Nyalandu in support of operation TOKOMEZA

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,162
2,000
Naibu waziri wa maliasili na utalii mh Nyalandu amesema matukio ya ujangili yameongezeka mara baada ya kusutishwa kwa operesheni ya 'kihalifu dhidi ya ubinadamu-operesheni Tokomeza.
Amesema jumla ya tembo 60 wameuawa na pia kuna matukio ya kushambuliwa kwa maafisa wa maliasili na utalii,haya yametokea kuanzia novemba mosi.
Hii inamaanisha naibu waziri bado anaamini operesheni hii ni ya mafanikio licha ya udhalimu ulioonekana.

UHALISIA WA JAMBO HILI NI UPI?

Nyalandu hajaeleze ni tembo wangapi au maafisa wangapi waliathiriwa na majangili katika kipindi cha mwezi novemba mpaka disemba mwaka 2012 au 2011 au 2010?

Nyalandu au tume ya Lembeli hawajaeleza mafanikio ya operesheni hii kwa kuangalia kwa ulinganifu(comperative analysis) idadi ya waathirika wa ujangili(iwe ni watu,miti au wanyama) kabla na baada ya operesheni TOKOMEZA!
 
fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
CCM imeshindwa kuwakamata wanaoua tembo zetu??? semeni hadharani wananchi wajue nini cha kufanya, tembo hawa walikuwepo kabla ya CCM, so wananchi wanajua na wanauwezo wa kufanya kama CCM imeshindwa
 
OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,160
1,250
Operesheni inatakiwa kuendelea kwa kurekebisha mapungufu!!!!!!

Hili wala haoihitaji mjadala isipokuwa kwa wanufaika na ujangili
 
kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,728
1,225
Majangili ndio walitesa na kuua watu ili operation isitishwe, cha kushangaza Kinana ndiye aliyereport kuhusu huo unyama na kuomba operation isitishwe (according to Makonda), what a concidence, na muda huu tembo watauawa kwa ari na kasi ya aina yake.

Ni Mungu pekee ndio anaweza kuwanusuru hawa tembo lakini si serikali ya CCM ambayo inafaidika na biashara hii.
 
Comi

JF-Expert Member
Oct 2, 2011
3,329
1,500
Hakuna haja ya operation ilihali wahusika wanafahamika na wanakumbatiana. Madawa ya kulevya, ujangili,ufisadi vyote hivyo vyanzo vyake vinajulikana na wahusika wanajulikana ila sababu ni miradi ya viongozi ndiyo maana kila leo tunapewa nyimbo mpya
 
Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
11,207
2,000
SEREKALI YA AJABU ZOEZI LA TOKOMEZA UJANGILI HALIKUPASWA KUSITISHWA ONA VIUMBE WENZETU 60 WAMEUWAWA BILA HATiA
 
Chris Lukosi

Verified Member
Aug 23, 2012
4,584
2,000
Hata mimi nasapoti hiyo operesheni kwani majangiri wamekuwa kero sana na wana roho kama shetani tu

Mimi ukinipa bunduki nikikutana na jangiri namuwasha ya makalio tu kwa sababu nikimuacha ataniua
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,614
2,000
Hata mimi nasapoti hiyo operesheni kwani majangiri wamekuwa kero sana na wana roho kama shetani tu

Mimi ukinipa bunduki nikikutana na jangiri namuwasha ya makalio tu kwa sababu nikimuacha ataniua

maccm mna kiu sana ya kuua.

ila rambirambi mkuu zinaku . . . . . .
 
Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
5,930
2,000
Hata mimi nasapoti hiyo operesheni kwani majangiri wamekuwa kero sana na wana roho kama shetani tu

Mimi ukinipa bunduki nikikutana na jangiri namuwasha ya makalio tu kwa sababu nikimuacha ataniua
Tukianzisha operesheni Tokomeza mafisadi mtuunge mkono pia!
 
ilboru1995

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,329
0
Majangili ndio walitesa na kuua watu ili operation isitishwe, cha kushangaza Kinana ndiye aliyereport kuhusu huo unyama na kuomba operation isitishwe (according to Makonda), what a concidence, na muda huu tembo watauawa kwa ari na kasi ya aina yake.

Ni Mungu pekee ndio anaweza kuwanusuru hawa tembo lakini si serikali ya CCM ambayo inafaidika na biashara hii.
Well said Mkuu, chakushangaza Nyalandu anajulikana kuwa yeye ni mmoja wapo wa beneficiary wa meno ya Tembo, wakati wa operation alikuwa anatoa siri kwa majangili sasa hivi anajinasibu kuwa eti anauchungu na hao Tembo... tunajua kuwa anaogopa kuondolewa kwenye hiyo nafasi si zaidi ya hapo...
 
The Prezident

JF-Expert Member
Jul 2, 2013
459
195

Mkuu umeona jambo kubwa. Na ni.mpango kabambe.
 
iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,230
2,000
Well said Mkuu, chakushangaza Nyalandu anajulikana kuwa yeye ni mmoja wapo wa beneficiary wa meno ya Tembo, wakati wa operation alikuwa anatoa siri kwa majangili sasa hivi anajinasibu kuwa eti anauchungu na hao Tembo... tunajua kuwa anaogopa kuondolewa kwenye hiyo nafasi si zaidi ya hapo...
Kuna harufu ya chuki binafsi hapa.
 
iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,230
2,000
Yaliyotokea bungeni yamewavunja moyo sana askari wa wanyamapori. Kazi ya kulinda wanyama siyo rahisi kama tunavyodhani. Unapokuwa porini una adui wawili. Wanyama hawajui kama unawalinda hivyo ukikaa vibaya wanakumaliza. Jangili akikuwahi anakupiga shaba. Askari akipigwa shaba na jangili hakuna tume itaundwa. Ila askari akimuwahi jangili na kumpa shaba tume zitaundwa. Katika mazingira haya hata kama ni mimi naweka silaha chini.

