Nyaronyo Kicheere 'ahamia CCM'


Mkuu Pasco Lowasa akiwa rais Rais akakukumbuka kwenye ufalme wake watoto wetu weupe watakwisha.
 
Last edited by a moderator:
Kwa hii thread, walofeli "literature" tutawajua tu kwa kuangalia comments zao!
Wako kibao humu. Lakini sio kufeli nadhani ni kutojua. Kwa kuwasaidia ni kuwa makala hii imeandikwa kwa mtindo wa kejeli. Kejeli maana yake huwa ni kinyume na inavyoelezwa. Mfano mtu anafungwa goli tano halafu anaambiwa "wewe ni kipa mzuri sana" Watu wajifunze kutafakari kabla ya kukurupuka kujibu hoja. Na wengi humu Jf huwa wanaangukia katika mtego huo. Ndio maana wengine badala ya kujadili hoja utakuta wanamshambulia mtoa hoja binafsi au mtu anajibu nje kabisa ya kinachojadiliwa. Kwa ufupi ni kwamba anamkandia Kikwete kwa udhaifu wake wa kutochukua hatua kwa wahalifu na kuwasifu viongozi wa CHADEMA kwa kuwa serious!
 
Unakumbuka kuna kipindi flani aliandika kuwa anataka kubadili jina aitwe riziwani na alipamba sana maandishi yake na kutoa sababu kem kem za yeye kubadili jina. Kweli huyu mwandishi ni mahiri , wanaosoma kichwa cha habari na kuchangia lazima waingizwe chaka lol.
 

sijakusoma....................
 
Tanzania inahitaji akili kama hizi siyo za kufuata mkondo kama mto.
 
Naam, ngoma inogile, tutampokea tundu lissu na pro.safari na baregu sio mda mrefu

Wewe kweli T2015 CCM maana unachangia bila ya kutambua maudhui ya MADA. Ungemfahamu Nyaronyo Kichere ni nani usingeandika ulichoandika
 
Mbona watu wanamtete sana eti lugha ya kimafumbo hamna kitu kama hiyo hapa bongo.Siasa haina fasihi wewe ipo siku mtasikia mbona Zitto aliposema Atakuwa wa mwisho kuondoka CDM mkasema mnafiki.Mimi simwamini hata siku moja mtu anayeongea kwa jina la Siasa hapa kuna kitu hizi statement hazitoki bure bure.2015 sio mbali just around the corner tutajua watoa statement zakujifanya kama hawataki lakini wanataka.
 
Naam, ngoma inogile, tutampokea tundu lissu na pro.safari na baregu sio mda mrefu


Hahahahah! Ndoto za alinacha, soma article uielewe, ukiishia kwenye heading utaonekana haunazo!
 
hizo ndizo sifa za kuwa kiongozi wa chama cha ccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…