Nyalandu: Ripoti ya Lembeli uongo mtupu

Nyalandu: Ripoti ya Lembeli uongo mtupu

Sijawahi kumkubali huyu mtu na.kama ni madaraka anapata ya uteuzi! !!!!!!
Hii nchi ina taabu sana na viongozi hawa!!!!!

Anaongea leo as if kaletwa na mafuriko hivi kazi tarajiwa haifanyiki basi hata kuheshimu ufahamu wetu pia ni ngumu????!!!!
 
Nchi yetu hatuna uwajibikaji! Nyalandu anataka aonekane mchapakazi wakati huu akiwa naibu waziri, kama alivyokuwa akifanya kuhusu lile sakata la TBS. Watawala wetu ndiyo wanaojihusisha na matatizo ya uwindaji haramu, usafirishwaji wa madawa ya kulevya, kwani wasingekuwa wao hali isingekuwa hivi.

Uko sahihi mkuu ila nadhani naibu waziri huyu alitakiwa aseme ina mapungufu badala ya kusema ni uongo mtupu.
Inawezekana Lembeli akawalinda wenzake kama alivyofanya Hosea wa akukuru kwenye issue ya richmond
lakini hapa mh.lazaro hakutakiwa kusema kuwa ni uongo bali alitakiwa ajazie pale penye mapungufu kama kweli yeye ni mkweli.
 
The world is turning around Yesterday becomes tomorrow when lies are said to be the truth and truth is said to be lie.
"No truth in this world"
 
Wajanja wajanja wa mjini na wapiga deal ndo wenye kuongoza maamuzi ya serikali. Who is Nyalandu,? Katokea wapi mpaka kufikia hapo alipo? Ni nani aliye nyuma yake? Na, je Ni juhudi zipi anafanya kujipatia nafasi anazozitafuta? Mimi sijui, ila nahisi naye Ni JANGA la Taifa.

Nyepesi nyepesi... RA na Mkulu ndio walomfikisha hapo alipo!

Who is Nyalandu....Ni tapeli tapeli fulani tokea Singida vijijini na ni jirani sana na IGP Mangu

Jamaa ni mzuri sana kwenye fani ya fitina, uchonganishi na majungu na ndimo alimoukwaa unaibu waziri na kesha wang'oa mawaziri wawili sasa

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/284474-waziri-wa-jk-na-naibu-wake-wahujumiana.html
 
Ukweli wote utafahamika hakuna wa kujificha kwa hili punde tu mbichi na mbivu zitafahamika tu.
 
Nyalandu: Ripoti ya Lembeli uongo mtupu

nyalandu1-300x169.jpg

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ameilalamikia Kamati ya Bunge ya Ardhi, Mazingira na Maliasili iliyoongozwa na James Lembeli kuwa taarifa iliyowasilisha bungeni na kuwang’oa mawaziri wanne ilikuwa ya uongo.

Nyalandu alitoa kauli hiyo juzi alipozungumza na viongozi wa taaluma mbalimbali pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dodoma na Manyara juu ya mgogoro wa mipaka kati ya hifadhi ya taifa ya Tarangire, Pori la Akiba Nkungunero na vijiji vya jirani uliofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

Alieleza kutokana na taarifa hiyo Tanzania kwa sasa imeonekana kushuka kwa kiwango kikubwa katika utawala bora ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Alisema kuna taarifa ambazo zilionyesha kuwa wapo watu ambao walibakwa jambo ambalo halikuwa la kweli.
Hata hivyo, alisema kwa sasa Rais Jakaya Kikwete amekubali kuunda tume ya kimahakama ambayo itafanya uchunguzi juu ya kuwepo kwa matukio hayo na itakapabainisha kuwa kuna watu walipotosha ni wazi watachukuliwa hatua kali za kisheria bila kujali cheo cha mtu ambaye alihusika na uongo au ukiukwaji wa sheria.

Katika hatua nyingine, Nyalandu ametangaza kumsimamisha kazi ofisa wanyamapori mwandamizi katika pori la akiba la Maswa, Lawrence Kileo, kwa kutuhumiwa kupokea rushwa na kuwatoza faini wafugaji bila kuzingatia taratibu.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache tangu atangaze kusimamishwa kazi kwa watumishi 22 wa wizara hiyo.
Ofisa huyo anatuhumiwa kuwatoza faini wafugaji wanaoingiza mifugo yao katika pori hilo bila kutoa risiti za serikali, na hivyo fedha hizo kujinufaisha mwenyewe kinyume cha kifungu cha sheria namba 116[2]C cha sheria ya kuhifadhi wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009.