Watanzania tumekuwa watu wa ajabu. Tume ya lembeli wameenda kuhoji majangili, unategemea watasema nini. Baadhi ya picha zilizotumika hazihusiani kabisa na operation. Lembeli and Co. Walikuwa na ajenda yao. Bahati mbaya wabunge nao wakaunga mkono.

Nawaambieni tume ya kimahakama ikiundwa Lembeli ataumbuka. Ingawa haitaweza ku reverse madhara yaliyopatikana na upotoshaji wao lakini ukweli utajulikana.
 
Ogah

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
6,238

.....ndio maana kuna taarifa zinasema Ripoti ya tume ya Lembeli ina mapungufu....kwani imeangalia zaidi upande mmoja tu.......iundwe tume huru kabisa na watu wote wahojiwe......hizi tume zingine za Bunge zimekaa "kimagumashi"......
 
Ogah

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
6,238
2,000
Hivi Nyalandu ni Naibu Waziri wa Utalii? au ni Naibu Viwanda na Biashara?.......au sasa hivi anakaimu Uwaziri wa Utalii?
 
Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
5,930
2,000
Hivi Nyalandu ni Naibu Waziri wa Utalii? au ni Naibu Viwanda na Biashara?.......au sasa hivi anakaimu Uwaziri wa Utalii?
Does it matter?!
La msingi ni kwamba ameunga mkono operesheni Tokomeza!
 
mapinduzi daima

JF-Expert Member
Sep 30, 2013
1,582
2,000
Hivi Nyalandu ni Naibu Waziri wa Utalii? au ni Naibu Viwanda na Biashara?.......au sasa hivi anakaimu Uwaziri wa Utalii?

Ni Naibu wa Waziri wa Utaliii na Kaimu Waziri wa Utaliii...baada ya Bosi wake Kagasheki kujiuzulu.
 
iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,230
2,000
.....ndio maana kuna taarifa zinasema Ripoti ya tume ya Lembeli ina mapungufu....kwani imeangalia zaidi upande mmoja tu.......iundwe tume huru kabisa na watu wote wahojiwe......hizi tume zingine za Bunge zimekaa "kimagumashi"......
Mpaka leo sijui ni nani na katika mazingira gani bunge lilipewa nguvu za kisheria kuunda tume za uchunguzi. Kuna vyombo vya serikali kwa ajili ya kazi hiyo. Wabunge hawana taaluma ya kuchunguza. Mbaya zaidi wanachunguza wao na kutoa hukumu wao.

Nafikiri ingekuwa vyema wakaachia vyombo vya uchunguzi kufanya hivyo na wao wakapelekewa report na kuijadili.

Uzoefu wangu na hizi tume unaonyesha kuwa zinakuwa na mlengo wa kisiasa kwa ajili ya kuwakomoa watu fulani. Bahati mbaya zaidi watuhumiwa hawapewi nafasi ya kusikilizwa.

Kwa mfano ingekuwa busara report za namna hiyo zinaposomwa mawaziri husika wanapewa nafasi ya kuwasilisha hoja zao kabla ya wabunge kuanza kujadili. Hii ingetoa nafasi kwa wabunge kusikiliza pande zote kabla ya kuanza kutoa michango yao.

Kuwapa nafasi mawaziri mwishoni wakati mijadala imesha kamilika siyo haki kabisa.

Na kama hali hii itaendelea basi tutakuwa tunashuhudia mawaziri wakiondoka kila kikao cha bunge.

Ingawa watu wengi hufurahia kung'oka kwa mawaziri lakini kimsingi faida inayopatikana ni ndogo sana kulinganisha na hasara. Waziri huitaji kati ya miezi 6 hadi mwaka ili kujifunza mambo ya wizara husika na kutengeneza mpango mkakati wa kutatua changamoto mbalimbali. Sasa hapa kwetu mawaziri wanapofika hatua ya kuelewa na kuanza mikakati wanaondolewa na kuletwa wengine ambao na wanahitaji muda kujifunza. Hivyo ndani ya miaka mitano unakuta hakuna la maana lililofanyika.

Pili binadamu wote tunajifunza kutokana na makisa. Mtu aliyekosea ana nafasi nzuri zaidi ya kutenda bora zaidi kwani amekuwa anajifunza. Hivyo si busara kumuondoa mtu pale anapokosea.

Hali hii ndo husababisha watu kutenda na kufanya kazi kwa business as usual. Kwani anaogopa kama akileta ubunifu flani na usipozaa matunda chanya ataondolewa bila kupewa nafasi ya kurekebisha makosa.

Hivyo tutaendelea na mambo yale yale kila siku. Hakuna atakayekuwa tayari ku risk kitumbua chake kwa kujaribu kitu kipya kwa kuogopa kukosea.
 
sem2708

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,304
2,000
Hata mimi nasapoti hiyo operesheni kwani majangiri wamekuwa kero sana na wana roho kama shetani tu

Mimi ukinipa bunduki nikikutana na jangiri namuwasha ya makalio tu kwa sababu nikimuacha ataniua

Si ukamuwashe? Kwani humjui? Mvizie akitoka kikao cha cc mpe za hizo sehemu ulizotaja
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom