Nyanza Road works wana bahati gani?

MARKYAO

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
672
1,000
Hii kampuni ya ujenzi wa barabara yenye makao yake pale Bwiru road Mwanza itakuwa na bahati sana.

Kila wakati inalalamikiwa sana kwa kuchelewesha miradi ya barabara lakini bado inapewa tenda.

Makonda kaisema sana kuhusu barabara ya Kitunda to Kivule mpaka katishia kutoipa tena Kazi mkoani Dar

Lakini pia kampuni hii ilipewa kazi ya kutengeneza Barabara ya Nyakanazi Kakonko mpaka Kibondo miaka mitano iliyopita. Lakini mpaka leo hakuna hata km30 zilizojengwa. Wakaazi wa Kigoma na Kagera hasa wilaya za Bihalamuro, Kakonko na Kibondo wanapata taabu sana. Barabara hiyo ni diversions to mpaka Kalenge.

Barabara za Musoma mjini nazo pia hoi na ni kampuni hiyo hiyo walipewa tenda. Au kuna kitu hatujui kuhusu kampuni hiyo. Inaweza kuwa ni kampuni ya serikali lakini hatujui.

Ndugu , hii ni moja ya makampuni yangalitakiwa kufungiwa kufanya kazi za kikandarasi hapa bongo na kupewa kesinya uhujumu uchumi maana hawana uwezo kuanzia human resource, capital, working equipment/ facilities, hawana weledi wa kazi na hata financial capability ya kuhandle project za barabara..

Kwa Nyakanazi- Kakonko wamekaa kuanzaia awamu ya 4 JPM akiwa waziri asa ni raid na hawajajenga hata nusu ya barabara waliyokuwa contracted na sehemu waliyojenga iko chini ya kiwango kulik kawaida.. Waliopita barabara hii watanielewa sana maana japo haijapitwa imeshabanduka na lami very light kwa maeneo walikomwaga..
Width ya barabara pia ni aibu tupu na abiria wanajua mwenye dili lote na hata jamaa na wanasema.. Divergence walizoweka zinaharibu sana magari ya watu na kufanya usafiri kuwa wa karaaa mno.. Kwa upande huu wa Nyakanazi to Kakonko nawalaani sana hawa jamaa..

Wana Kigoma wanalia sana na hii kitu maana ni major road to Bukoba, Kwanza, Kahama, Rwanda, Burundi, Congo na comnectio ya nchi nzima na hata wanapopita mawaziri na wabunge wananyamaza tu maana wanakuja mwenye malkaka na hii kampuni.. Ni hayo tu kuhusu Nyakanazi to Kakonko road..
 
Oct 4, 2019
16
45
Dodoma,Kuna barabara ya Kutoka geti la UDOM hadi njia ya panda ya barabara ya kwenda Moro.Ni kipande cha km 15 tu.Huu ni mwaka wa saba hawajamaliza.Mimi siamini kama ni ya Mjomba Magu,isingekuwa ya kichovu kiasi hiki
amin ni yake statement yko ingkua hivi ingkua sio ya magufuli angkua kashaitumbua
 

PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
17,240
2,000
Wanasiasa wanajinasibu kutukana wakandarasi wakati hawalipi?

Miradi mingi ambao serikali ndiyo mtoa pesa hawalipi kwa wakati na wanataka wapewe na 10%.

Ukiona mwanasiasa anamzodoa mkandarasi ujue hajapata 10% yake tu akipewa anasifia.

Na ndiyo kula ya viongozi wetu tunaongozwa majizi na mazandiki tu.

Serikali ya ccm huwa haiwalipi wakandarasi hasa wa ndani
Miradi yote inayotekelezwa kwa fedha za ndani maarufu kama development budget projects huwa haikamiliki kwa wakati na sio huko tuu ni nchi nzima,lawama kwa John maana serikali huwa haina pesa ila ukiona mradi uko Fasta jua ni mkopo au mfadhili
 

logframe

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
4,016
2,000
Hyo ni kampuni ya Maghufuli, alinunua vifaa toka Kwa waitaliano wa Astard waliojenga kipande cha Kutoka Nyanguge mpak mwanza mjin toward airport mwanzoni mwa miaka ya 2000..
Lakn mpak leo hakuna repair kwenye vifaa vyao , vimechoka vibaya....ukiachilia mbali pesa ya miradi kuchelewa lakn pia wapo narrow Sana kurun project nying nying Kwa mpigo....wingi wa miradi unazidi uwezo wao wa kuhudumia
Ila muitaliano ile Barabara ailiijenga kwa viwango vikubwa... Ni lami nzuri kwamkoa wa Mwanza sioni kipande cha kuilinganisha japo ina miaka kama 14 sasa.
Nyanza Road hata hiki kipande cha Usagara-Kisesa kitafumuka na kuiacha Barabara ya Mwanza _ Nyanguge.. Nimeona kwa macho yangu sio engineer lakini ni vumbi tupu limejazwa hasa hapo karibu na kituo cha polisi Kisesa.
 

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
697
1,000
Ni kama barabara ya Tinde to Isaka. Iko vizuri sana, huwezi linganisha na ile ya Tinde to Shinyanga
Ila muitaliano ile Barabara ailiijenga kwa viwango vikubwa... Ni lami nzuri kwamkoa wa Mwanza sioni kipande cha kuilinganisha japo ina miaka kama 14 sasa.
Nyanza Road hata hiki kipande cha Usagara-Kisesa kitafumuka na kuiacha Barabara ya Mwanza _ Nyanguge.. Nimeona kwa macho yangu sio engineer lakini ni vumbi tupu limejazwa hasa hapo karibu na kituo cha polisi Kisesa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom