Nyalandu: Ripoti ya Lembeli uongo mtupu

Nyalandu: Ripoti ya Lembeli uongo mtupu

Kabla ya kuendeleaa na hii mada hebu tuambie ni lini Omary Nundu aliwahi kuwa Waziri waa viwanda na biashara???????

Alisahau kidogo, nundu alikuwa waziri wa uchukuzi, na nyalandu hakuwa naibu wake, nyalandu alikuwa viwanda na biashara chini ya mkibosho mmoja anaitwa Cyril chami, sijui yuko wapi siku hizi
 
Ungekuwa wa kike, mbowe angeshakuchumbia, watu wanajadili hili wewe unakuja na mbowe... shame

Bora umwambie wazi ni lijinga sana! mkuu unajua mijitu mingine ikishavuta mibange yaisomi kilichoandikwa yanajimwaga tu na utumbo wao!
 
Watu wengine bwana kwa upotoshaji hawajambo. Mh Omary Nundu hajawahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara. Alikuwa Mh Cyrill Chami
 
Kabla ya kuendeleaa na hii mada hebu tuambie ni lini Omary Nundu aliwahi kuwa Waziri waa viwanda na biashara???????

Nadhani kuna timu ya kumchafua huyu jamaa inaibuka taratibu,pamoja na kuwa hata mimi huwa sioni kwa nini huyu jamaa ni waziri (naibu) lakini uandishi uwe na umakini!!!!!!

Hivi anatokaje waziri naibu akabaki au hii ni kuthibitisha kuwa naibu huwa hafanyi kazi yoyote??!!!!!
 
Tunapaswa kisubiri tume ya kimahakama iliyoundwa, tuache utabiri wa nyota.
 
Watu wengine bwana kwa upotoshaji hawajambo. Mh Omary Nundu hajawahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara. Alikuwa Mh Cyrill Chami

amekosea hajapotosha. Mantiki ya mjadala imeeleweka kuwa nyalandu alimfitinisha waziri wa viwanda na biashara wa wakati huo cyril chami
 
Nadhani kuna timu ya kumchafua huyu jamaa inaibuka taratibu,pamoja na kuwa hata mimi huwa sioni kwa nini huyu jamaa ni waziri (naibu) lakini uandishi uwe na umakini!!!!!!

Hivi anatokaje waziri naibu akabaki au hii ni kuthibitisha kuwa naibu huwa hafanyi kazi yoyote??!!!!!

mbaya zaidi hata katibu mkuu wa wizara yake nae amependekezwa kutimuliwa kama mbwa. Imagine waziri na katibu mkuu wanawajibishwa halafu mtu wa katikati anaachwa. Double standards
 
Nyalandu: Ripoti ya Lembeli uongo mtupu

nyalandu1-300x169.jpg


NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ameilalamikia Kamati ya Bunge ya Ardhi, Mazingira na Maliasili iliyoongozwa na James Lembeli kuwa taarifa iliyowasilisha bungeni na kuwang’oa mawaziri wanne ilikuwa ya uongo.

Nyalandu alitoa kauli hiyo juzi alipozungumza na viongozi wa taaluma mbalimbali pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dodoma na Manyara juu ya mgogoro wa mipaka kati ya hifadhi ya taifa ya Tarangire, Pori la Akiba Nkungunero na vijiji vya jirani uliofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

Alieleza kutokana na taarifa hiyo Tanzania kwa sasa imeonekana kushuka kwa kiwango kikubwa katika utawala bora ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Alisema kuna taarifa ambazo zilionyesha kuwa wapo watu ambao walibakwa jambo ambalo halikuwa la kweli.

Hata hivyo, alisema kwa sasa Rais Jakaya Kikwete amekubali kuunda tume ya kimahakama ambayo itafanya uchunguzi juu ya kuwepo kwa matukio hayo na itakapabainisha kuwa kuna watu walipotosha ni wazi watachukuliwa hatua kali za kisheria bila kujali cheo cha mtu ambaye alihusika na uongo au ukiukwaji wa sheria.

Katika hatua nyingine, Nyalandu ametangaza kumsimamisha kazi ofisa wanyamapori mwandamizi katika pori la akiba la Maswa, Lawrence Kileo, kwa kutuhumiwa kupokea rushwa na kuwatoza faini wafugaji bila kuzingatia taratibu.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache tangu atangaze kusimamishwa kazi kwa watumishi 22 wa wizara hiyo.

Ofisa huyo anatuhumiwa kuwatoza faini wafugaji wanaoingiza mifugo yao katika pori hilo bila kutoa risiti za serikali, na hivyo fedha hizo kujinufaisha mwenyewe kinyume cha kifungu cha sheria namba 116[2]C cha sheria ya kuhifadhi wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009.

Nyalandu ametangaza kuanza kwa uchunguzi kwa Ofisa Wanyamapori wa Wilaya ya Kasulu, Benjamini Mkosamali, kabla ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kuwaruhusu watuhumiwa wa ujangili kuondoka na nyara za serikali walizokamatwa nazo kabla ya kukamatwa tena kwa msaada wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Nyalandu alisisitiza kuwa serikali itaendelea kuchukua hatua zaidi kwa maofisa wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vyovyote vile vya kukiuka maadili ya kazi yao.

Watuhumiwa hao wa ujangili mkoani Kigoma ambao walikamatwa wakiwa wamebeba wanyama aina ya tohe 12, madume watano na majike saba wakiwa pia na insha wanne aina ya Oribi ambao hawakupaswa kuwinda kwa mujibu wa leseni yao ya uwindaji namba B59921 iliyotolewa Kigoma.

Alisema awali watuhumiwa hao walikamtwa na kikosi cha doria cha Kampuni ya Friedkin Conservation Fund na kumuita ofisa huyo kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi ambapo alipofika na kuzungumza na watuhumiwa aliwaruhusu kuondoka na wanyama hao.

Nyalandu alisema Benjamini akiwa na taaluma ya kusimamia wanyamapori huku akifahamu majangili waliokamatwa wamekutwa na nyara za serikali na wamekutwa katika kitalu cha uwindaji sehemu ya Kibenge, baada ya kupata taarifa kwa wahusika, aliamua kwa makusudi kuwaruhusu majangili hao kuondoka.

“Hivyo nimeagiza mamlaka husika kukamilisha uchunguzi na kumchukulia hatua za kinidhamu na za kisheria haraka sana ofisa huyo,” alisema Nyalandu.

Alisema kuwa vita dhidi ya ujangili itaendelea kwa kasi na hata rais ameishaahidi kuwa operesheni ujangili awamu ya pili itarejea hivi karibuni baada ya kurekebisha kasoro zilizojitokeza katika awamu iliyomalizika.

Alifafanua kuwa kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita baada ya kusitishwa kwa operesheni hiyo, tembo 60 waliuawa na majangili hao kitendo ambacho hakitakiwi kuvumiliwa.

Source:
Tanzania Daima (Tanzania Daima – Nyalandu: Ripoti ya Lembeli uongo mtupu)

Pumbafu alikuwa wap kupinga bungeni?????
 
Bora umwambie wazi ni lijinga sana! mkuu unajua mijitu mingine ikishavuta mibange yaisomi kilichoandikwa yanajimwaga tu na utumbo wao!

wewe ndio unakuwa mwehu zaidi kwa kutoa matusi, nadhani ni kwa ajili ya gongo unayokunywa
 
Kusema ni uongo ni general generalization,alipaswa kusema uongo ni upi kwani haiwezekani ripoti yoye ikawa uongo,kwani sio kweli kwamba kuna watu walikuwa tortured na kuuwawa bila sababu?
 
Viongozi wa magazeti na social media, badala ya kuingia field na kupiga kazi wamekalia kujibiza wao kwa wao tu
 
nyalandu1-300x169.jpg

Mwanaumme mwenye busara hajichubui kwahiyo anachosema lazima ni utumbo mtupu. Anajipigia ndogondogo awe waziri wa hiyo wizara.............................hatapewa na atahamishwa maana ana kiherehere. Alishirikiana na Lembeli kumpiga vita bosi wake sasa anajitenga nao..................kama huu siyo unafiki ni nini basi?
 
mbaya zaidi hata katibu mkuu wa wizara yake nae amependekezwa kutimuliwa kama mbwa. Imagine waziri na katibu mkuu wanawajibishwa halafu mtu wa katikati anaachwa. Double standards

Hapo ndio huwa nakumbuka maneno ya chama kina wenyewe!!!
 
Nyalandu anajaribu kujijenga mbele ya macho ya rais ili kubali kupata kibali kamili cha uwaziri kwa kuhusisha kushuka kwa alama za utawala bora kimataifa kunakotokana na ripoti hiyo na hivyo;
1. Kumfitinisha rais na mwenyekiti wa tume hiyo
2. Kupotosha umma kama walivyojaribu kudadavua wasemaji wengine hapo juu.
Kwa ujumla uchochoro huu kwa watu makini hautamnufaisha kama ikibainika madai ya tume yana ukweli ndani yake adhawaizi tume ya kimahakama ikiamua kufanya report moderation kukidhi matakwa ya watawala basi atawini na tume itapoteza hadhi kwa kuonekana inaleta fitina . Hata hivyo kuna mambo ambayo yako wazi kiasi kwamba tume ya kimahakama itakuwa na kazi ngumu kupotosha umma mfano yule mwanamke wa galapo itabidi wajipange namna ya kuupotosha umma kukidhi matakwa ya watawala.
 
Back
Top Bottom