Nyalandu alishinda ubunge kwa rushwa - CCM

Nyalandu alishinda ubunge kwa rushwa - CCM

Ifike mahali wana Lumumba muwe mnakaa na kukiri miujiza mnayoifurumusha,
La ajabu anaeongea hayo ni kiongozi,na mijitu ipo kimyaaa
 
Chadema wanapenda sana mambo kama hayo bora ameamua kwenda huko kwao.
 
Mimi sio mwanasiasa na sina chama ila ccm kwa mtindo huu mnajiaibisha sana tena sana
 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Martha Mlata amesema kuwa Lazaro Nyalandu alianza kuwa shida tangu alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri wa viwanda na biashara, aliposhindwa kufanya kazi za ubunge jimboni kwake.

"Kwa hiyo akawa mzigo jimboni kutokana na kutofika na akifika, anasimama jukwaani dakika mbili halafu anashuka huku kukiwa hakuna cha maana alichokiongea. Na hata alipokuwa jimboni, hakuweza kuwatetea wananchi wake na hatimaye akawa bubu kabisa" - Mlata.

Mlata alidai kuwa katika kipindi chote cha ubunge, Nyalandu hakuwahi kushinda kwa kupigiwa kura na wananchi zaidi ya kuhonga wapiga kura na shughuli zote za ubunge zilikuwa zikifanywa na wasaidizi wake watatu na yeye anafika jimboni ikiwa zimebaki siku saba za uchaguzi.

My take:
Nadhani nikisema CCM haina dhamira ya dhati kupambana na rushwa sitakosea. Mlishindwaje kumshtaki Nyalandu kwa kutoa rushwa ili ashinde ubunge, mkasubiri ahame mfanye siasa za utapeli na kutapa tapa?
Huyoo mwenyekitiii hanaa akiliii kwanini siku zotee hakusemagaaa leo ameondokaaa ndio mnanyanyua midomooo
Mimi binafsii Ccm siwaelewegii anzia mzee hadii mtoto maana akili zao zinafanana labdaa hawafikirigiiiii
 
Back
Top Bottom