Nyalandu kuhamia CHADEMA ameisababashia kupata mpasuko mkubwa na humo ndani ni fataki na mtifuano tu

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,399
Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na kasi kubwa ya kuhama kwa wanachama wa Chadema hasa baada ya aliekuwa waziri wa maliasili na utalii bwana Lazaro Nyalandu kuhama CCM na kwenda Chadema.

Safari ilokuwepo kwa Chadema unazidi kupotea baada ya kumkaribisha Nyalandu mtu ambae ana lundo la tuhuma za ufisadi.

Kwa upinzani huo wa CDM sahauni habari ya Urais na kuingia Ikulu.

Ndani ya Chadema sasa hivi kuna mpasuko mkubwa wa kiutawala na maslahi na hakuna dalili za mwenyekiti kuachia kiti hicho ili kusiwepo na nadharia kwamba mwenyekiti Freeman Mbiwe naye ni dikteta ndani ya Chadema..

Chadema walimpoteza Dr Slaa na leo hii ameteuliwa kuwa balozi na mheshimiwa raisi John Magufuli.

Wale wote wanaotoka sasa Chadema kwenda CCM waliingia enzi za Slaa akiwa katibu mkuu makini ambae ni mtu mwenye msimamo na husimamia kile anachokiamini.

Fred Mpendazoe
Profesa Kitila Mkumbo.
Lawrence Masha
Patrobas Katambi
David Kafulila
Dr Wilbroad Slaa?
Samson Mwigamba
Albert Msando

Kitendo cha Chadema kula matapishi ya CCM ni kitendo kityakachokigharimu chama hiki na hata upinzani kwa ujumla.

Leo hii wale wote ambao wanajiondoa CCM kukimbia tuhuma za ufisadi, leo hii wanaonekana ni lulu kwa upinzani.

Mwizi na fisadi yoyote hawezi kukaa ndani ya CCM atatafuta pa kukimbilia, lakini ni kwanini isiwe mahali pengine bali Chadema?

Edward Lowasa alitajwa kuwa fisadi na Chadema na akafanywa mtaji mkubwa wa Chadema kiasi cha kumuondoa Dr Slaa.

Hakika nimeamini CCM ni mashine kubwa ya kutengeneza propaganda na zikaleta madhara makubwa sana.

Chadema amkeni kabla ya mambo hayajawa mazito zaidi na maji kufika shingoni.
 
Nini kifanyike ili kuzia CCM kuhonga wapinzani vyeo na fedha tasilimu?

Ni vigumu sana CCM iliyo chini ya Mgufuli kurudi tena kwenye mambo kama hongo, na ufisadi.

Kiukweli, ni Chadema ndiyo walomhonga Lazaro Nyalandu au siyo?

CCM kuna utaratibu wa kufanya mkutano wa halmashauri kuu kuwajadili waombaji uanachama.

Chadema sijaona wanafanya hivyo, mara tu tumeshuhudia Lowasa, Sumaye, mzee Ngombale Mwiru na Nyalandu wakikaribishwa bila wanachama kuridhia.
 
Ni kweli kabisa.
Na hii kauli ya mara kwa mara ya Lowasa ya kusema kuwa atagombea Urais inawakwaza wengi.

Ukizingatia kuwa kuna watu wengi ndani ya Chadema wenye sifa zaidi na nguvu na uwezo wa kujenga hoja.

Lowasa ashauriwe tu kuwa Urais wa mioyo ya watu ni heshima kubwa sana.
Aishie hapa hapo.

2020 mchuano aachie wengine ,akina Tundu, Nyalandu, Sumaye,Mbowe, Mdee, Heche jembe la kubota n.k

Pia ni wakati sasa wa kujipanga kiitikadi kwani CCM nayo haiko salama.
Vyuma vimekaza na wenyeji wanawekwa pembeni kwenye ulaji na vyeo.

Na ningetamani kuona Chadema yote inahamia CCM na CCM inakaa benchi waisome Namba kwa lugha za kiaramaini.

Wale chadema wanaoitwa kule kwa ajili ya kufanya manadiliko ya kweli ya nchi basi wasione nongwa kwenda kwani hii nchi sio ya urithi wa watoto wa vigogo wa CCM.

