaji kwa kutumia Google reverse image search umebainisha kuwa uhalisia ni kuwa video hiyo ni Mafinga nchini Tanzania hii ni mara baada ya mvua ya barafu kunyesha eneo hilo kipindi cha mwaka mmoja uliopita (Oktoba 1, 2024)
Vyanzo mbalimbali na watumiaji tofauti wa mitandao ya kijamii waliripoti uwepo wa hali hiyo (mvua ya barafu) ambapo huwa si hali ya kawaida nchini Tanzania na hivyo kusisimua hisia za watu wengi wa eneo hilo. Tizama hapa na hapa kuona vyanzo vilivyoripoti kuhusu tukio hilo.