Nyakarungu
JF-Expert Member
- May 1, 2011
- 472
- 377
Basi Kisha Mtemi WA Wanatta akaendelea.
"Siku Moja nilimvizia yule shujaa WA kijiji akiwa amekaa pembezoni mwa mto nikamsukuma akaangukia Mtoni, Kisha nikapiga filimbi na kelele za kuwatangazia wanakijiji kwamba nimeshindana mieleka na shujaa wenu na hakufua dafu nimemtokomezea Mtoni, kijiji chote kilikusanyika wakinisifu na kutaka kujua uwezo nilio nao.
Alipotoka Mtoni akiwa Amenikazia macho na kutaka turudie shindano lile la mieleka huku akijitetea kwamba hakujua kama wakati napita nyuma yake nilipanga kumsukumia Mtoni, hivyo akawaomba wanakijiji wasimame kando washuhudie marudio ya shindano,
Mimi nilijua nitapigwa kipigo cha paka shume nikakataa katakata, ilibidi wazee WA kijiji waniulize ikiwa wakibatilisha ushindi wangu nitajisikiaje, nikawajibu kwamba sitautambua ushindi wake
Walimtangaza akaendelea kushikilia lile Dume la kondoo kama ishara ya shujaa WA kijiji,
Japo Kwa kakikundi ka Watu waliokuwa Sana chuki nae za kifamilia wakaanza kunipongeza na kuniita shujaa WA Amani ya kijiji niliyekataa kupigana." Kisha nikamuuliza Mtemi Una maana gani mfano huu kwetu na kizazi cha Leo ili hali yalitokea zamani za ujima na ujana wenu?
Akajibu "kutatokea mambo kama hayo na yasiwasumbue hata kizazi chetu yalitokea."
Akamaliza na kikao kikafungwa huku akivuta kiko chake.