Mabadiliko mbele kwa mbele.
 
Hiyo kauli ya makalai aliitoa Patrobas na ni kauli nzito sana.
Hii kauli inaonekana ni kauli inayosemwa na vijana wa Bavicha kichinichini. Sidhani kama Katambi aliibuwa tu pale Ikulu. Kuna Bavicha wengi wanaoona wanatumika kama makalai lakini hawasemi wazi wazi. Kibaya ni kwamba uongozi wa juu wa Chadema watapuuzia madai ya Katambi. Lakini msemo wa makalai ndio umeshatoka hivyo.
 
Ni vigumu sana CCM iloyo chini ya Mgufuli kurudi tena kwenye mambo kama hongo, na ufisadi.

Kiukweli, ni Chadema ndiyo walomhonga Lazaro Nyalandu au siyo?

CCM kuna utaratibu wa kufanya mkutanio wa halmashauri kuu kuwajadili waombaji uanachama.

Chadema sijaona wanafanya hivyo, mara tu tumeshuhudia Lowasa, Sumaye, mzee Ngombale Mwiru na Nyalandu wakikaribihsw abila wanachama kuridhia.
Ni nani ambaye ana fedha za umma? Upinzani au chama tawala?
 
Ni wote.

Upinzani wanapewa fedha za umma kwa jina la ruzuku.

Actually, CCM wana miradi ya kujiendesha.

Je, Chadema wana miradi mingapi nje ya kutegemea fedha za ruzuku?
Upinzani ungekuwa na hela akina Masha na Kafulila wasingekimbia.
Slaa mwenyewe aliingiziwa muhamala wa mabilioni.
ZILE walizopewa madiwani waliohama sipendi kuzizungumzia ila kwa kifupi ni kuwa mfumo wa rushwa katika siasa umesharasimisha.Natabiri katika uchaguzi wa 2020 fedha nyingi ya umma itatumika kuratibu nani apate mgao wa rushwa.
 
Masha na Kafulila hawajaondoka Chadema kwa sababu ya fedha bali kutofahamu nini itikadi ya chama, malengo, Sera, na Ilani.

Dr Slaa aliondoka Chadema baada ya kuona kwamba hawezi kula matapishi yake mwenyewe aliyoyatoa viwanja vya Mwembeyanga.

Hakuwa tayari kuanza kumtetea tena Lwasa ambae yeye Dr Slaa aliwishwaambia watanzania kwamba ni fisadi na ana kashfa ya Richmond.

Hilo la kuhusu Udiwani na harakati za 2020 naona unaongelea dhana zaidi ya uhalisia.

Tatizo la dhana ni kuwa ukiamini sana hivyo hutaweza kuamini yale yanayotokea wakati huo hasa hili la Dr Slaa yuleyule kuchaguliwa kuwa balozi.

Ni jambo la hatari sana kuamini katika dhana au "assumptions".
 
Hebu acha uongo Mkuu! You’re better than this rubbish! Dah! Hivi kwa akili yako udikteta uchwara unaofanywa dhidi ya Chadema/UKAWA kupitia mtutu wa bunduki, wizi wa kura, kuzuiwa kufanya shughuli zao za kisasa, kupandikiziwa majambazi yanayopora vyama kwa nguvu ya dola jambazi Lipumba na majambazi wenzake, kutumia vyeo na pesa ili kutoa rushwa kununua wachumia tumbo kutoka upinzani unategemea kweli upinzani waingie Ikulu katika mazingira kama haya?

CUF walishinda uchaguzi lakini Kikwete akaingia usiku usiku Zenj siku ile ya uchaguzi kuyafuta matokeo yale yenye aibu kwake kama Mwenyekiti na Rais.

Chadema hakuna mpasuko hilo ni uzushi tu unaofanywa na wahuni na mafisadi ambao wanaihofia Chadema.

Tumieni mpasuko wa Chadema basi ili uchaguzi wa 2020 uwe huru na wa haki kupitia katiba mpya ya rasimu ya Warioba na Tume huru ya uchaguzi ili kuonyesha Watanzania na Walimwengu MACCM ni chama pendwa hakihitaji ushindi haramu wa kupitia mtutu wa bunduki na wizi wa kura toka kwa kitengo chenu cha wizi wa kura.

Eti umeamini CCM ni mashine kubwa!! Lakini wakati huo huo uovu unaofanywa na uchwara dhidi ya Watanzania huuoni!!! Bila shaka labda nawe umeanza kutafuta teuzi!! Si kwa speed hii ya kumsifia mwizi, fisadi, muongo, anayedharau wananchi, mahakama, Bunge, katiba, sheria za nchi, taratibu za manunuzi Serikalini na kujichotea trillions bila idhini ya Bunge.

Kampeni meneja wa Katambi, mwenyekiti wa BAVICHA Shinyanga Mjini aanika siri za katambi kuhamia CCM

Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na kasi kubwa ya kuhama kwa wanachama wa Chadema hasa baada ya aliekuwa waziri wa maliasili na utalii bwana Lazaro Nyalandu kuhama CCM na kwenda Chadema.

Safari ilokuwepo kwa Chadema unazidi kupotea baada ya kumkaribisha Nyalandu mtu ambae ana lundo la tuhuma za ufisadi.

Kwa upinzani huo wa CDM sahauni habari ya Urais na kuingia Ikulu.

Ndani ya Chadema sasa hivi kuna mpasuko mkubwa wa kiutawala na maslahi na hakuna dalili za mwenyekiti kuachia kiti hicho ili kusiwepo na nadharia kwamba mwenyekiti Freeman Mbiwe naye ni dikteta ndani ya Chadema..

Chadema walimpoteza Dr Slaa na leo hii ameteuliwa kuwa balozi na mheshimiwa raisi John Magufuli.

Wale wote wanaotoka sasa Chadema kwenda CCM waliingia enzi za Slaa akiwa katibu mkuu makini ambae ni mtu mwenye msimamo na husimamia kile anachokiamini.

Fred Mpendazoe
Profesa Kitila Mkumbo.
Lawrence Masha
Patrobas Katambi
David Kafulila
Dr Wilbroad Slaa?

Kitendo cha Chadema kula matapishi ya CCM ni kitendo kityakachokigharimu chama hiki na hata upinzani kwa ujumla.

Leo hii wale wote ambao wanajiondoa CCM kukimbia tuhuma za ufisadi, leo hii wanaonekana ni lulu kwa uipnzani.

Mwizi na fisadi yoyote hawezi kukaa ndani ya CCM atatafuta pa kukimbilia, lakini isiwe nai Chadema.

Edward Lowasa alitajwa kuwa fisadi na Chadema na akafanywa mtaji mkubwa wa Chadema kiasi cha kumuondoa Dr Slaa.

Hakika nimeamini CCM ni mashine kubwa ya kutengeneza propaganda na zikaleta madhara makubwa sana.

Chadema amkeni kabla ya mambo hayajawa mazito zaidi na maji kufika shingoni.
 
Masha na Kafulila hawajaondoka Chadema kwa sababu ya fedha bali kutofahamu nini itikadi ya chama, malengo, Sera, na Ilani.

Dr Slaa aliondoka Chadema baada ya kuina h=kwamba ahwezi kula matapishui yake mwenyewe aliyoyatoa viwanja vya Mwembeyanga.

Hakuwa tayari kuanza kumtetea tena Lwasa ambae yeye Dr Slaa aliwishwaambia watanzania kwamba ni fisadi na ana kashfa ya Richmond.

Hilo la kuhusu Udiwani na harakati za 2020 naona unaongelea dhana zaidi ya uhalisia.

Tatizo la dhana ni kuwa ukiamini sana hivyo hutaweza kuamini yale yanayotokea wakati huo hasa hili la Dr Slaa yuleyule kuchaguliwa kuwa balozi.

Ni jambo la hatari sana kuamini katika dhana au "assumptions".

Mkuu badala ya kujifunza propaganda nyepesi ulipaswa kujifunza kuandika kwanza.
 
Back
Top Bottom