Nyalandu kufa kisiasa kama Lowassa na Lembeli

Nyalandu kufa kisiasa kama Lowassa na Lembeli

Sidhani kama umefiria vyema kwa kusema yeye kajiona anapendwa sana na hakuna mtu mwingine zaidi yake..

Mtu kaamua kuutema ubunge na kuhamia chama kingine,tena chama pinzani chenye kuandamwa kwa uonevu na serikali pamoja na vyombo vya usalama bado una mawazo ya kuwa huyu mtu anahitaji Kiki ili abaki kwenye ramani za siasa !!!

Nyie na bashite wenu endeleeni kutafuta kiki kila leo ili msipotee kwenye ramani za siasa,tunanataka tuone mpk mwisho wenu ukoje

Na hayo maneno yenu muyasemege wakiwa bado wamo kwenye chama chenu,mnachofanya sasa ni sawa na mwanamke baada kuachwa ndo anapata kujua kwamba jamaa ana kibamia.....uuffffff !!!!!!

Kama hakutaka kiki za siasa angejiuzulu tu akakaa pembeni. Kwani zile kauli zake alizozitoa akijiuzulu hukuzisikia kwamba zililenga kuendeleza siasa katika mlengo mwingine? Hayo mengine ni maneno ya khanga tu
 
Lakini cha kushangaza waliojifanya wanapinga wizi wa mali za umma, ndio kwanza wanawapokea wezi na wabadhirifu wa mali hizo kama mashujaa. Kwa kweli ni ngumu sana kuwaelewa hawa wanaharakati wa upinzani
Kama raisi mwenyewe ambaye anapewa sifa za uzalendo kwa kujifanya anatetea rasilimali za nchi,mwaka wa pili sasa madarakani lkn hajamchukulia hatua zozote kisheria kwanini CHADEMA wasimpokee
 
Hao wote walidhani wanapendwa sana, kumbe watu walipenda mfumo na components parts zake. Being isolated as a component of a system waliona vividly kwamba watu hawawapendi wao as individuals
....Kura za Ukawa kupitia Lowassa zilitokana na mfumo au influence ya Lowassa as an individual? Kura za Magufuli was it due to ccm or himself? Unajua ni kwa nini kauli mbiu yake ilikuwa chagua Magufuli?
 
Kama hakutaka kiki za siasa angejiuzulu tu akakaa pembeni. Kwani zile kauli zake alizozitoa akijiuzulu hukuzisikia kwamba zililenga kuendeleza siasa katika mlengo mwingine? Hayo mengine ni maneno ya khanga tu
Maneno ya khanga mnaleta nyie mtu akihama chama mnaleta maneno kana kwamba mlikuwa hamumjui wakati alipokuwa CCM ila siku mbili tu za kuhama mmemjua nje ndani....kima nyie
 
Nimemsikia Spika wa bunge Job Ndugai akisema hatambui kujiuzulu kwa mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu na kwamba akienda bungeni wakati wowote atampokea!

Maswali yangu ni je,
1. CCM watampokea?
2.Yale matusi waliomtukana watayafutaje?
3.Tuhuma za ufisadi walizomtupia watamsafishaje?
4.Mzee Polepole akiitisha press conference atatuambia mini?

Tunajua juhudi za kumbembeleza Nyalandu abatilishe uamuzi wake zinaendelea na kazi hiyo amepewa spika wa bunge Ndugai.Pamoja na spika wa bunge kupokea barua ya Nyalandu ya kujiuzulu amegoma kukiri hadharani kwa matumaini kwamba atabatilisha uamuzi wake.Tusibiri kuona kama Nyalandu atabadili via angani kama Lipumba au atashikilia msimamo wake.
 
Edo kaisha kisiasa? Unafikiri kwa nini siasa zinazuiwa, yale mafuriko yako pale pale, na yanaogopwa sana
 
Lazaro Nyalandu naye inaonekana amefanya kosa linalofanana kabisa na kosa lililofanywa na akina Lowassa na Lembeli. Ni kosa la kudhani kwamba unapendwa sana na unamashabiki wengi ambao wataambatana na wewe popote utakapokuwa. Ni kosa la kuona kwa “hakuna mtu mwingine” zaidi yako atakayeweza kufanya kile ulichokuwa ukikifanya katika ubora uleule au hata zaidi yako. Ni kosa la “miscalculation” na kuwa “overoptimistic” juu yako mwenyewe.