Nyalandu ametangaza kuanza kwa uchunguzi kwa Ofisa Wanyamapori wa Wilaya ya Kasulu, Benjamini Mkosamali, kabla ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kuwaruhusu watuhumiwa wa ujangili kuondoka na nyara za serikali walizokamatwa nazo kabla ya kukamatwa tena kwa msaada wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Nyalandu alisisitiza kuwa serikali itaendelea kuchukua hatua zaidi kwa maofisa wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vyovyote vile vya kukiuka maadili ya kazi yao.
Watuhumiwa hao wa ujangili mkoani Kigoma ambao walikamatwa wakiwa wamebeba wanyama aina ya tohe 12, madume watano na majike saba wakiwa pia na insha wanne aina ya Oribi ambao hawakupaswa kuwinda kwa mujibu wa leseni yao ya uwindaji namba B59921 iliyotolewa Kigoma.

Alisema awali watuhumiwa hao walikamtwa na kikosi cha doria cha Kampuni ya Friedkin Conservation Fund na kumuita ofisa huyo kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi ambapo alipofika na kuzungumza na watuhumiwa aliwaruhusu kuondoka na wanyama hao.

Nyalandu alisema Benjamini akiwa na taaluma ya kusimamia wanyamapori huku akifahamu majangili waliokamatwa wamekutwa na nyara za serikali na wamekutwa katika kitalu cha uwindaji sehemu ya Kibenge, baada ya kupata taarifa kwa wahusika, aliamua kwa makusudi kuwaruhusu majangili hao kuondoka.
“Hivyo nimeagiza mamlaka husika kukamilisha uchunguzi na kumchukulia hatua za kinidhamu na za kisheria haraka sana ofisa huyo,” alisema Nyalandu.

Alisema kuwa vita dhidi ya ujangili itaendelea kwa kasi na hata rais ameishaahidi kuwa operesheni ujangili awamu ya pili itarejea hivi karibuni baada ya kurekebisha kasoro zilizojitokeza katika awamu iliyomalizika.
Alifafanua kuwa kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita baada ya kusitishwa kwa operesheni hiyo, tembo 60 waliuawa na majangili hao kitendo ambacho hakitakiwi kuvumiliwa.

Source: Tanzania Daima (Tanzania Daima – Nyalandu: Ripoti ya Lembeli uongo mtupu)

Unajua huyu jamaa ni mjanja sana baada ya kuona bos wake kajiuzulu bas anaanza kuwasimamisha kazi dagaa na kutangaza mbele ya waandishi wa habar ili aonekane anapiga kazi kuliko bos wake aliyepita lengo hasa ni kupata umaarufu ili apewe wizara kamili. Lakin tumeshaijua janja yake!!!
 
Ingekuwa uongo mawziri wangejiuzulu????acha kudanganya watu wewe waziri ndio muongo,acheni kupotosha watu
 
LEMBELI ALIDANGANYA KWA FAIDA YA NANI? jE YEYE NI JANG-HIL LA TEMBO?
 
Shida yake kuingiza mkenge mkulu.alimfitinisha chami wizara ya viwanda kagasheki leo kapaki gari.kijana hatari eti naye anadai kama makamba junior kwamba wamarekani wanataka awe Rais wa 5 wa URT mahooooka!!!!!!!!!
 
Nyarandu na Katibu wa wizara hiyo nahisi siku zote lengo lao limekuwa moja Vs Kagasheki.
Ila the good thing ni kuwa this time hatakuwemo kwenye cabinet badaa ya cabinet kufanyiwa marekebisho.
 
Kweli huyu kijana mfitini mbaya sana na anadaiwa hajambo ktk sayansi ya giza,ameshirikiana na watendaji wa wizara wakamtenga waziri Kagasheki,leo anakurupuka na kuongea mbofu mbofu!! Amezoea toka yupo naibu kwa Ciril Chami ni mtu wa majungu na fitina.
 
CCM hakuna mwenye afadhali.yule unayemdhani hachelewei tia aibu kabisa...Sas huyu anakumbusha watu kuwa alisahaulika.Kweli hii mizigo inayokumbusha abiria kuchukua mzigo wake ni nouma.
 
Nyarandu na Katibu wa wizara hiyo nahisi siku zote lengo lao limekuwa moja Vs Kagasheki.
Ila the good thing ni kuwa this time hatakuwemo kwenye cabinet badaa ya cabinet kufanyiwa marekebisho.
mkuu ulichosema kina ukweli 100%
 
Nyalundu is a minster of just for show.that also singida is present .yale yale kuchagua kiongozi kutokana na eneo analotoka or let say kabila .na sio kutokana na kipaji cha kuongoza .this must go down with ccm .2015
 
Umewahi kujiuliza ni nani alipiga picha wakati yule jamaa ana...za mti? au ni wakati gani kwenye maeneo yote ya matukio picha zilipigwa na nani alihariri?

