FYATU
JF-Expert Member
- Dec 7, 2011
- 5,867
- 5,064
Kama ni kweli ametamka au kuonyesha wasiwasi huo, basi namuunga mkono Nyalandu kwenye hili.
Na sijui ni kwa nini wengi mnakimbilia kumshutumu yeye ili tu ibaki kuwa kuna ukiukwaji wa haki za biinadamu wa kiwango kile ulifanyika....mnanufaika na nini ripoti ikiwa vile ?...na hata kama kuna ukiukwaji (siwezi kuwaamini watendaji wote kwa asilimia mia moja) lakini kwa ripoti ilivyo nadhani imepitiliza.
Ni uwezo gani wa ki taaluma ambao walikuwa nao wanakamati kuweza kuwahoji wahanga na kuridhika kwa yale wanayoongea ?
Watanzania tuna asili na vipaji vya kuzusha na kuongea uongo na tuna mifano lukuki.... ni juzi tu tumeambiwa kwamba samaki ameingia tumboni.....tuliwahi kuambiwa kuna mtu kageuka chatu.....tumewahi kusikia eti mbwa kazaa watoto wa nguruwe...ni wanainchi haohao ukipiga mbinja kijijini au mtaani kwamba bibi fulani ni mchawi watakupa ushirikiano wa hali ya juu wa kumuangamiza kikatili...ukiwaambia kuna babu anatibu ukimwi nchi nzima inahamia huko bila hata kujiuliza mara mbili n.k.
Ni wabongo nyie nyie mnaojitahidi kuiaminisha jamii kuwa mashahidi waliopelekea babu Seya kufungwa walipikwa...iweje kwenye hili uwezekano huo mmeutupilia mbali na wala hamtaki kusikia ? kuna nini hapa ?
Nitafurahi sana nikisikia kutoka kwa wale wote walioshiriki kwenye zoezi hili nao wakitoa maelezo yao....najua hawatokosekana waliokiuka maadili ya kazi lakini kamwe si kwa kiwango hiki.
Twajua kuna NGO zinazonufaika kwa uwepo wa sintofahamu hizi kwani wameshapeleka ripoti kwa wakubwa na wasingependa ipatikane ripoti tofauti na ile.