Kilichowapata Lowassa na Lembeli sote tunajua. Sasa wamepotea kabisa katika uringo wa siasa, hakuna anayewataja tena. Watu waliodhani kwamba wangewafuata kule waliko, waliamua kubaki ndani ya hema la CCM ambako waliona ni salama zaidi ya kwenda wasikokujua. Hakika lilikuwa ni kosa kubwa la kujivika “Umungu Mtu” lililopelekea kufa kabisa kisiasa.

Cha ajabu sana tena sana, Lazaro naye amecheza mchezo huo kwa namna ile ile ulivyochezwa na L&L. Mwalimu Nyerere alipata kusema, kuna wakati mtu unajiita au kuitwa vile unavyojiita au kuitwa kwa sababu ya mfumo uliopo ndani yake; nje ya huo mfumo si wewe tena; akitumia maneno “Nje ya Muungano hakuna Mzanzibari ila kuna Muunguja na Mpemba”. Hawa 3L’s wameshindwa kuliona hilo kabisa, kwamba wanatazamwa vile walivyo wakiwa ndani ya mfumo uliowajenga, nje ya hapo they are not the same. Zaidi ya hapo Lazaro alishindwa kukumbuka kwamba, yeye katika uringo wa siasa aliibuka tu kama uyoga, hakuwa na background strong sana kama akina Lowassa ambao pia wamepotezwa, lakini bado akashupaa shingo na kudanganyika kwamba ataendelea kuwa on top hata ndani ya mfumo mpya. Goodbye forever Lazaro, tutai-miss sana sauti yako Bungeni.
Kwani lazima uwe kwenye siasa kila mara. Kila moja anayohaki ya kujiamulia mambo yako na kuona inayomfaa. Akifa kisiasa c anakufa yeye tatizo ni nini c wataibuka wengine. Kila kitu na zama zake
 
Ningekua mimi narudi kupima upepo kama hassan dalali
 
....Kura za Ukawa kupitia Lowassa zilitokana na mfumo au influence ya Lowassa as an individual? Kura za Magufuli was it due to ccm or himself? Unajua ni kwa nini kauli mbiu yake ilikuwa chagua Magufuli?

Kwani mlipozungusha mikono mliimba MABADILIKO nani vile??? Kwa nini msingesema mabadiliko UKAWA???
 
Kuna wanasiasa na wanaharakati pia wakubebwa kwa elimu zao mtu kama muhongo sio mwanasiasa anabebwa na elimu yake na wapo wengi ccm uwepo wao ni elimu na rushwa zimewafikisha hapo walipo sasa kutomsikia coz awezi kujigamba au majukwaa kwao ni adhabu kwaiyo usishangae kwa hayo mtu kama nape aende popote utamsikia coz ategemei tukio so kua mpinzani lazima ujiweze kwa kila kitu la sivyo utapotea tofauti na ccm chama pamoja na udola utakubeba
 
Lazaro Nyalandu naye inaonekana amefanya kosa linalofanana kabisa na kosa lililofanywa na akina Lowassa na Lembeli. Ni kosa la kudhani kwamba unapendwa sana na unamashabiki wengi ambao wataambatana na wewe popote utakapokuwa. Ni kosa la kuona kwa “hakuna mtu mwingine” zaidi yako atakayeweza kufanya kile ulichokuwa ukikifanya katika ubora uleule au hata zaidi yako. Ni kosa la “miscalculation” na kuwa “overoptimistic” juu yako mwenyewe.

Kilichowapata Lowassa na Lembeli sote tunajua. Sasa wamepotea kabisa katika uringo wa siasa, hakuna anayewataja tena. Watu waliodhani kwamba wangewafuata kule waliko, waliamua kubaki ndani ya hema la CCM ambako waliona ni salama zaidi ya kwenda wasikokujua. Hakika lilikuwa ni kosa kubwa la kujivika “Umungu Mtu” lililopelekea kufa kabisa kisiasa.

