Nyalandu kufa kisiasa kama Lowassa na Lembeli

Kinachoniuma ni kuwa watu mnamshangilia blindly, wakati hapo awali vilevile mlikuwa mkimponda kwamba anawapandisha ndege Twiga na wanyama wengine. Kweli, nimeamini ukiwa CDM hata uwe mwizi basi wewe ni shujaa. Mie madarasa nishamaliza ndugu yangu. I don't need any more classes
ufipa wana matatizo sana ,wasamehe tu
 
Lazaro Nyalandu naye inaonekana amefanya kosa linalofanana kabisa na kosa lililofanywa na akina Lowassa na Lembeli. Ni kosa la kudhani kwamba unapendwa sana na unamashabiki wengi ambao wataambatana na wewe popote utakapokuwa. Ni kosa la kuona kwa “hakuna mtu mwingine” zaidi yako atakayeweza kufanya kile ulichokuwa ukikifanya katika ubora uleule au hata zaidi yako. Ni kosa la “miscalculation” na kuwa “overoptimistic” juu yako mwenyewe.

Kilichowapata Lowassa na Lembeli sote tunajua. Sasa wamepotea kabisa katika uringo wa siasa, hakuna anayewataja tena. Watu waliodhani kwamba wangewafuata kule waliko, waliamua kubaki ndani ya hema la CCM ambako waliona ni salama zaidi badala ya kwenda wasikokujua. Hakika lilikuwa ni kosa kubwa la kujivika “Umungu Mtu” lililopelekea kufa kabisa kisiasa.

Cha ajabu sana tena sana, Lazaro naye amecheza mchezo huo kwa namna ile ile ulivyochezwa na L&L. Mwalimu Nyerere alipata kusema, kuna wakati mtu unajiita au kuitwa vile unavyojiita au kuitwa kwa sababu ya mfumo uliopo ndani yake; nje ya huo mfumo si wewe tena; akitumia maneno “Nje ya Muungano hakuna Mzanzibari ila kuna Muunguja na Mpemba”. Hawa 3L’s wameshindwa kuliona hilo kabisa, kwamba wanatazamwa vile walivyo wakiwa ndani ya mfumo uliowajenga, nje ya hapo they are not the same. Zaidi ya hapo Lazaro alishindwa kukumbuka kwamba, yeye katika uringo wa siasa aliibuka tu kama uyoga, hakuwa na background strong sana kama akina Lowassa ambao pia wamepotezwa, lakini bado akashupaa shingo na kudanganyika kwamba ataendelea kuwa on top hata ndani ya mfumo mpya. Goodbye forever Lazaro, tutai-miss sana sauti yako Bungeni.

Ni kosa kama lengo kuu ni mafanikio ya kisiasa, lakini kama lengo ni haki na maendeleo basi siasa inakuwa ni 'vehicle' tu au mbinu ya kufikia hapo. Unapong'ang'ania 'vehicle' au mbinu au mafanikio kisiasa badala ya kisimamia lengo (purpose and principals) basi huna dira unakuwa ni sawasawa na mtu anapigania ramani ya nyumba badala ya nyumba yenyewe
 
lowasa kuisha kisiasa hizo ni taarifa za mwendawazimu, hebu ccm waweke watu uwanja wa uhuru na cdm waweke watu uwanja wa taifa ndio utajua kwanini anaitwa 'mzee wa mafuriko".
Labda kama bado amevaa lile pete la kipepo from Nigeria otherwise hana lolote na hakuna hata anaemuwaza KWISHA HABARI YAKE GADEEEEEEEEEEEEEEEEM.
 
Oktoba 30, 2017 Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu atangaza kujivua Ubunge wa Jimbo hilo. Amesema CCM imepoteza uelekeo na kuomba Wanachama wa CHADEMA kama wataona inafaa wamkaribishe.

Nyalandu ametoa sababu zilizomfanya ahame na Watu wengineo nao pia wametoa sababu za kuhama kwa Nyalandu lakini ukweli unabaki palepale Nyalandu ametumia haki yake ya msingi kabisa ya kwenda sehemu anayoamini ni sahihi kwake.

Hama hii ya Nyalandu haiwezi kuleta madhara yeyote kwa Chama Cha Mapinduzi ama kwa Serikali kwa sababu si mara ya kwanza kwa Wanachama au waliokuwa viongozi waandamizi wa chama na Serikali kuhama CCM lakini bado CCM ikaendelea kuwa imara.

CCM imeshapita kwenye majaribu mazito kadhaa lakini bado ikaendelea kuwa imara kabisa. Tuweke sawa kumbukumbu. Mathalani mwaka 1968, aliyekuwa Katibu Mkuu wa TANU na wa pekee, Oscar Kambona ; aliyekuwa Mwenyekiti wa kwanza wa UWT, Bibi Titi Mohammed; Katibu Mwenezi wa TANU, na Mbunge wa Geita Mashariki, Fortunatus L.Masha; Katibu Mkuu wa TANU Youth League “TYL” na Mbunge wa Rungwe , Elli Anangisye walifukuzwa ndani ya chama kutokana na utovu wa nidhamu ukiwamo na kutuhumiwa kwa kutoliafiki azimio la Arusha waliloshiriki kulipitisha. Kwa tuhuma hiyo, Halmashauri Kuu (T) ya TANU ilipokaa Tanga haikutaka ushahidi zaidi wa juu ya uwaminifu wao katika chama, zaidi ya kuwafukuza ndani ya chama lakini TANU.

Tuendelee kukumbuka sakata la Seif kufukuzwa na wenzake sita mwaka 1987 lakini CCM ikaendelea kuwa imara na kushika hatamu zaidi.

Halikadhalika aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Horace Kolimba kuvuliwa wadhifa mwaka 1994 kutokana na kauli yake aliyoisema ya kuwa CCM imepoteza dira. Katibu Mkuu CCM alitimuliwa lakini bado Chama kiliendelea kuwa imara kabisa na kushinda kwa kishindo uchaguzi mkuu wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995 na hatimaye kushika dola.

Tusisahau sakata la Rais wa pili wa Zanzibar, Aboud Jumbe la kutaka Muungano uvunjwe na katiba ya nchi ibadilishwe, hali iliyochafua hali ya hewa visiwani Zanzibar. Kitendo hicho kilimkera sana Mwasisi wa Muungano na baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na kuamua kumpa adhabu kali Mzee Jumbe, hali iliyozua kizaazaa lakini mwishowe CCM iliendelea kuwa imara na kushinda uchaguzi na kuendelea kushika dola.

Pia tuendelee kukumbuka sakata la kundi la G55 na hatma ya uongozi wetu. G55 lilikuwa ni kundi lililoibuka Bungeni miaka ya 1990 hadi 1992 lililokuwa na nguvu kubwa sana lililokuwa likidai Serikali 3. Kundi hili lilikuwa likiongozwa na viongozi wazito ndani na nje ya Bunge kama akina Njelu Kasaka, Philipo Marmo, Masumbuko Lamwai na wengineo lilizua mtikisiko mkubwa lakini hekima na busara za Mwalimu Nyerere zilisaidia kutuliza hali ya hewa. Licha ya mazito hayo lakini bado CCM iliendelea kuwa imara, kushinda chaguzi na kushika dola.

Tuendelee kukumbuka dhoruba kali lililotokea mwaka 2015 kwenye uchaguzi mkuu uliopelekea Mawaziri wakuu wastaafu wawili na viongozi wazito waandamizi wa Serikali na chama kuhama CCM na kujiunga na chama cha upinzani lakini mwisho wa siku CCM iliendelea kuwa imara, ikashinda vita ya uchaguzi na hatimaye kushika dola.

Suala la kuhama kwa Nyalandu lisiwe gumzo la kupelekea baadhi ya watu kumuweka kwenye level tofauti ya juu sana kisiasa na kuishusha hadhi CCM na Serikali yake. Wakati wakiyafikiria hayo wajiulize wako wapi waliohama kwa mbwembwe mwaka 2015? Wako wapi waliotikisa sakata la G55? Kati yao na CCM nani anaendelea kuwa lulu? Ukipata majibu ya maswali hayo utagundua kuhama kwa Nyalandu si lolote, si chochote!!

Nyalandu si wa kwanza, wala si wa mwisho kuihama CCM. Nyalandu ametumia haki yake ya kikatiba kabisa ya kuchagua anachotaka lakini anapokosea yeye ni kuondoka na kuanza kushusha kebehi na lugha za kuudhi kwa kusema CCM na Serikali ya sasa imepoteza dira. Kwa kauli hii, unadhani wana CCM watakaa kimya wasimshambulie Nyalandu? Angeondoka kimya kimya bila lugha ya kuudhi angepungukiwa na nini?

Nyalandu anaposema CCM imepoteza dira nashindwa kuielewa hiyo dira yake anayoimaanisha. CCM anayodai imepoteza dira ndio hiyo hiyo inayoisimamia Serikali inayotoa elimu bure kuanzia shule ya msingi, hadi Sekondari; ndio Serikali inayotoa mikopo ya elimu ya juu kwa Wanafunzi wanaostahili; inayofuta kodi na kuboresha kilimo nchini; Inayonunua vifaa tiba na madawa hospitalini; Inayojenga hostel za wanafunzi; Inayonunua ndege 6 mpya; Inayojenga reli ya kisasa ya standard gauge; Inayosimamia rasilimali madini ziwanufaishe watanzania wote; Inayojenga miundombinu na kuboresha huduma za kijamii kila sehemu nchini; Inayoboresha mapato ya ndani na mengineyo kibao.
Kwa hayo baadhi tu ya machache niliyoyataja yanayoonyesha Matokeo chanyA+ ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi. Hivi utasemaje CCM hii imepoteza dira? Utasemaje Serikali hii imepoteza dira? Haoni uelekeo wa CCM?

Nyalandu ni lazima ajiulize yuko wapi Lawlence Masha, yuko wapi Kingunge, yuko wapi Mgeja, yuko wapi James Lembelii, yuko wapi Sumaye? Inabidi awatazame hawa walipo, naye atajua atakapokuwepo katika hali na nafasi ya kisiasa nchini.

Emmanuel J. Shilatu
01/11/2017

Safi sana mkuu kwa bandiko zuri, lenye kutoa elimu ya kina kwa wale ambao akili zao zipo tayari kujifunza.
 
Spika amepokea barua ya ccm kumtimua Nyalandu tokea tarehe 30 Nov.Inaelekea Nyalandu alinusa kufukuzwa akawahi kutangaza kujiuzulu,bahati mbaya barua ya ccm imewahi bungeni kabla ya Nyalandu

Bongo movie hiyo though kaondoka kwa maneno yenye kutaka jamii kumuonea huruma au kumuunga mkono. Kali ya mwaka hiyo
 
Back
Top Bottom