Najua wewe ni kiongozi wetu shupavu, mpenda mageuzi, mtu wa watu, katika saula la mgombe wa ubunge jimboni mwako, angalia nguvu ya chama chetu ukilinganisha na vyama vingine vya UKAWA hasa CUF, NLD na CHADEMA. Zingatia matokeo ya chaguzi za serilaki za mitaa. ukiona chama chetu kinatosha ok pigania hiyo nafasi. Lakini kama kuna chama kimetupiku na mkakati ni kuiondoa CCM, basi tuwaachie waliofanya vizuri waendelee na kinyang'anyiro hicho sisi tupige kampeni tu. Jambo la muhimu ni wewe kupata maslahi kutoka ruzuku zitakazopatikana kutokana na ushindi wa ujumla wa chama kama wenzetu CDM wanavyofanya kwa Dr. Slaa ilimradi wewe uendelee kujenga chama. Bado tunahitaji viongozi wengi tu baada ya kushika dola. wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi n.k Huwezi kukosa wadhifa.