Cha ajabu sana tena sana, Lazaro naye amecheza mchezo huo kwa namna ile ile ulivyochezwa na L&L. Mwalimu Nyerere alipata kusema, kuna wakati mtu unajiita au kuitwa vile unavyojiita au kuitwa kwa sababu ya mfumo uliopo ndani yake; nje ya huo mfumo si wewe tena; akitumia maneno “Nje ya Muungano hakuna Mzanzibari ila kuna Muunguja na Mpemba”. Hawa 3L’s wameshindwa kuliona hilo kabisa, kwamba wanatazamwa vile walivyo wakiwa ndani ya mfumo uliowajenga, nje ya hapo they are not the same. Zaidi ya hapo Lazaro alishindwa kukumbuka kwamba, yeye katika uringo wa siasa aliibuka tu kama uyoga, hakuwa na background strong sana kama akina Lowassa ambao pia wamepotezwa, lakini bado akashupaa shingo na kudanganyika kwamba ataendelea kuwa on top hata ndani ya mfumo mpya. Goodbye forever Lazaro, tutai-miss sana sauti yako Bungeni.
 
Kuna wanasiasa na wanaharakati pia wakubebwa kwa elimu zao mtu kama muhongo sio mwanasiasa anabebwa na elimu yake na wapo wengi ccm uwepo wao ni elimu na rushwa zimewafikisha hapo walipo sasa kutomsikia coz awezi kujigamba au majukwaa kwao ni adhabu kwaiyo usishangae kwa hayo mtu kama nape aende popote utamsikia coz ategemei tukio so kua mpinzani lazima ujiweze kwa kila kitu la sivyo utapotea tofauti na ccm chama pamoja na udola utakubeba

Umenena vema mkuu. Kwa kweli kuna wanasiasa wasiojua kabisa kwamba mfumo ndio unaowabeba, na nje ya mfumo huo they are almost dead. Na utakuta muda mwingi wanacheza tu na akili zetu.
 
Kwani ikiwa Lowassa na Lembeli hawatajwi, umesikia wanalala njaa.
Ni heri usitajwe pembeni peke yako kuliko kutajwa pamoja na jamii ya akina Mussolin, Bokkasa, Idd Amin nk
 
Kwani ikiwa Lowassa na Lembeli hawatajwi, umesikia wanalala njaa.
Ni heri usitajwe pembeni peke yako kuliko kutajwa pamoja na jamii ya akina Mussolin, Bokkasa, Idd Amin nk

Wala hakuna aliyesema LN atalala njaa, tusilishane maneno. Kama siasa kwake siyo muhimu kwa nini anacheza na akili zetu si aende tu akafanye shughuli zake nyingine?
 
Lakini cha kushangaza waliojifanya wanapinga wizi wa mali za umma, ndio kwanza wanawapokea wezi na wabadhirifu wa mali hizo kama mashujaa. Kwa kweli ni ngumu sana kuwaelewa hawa wanaharakati wa upinzani
Hatuna wapinzani tuna wasanii tu na waganga njaa
Sasa hivi zitto kageuka kuwa shujaa wa chadema
 
Bado siamini kama kweli Tanzania kuna upinzani wenye nia ya dhati kabisa ya kutengeneza mfumo bora wenye utofauti na wa chama tawala.
Kama mnatuwekea watu wale wale kutoka chama tawala waliokuja kwenye chama chenu hapo hakuna mfumo/UONGOZI mpya utakaokuwepo zaidi.
Kama mantiki hiyo kuliko kuchanganya CHADEMA na CCM ni bora kuwa na CCM iliyoimara tu.
 
Kwa kweli ndugu, kuna wanasiasa wakihama chama wanajivika utakatifu sana kumbe sivyo walivyo kutokana na rekodi za utendaji wao.
 
Bado siamini kama kweli Tanzania kuna upinzani wenye nia ya dhati kabisa ya kutengeneza mfumo bora wenye utofauti na wa chama tawala.
Kama mnatuwekea watu wale wale kutoka chama tawala waliokuja kwenye chama chenu hapo hakuna mfumo/UONGOZI mpya utakaokuwepo zaidi.
Kama mantiki hiyo kuliko kuchanganya CHADEMA na CCM ni bora kuwa na CCM iliyoimara tu.

Bila CCM kuwa chama cha upinzani hakuna Tanzania ya kesho zaidi ya kuparaganyika kwa umoja wa kitaifa na kulinda maslahi ya chama cha mapinduzi.

Wewe ni shahidi kuwa ili pawe na dira nzuri ya kitaifa ;kiuchumi, kisiasa na kijamii ni lazima pawe na mjadala mpana wa kitaifa.
Ili pawe na bunge imara lenye kujali maslahi ya Taifa na sio maslahi ya mtu mmoja na wateule wake ni lazima nguvu ya CCM ipungue bungeni.