.........hakuna mtu amepigwa picha anafanya mti, ingawa hao hao watesaji, for funny wanaweza wakapiga picha. Kilichotokea ni Mlalamikaji kutoa ushuhuda wa aliyotendewa. Kingine picha nyingi ni za majeruhi, ambao wako mpaka leo na wapo watu aliopotea hadi leo.
Nyalandu anapiga samasoti na taulo !:A S 112:
 
Nyalandu: Ripoti ya Lembeli uongo mtupu

nyalandu1-300x169.jpg

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ameilalamikia Kamati ya Bunge ya Ardhi, Mazingira na Maliasili iliyoongozwa na James Lembeli kuwa taarifa iliyowasilisha bungeni na kuwang'oa mawaziri wanne ilikuwa ya uongo.

Nyalandu alitoa kauli hiyo juzi alipozungumza na viongozi wa taaluma mbalimbali pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dodoma na Manyara juu ya mgogoro wa mipaka kati ya hifadhi ya taifa ya Tarangire, Pori la Akiba Nkungunero na vijiji vya jirani uliofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

Alieleza kutokana na taarifa hiyo Tanzania kwa sasa imeonekana kushuka kwa kiwango kikubwa katika utawala bora ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Alisema kuna taarifa ambazo zilionyesha kuwa wapo watu ambao walibakwa jambo ambalo halikuwa la kweli.
Hata hivyo, alisema kwa sasa Rais Jakaya Kikwete amekubali kuunda tume ya kimahakama ambayo itafanya uchunguzi juu ya kuwepo kwa matukio hayo na itakapabainisha kuwa kuna watu walipotosha ni wazi watachukuliwa hatua kali za kisheria bila kujali cheo cha mtu ambaye alihusika na uongo au ukiukwaji wa sheria.

Katika hatua nyingine, Nyalandu ametangaza kumsimamisha kazi ofisa wanyamapori mwandamizi katika pori la akiba la Maswa, Lawrence Kileo, kwa kutuhumiwa kupokea rushwa na kuwatoza faini wafugaji bila kuzingatia taratibu.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache tangu atangaze kusimamishwa kazi kwa watumishi 22 wa wizara hiyo.
Ofisa huyo anatuhumiwa kuwatoza faini wafugaji wanaoingiza mifugo yao katika pori hilo bila kutoa risiti za serikali, na hivyo fedha hizo kujinufaisha mwenyewe kinyume cha kifungu cha sheria namba 116[2]C cha sheria ya kuhifadhi wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009.

Nyalandu ametangaza kuanza kwa uchunguzi kwa Ofisa Wanyamapori wa Wilaya ya Kasulu, Benjamini Mkosamali, kabla ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kuwaruhusu watuhumiwa wa ujangili kuondoka na nyara za serikali walizokamatwa nazo kabla ya kukamatwa tena kwa msaada wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Nyalandu alisisitiza kuwa serikali itaendelea kuchukua hatua zaidi kwa maofisa wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vyovyote vile vya kukiuka maadili ya kazi yao.
Watuhumiwa hao wa ujangili mkoani Kigoma ambao walikamatwa wakiwa wamebeba wanyama aina ya tohe 12, madume watano na majike saba wakiwa pia na insha wanne aina ya Oribi ambao hawakupaswa kuwinda kwa mujibu wa leseni yao ya uwindaji namba B59921 iliyotolewa Kigoma.

Alisema awali watuhumiwa hao walikamtwa na kikosi cha doria cha Kampuni ya Friedkin Conservation Fund na kumuita ofisa huyo kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi ambapo alipofika na kuzungumza na watuhumiwa aliwaruhusu kuondoka na wanyama hao.

Nyalandu alisema Benjamini akiwa na taaluma ya kusimamia wanyamapori huku akifahamu majangili waliokamatwa wamekutwa na nyara za serikali na wamekutwa katika kitalu cha uwindaji sehemu ya Kibenge, baada ya kupata taarifa kwa wahusika, aliamua kwa makusudi kuwaruhusu majangili hao kuondoka.
"Hivyo nimeagiza mamlaka husika kukamilisha uchunguzi na kumchukulia hatua za kinidhamu na za kisheria haraka sana ofisa huyo," alisema Nyalandu.

Alisema kuwa vita dhidi ya ujangili itaendelea kwa kasi na hata rais ameishaahidi kuwa operesheni ujangili awamu ya pili itarejea hivi karibuni baada ya kurekebisha kasoro zilizojitokeza katika awamu iliyomalizika.
Alifafanua kuwa kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita baada ya kusitishwa kwa operesheni hiyo, tembo 60 waliuawa na majangili hao kitendo ambacho hakitakiwi kuvumiliwa.

Source: Tanzania Daima (Tanzania Daima – Nyalandu: Ripoti ya Lembeli uongo mtupu)

............daaah huyu Msingida ametudharau sana !:A S 13:
 
Back
Top Bottom