Nyama ngumu kama manati haipendezi, jitahidi mpishi ukipika nyama yoyote ile iwe laini

Waislamu kwenye kupika tuko vyedi mkuu
Upishi ni swala binafsi. Usiseme Waislamu.

Kwa sababu hakuna somo la mapishi kwenye mafundisho ya dini.

Nenda Kigoma Ujiji, waislamu kede. Lakini sasa, achia hapo.

Nadhani mabinti wa pwani haswa Dar na Tanga ndiyo wataalam wa mapishi. Na kutokana na uhalisia, maeneo hayo watu wengi ni Waislamu. Ila hawajui kupika kwa sababu ya Uislamu, bali kwa sababu ya tamaduni za eneo husika.

Eid Mubarak!.
 
Upishi ni swala binafsi. Usiseme Waislamu.

Kwa sababu hakuna somo la mapishi kwenye mafundisho ya dini.

Nenda Kigoma Ujiji, waislamu kede. Lakini sasa, achia hapo.

Nadhani mabinti wa pwani haswa Dar na Tanga ndiyo wataalam wa mapishi. Na kutokana na uhalisia, maeneo hayo watu wengi ni Waislamu. Ila hawajui kupika kwa sababu ya Uislamu, bali kwa sababu ya tamaduni za eneo husika.

Eid Mubarak!.
Waislamu kupika labda uji wa muhogo
Kupika ni suala la mtu binafsiiiiiiiii
 
Nyama inategemeana mnyama pia.

Nyama ya ngoro (ng'ombe aliyekonda na mwenye njaa) hata uweke recipes zako, hailainiki ng'oo.

Nyama ya ng'ombe aliyenona automatically huwa na ulaini fulani.

Lakini pia, usipike nyama kwa moto mkali sana. Ninakuhakikishia zitakuwa ngumu tu. Pika kwa moto wa wastani.

Kuna aina ya ukataji pia ambao walau vile vinyuzi nyuzi (fibers) zitaiva kwa uharaka.
 
Wapishi wa nyama katika migahawa, Bar, hotel, sherehe na hata majumbani hakikisheni nyama zinaiva vizuri na kuwa laini kabisa. Iwe nyama ya kuchemsha, kuchoma au kukaanga nyama inatakiwa iwe laini kabisa uweze kuichambua au kuitoa kwenye mfupa au kuitenganisha kwa kijiko, uma au mkono mmoja tu.

Iwe nyama ya ng'ombe, mbuzi, kuku wa kienyeji au kitimoto nyama inatakiwa kuivishwa na kuwa laini kabisa. Iwe utumbo, mbavu, paja, mguu au sehemu yoyote ile inatakiwa iive iwe laini.

Haipendezi na Inakera sana kula nyama huku unavuta kwa mikoni miwili kama manati au unatafuna kama bigijii, Inakera kula nyama huku zinabaki kung'ang'ania katikati ya meno na kukuhitaji kumaliza toothpick kikopo kizima kusafisha mabaki ya nyama kwenye meno.
huku maporini kwetu nyama kuiva au kua laini sio issue, ilimradi imekatatwa vipande vidogo vidogo na ni ya moto na haibani mdomo 🐒

ikiwa ngumu unameza tu mapishi ya kuilainisha itafanyika huko ndani tumboni na kazi inaendelea mpaka utakapotosheka🐒
 
Hii comment imepewa like na jamaa yangu mmoja mpenda nyama, naunga mkono hoja hii.

😁
Carleen
Wengi hawajui kupika supu, nyama inatakiwa ichemshwe kwa kuongeza maji kidogo kidogo sana mpaka iive kabisa ndio uongeze maji hata kama ni pipa zima kama unavyotaka. Tofauti na hapo ukiijaza maji tokea mwanzo itakubidi utumie muda mrefu sana na moto mwingi sana kuichemsha mpaka iive kabisa.
 
Back
Top Bottom