Ili pawe na Mahakama inayofanya kazi yake vizuri na kwa kujali haki ya kila mtu ni lazima Wateule wa mhimili huo watokana na mhimili huo zaidi na sio wanasiasa na watawala.

Ni wazi kuwa kila mtu anafanya kazi kwa hofu ya mwenye uwezo wa kumtoa saa yoyote anayotaka.
Leo hii hata mwanaCCM mwenye mawazo tofauti ana hofu mana mwenyekiti wake ndiye aliyeshika vyombo vyote vya dola. Ana nafasi za uteuzi wenye maslahi bora zaidi ya mamia.
Nguvu ya nchi nzima imewekwa nikonini mwa mtu mmoja.
Nyuma yake kiko chama kimoja chenye nguvu kubwa na hakina watu wenye maono ya kuona kosa kubwa la kuiweka nchi chini ya mtu mmoja. Yani ni uamuzi wake tu kuwa awe na hulka gani.!
Ni hatari sana naamini iko siku tutampata mtu chini ya mfumo huu wa CCM atatokea mtawala mbaguzi na mdini ambaye atawateua watu wote kwa itikadi yake na atatumia nguvu kuwanyamazisha watakaojaribu kumkosoa na kumpinga na CCM na wabunge wake kwa sababu ya kuhofia nafasi zao watakaa kimya nchi itaangamia.

Nakumbuka awamu ya nne ilikuja ishu ya Mahakama ya kadhi.
Kama Kikwete angekua ni mbinafsi na mdini angeweza kutumia nguvu kubwa na wingi wa watu wa dini yake na nguvu yake kikatiba kuipitisha ile sheria na anheweza kumnyamazisha yeyeote ambaye angejaribu kupingana na ile ilani ya Chama cha mapinduzi ya kuanzisha mahakama ya kadhi.
Hata hivyo kwa uzalendo wake wa kweli na upendo wake kwa watanzania wa dini zote aliamua kusikiliza mashinikizi na matamko ya watu nje ya CCM na nje ya Bunge zaidi aliangalia umoja wa watanzania. Chama chake kilitaka hiyo mahakama iwepo kwa ajili ya kupata kura. Lakini JK aliangalia maslahi ya nchi hakusema kuwa ni lazima hiyo mahakama ianzishwe kwa kuwa waliompa kura wengi wao waoiitaka.

Ili tuwe na dira imara ya kisiasa ni lazima CCM iwe chama cha upinzani.
CCM wakikaa pembeni wataweka shinikizo kwa serikali ya chama kingine ili pawe na usawa na kila mtu aheshimike.
Watapinga na kukataa kuona adha ya kubaguliwa na iunyanyaswa kwa sababu ya kutoa mawazo yao. Watataka haki za watu zilindwe .
Watapinga suala la watawala kuweka sheria ngumu kwa wananchi ili hali watawala wakiwa wanazuia kila aina ya kukosolewa na wale wanaolipa kodi zao ili waishi maisha bora na ya kifahari.

CCM ikiwa chama cha upinzani naamini kuwa kitakua ni chama chenye nguvu kubwa ambacho hakitakubali kunyamazishwa kwa manufaa ya watawala wa chama kingine.

CCM ikiwa chama cha upinzani naamini kuwa watapenda kuona kuwa Mahakama inakuwa huru ili mtu au taasisi ikidhulumiwa na watawala basi watapata pa kukimbilia na haki itapatikana.

Hebu fikiri kama CCM ingekuwa ndio chama cha upinzani chenye wabunge 47% halafu nyumba zenye zuio la mahakama zinabomolewa na hakuna mtu aliyewajibishwa kwa kuidharau amri ya mahakama na akatakiwa kulipa fidia kwa wahanga.

Haki haitaweza kushamiri kama CCM itajiona ndicho chama bora duniani na kinajua watanzania wengi bado hawana elimu ya kutosha kupambanua mambo.
 
Kuna mambo hata ujifanye hutaki kuyasikia, lakini ukweli wake utabaki pale pale. Najua unalitambua hilo kwa sababu liko wazi kibisa
Ifike mahali mtwambie mafisadi kabla hayajahama sisiem. Msisubiri wakiondoka ndo muwatangaze mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom