Nyaisangah hakutendewa haki hata kidogo

Si vyema kukumbushia habari zao waliolala mauti. Waacheni wafu wazike wafu wao, ndivyo maandiko yanavyosema. Lakini katika hili la Nyaisanga tuna la kujifunza hasa kwa sisi wenye taaluma ya habari..

Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya familia zinadai kuwa wakati Nyaisanga alipokuwa mgonjwa, hakuna hata mwanahabari mmoja aliyekuwa akijali afy
a yake.

Alisumbuliwa na kisukari kwa zaidi ya miaka 20 lakini hakuna aliyejali. Si waajiri wake (ambao Nyaisanga aliwaingizia mamilioni ya fedha kwa umahiri wake wa kazi), si wanahabari wenzie, wala marafiki zake.

Licha ya kusumbuliwa na maradhi muda mrefu na licha ya wenzie kutoonesha support lakini, hakujali, aliendelea na kazi zake.

Wakati Radio One inaanzishwa alikubali kujitoa sadaka na kuacha kazi RTD ili kuhakikisha Radio One inaanzishwa na inasimama imara. Wakati ule na kina Charless Hilary, Mickdady Mahmood, Flora Nducha, Abdalah Majura na wengine.

Mtangazaji mararufu wa BBC, Aboubakar Liongo anadai ni Julius aliyemshawishi kuingia kwenye taaluma ya habari. Ni yeye aliyempeleka Radio One kufanya majaribio yake ya kwanza kama Radio Presenter. Hata baba yake Liongo alipoonesha wasiwasi Nyaisanga ndiye aliyemtoa wasiwasi huo kwa kumhakikishia usalama wa mwanae.

Hata baadae iliporipotiwa amesimamishwa kazi Radio One licha ya kuitumikia kwa takribani miaka 15, hakukata tamaa, aliendelea kupambana. Hatimaye akapata ajira Abood Media Morogoro.

Alipokuwa Morogoro bado aliendelea kusumbuliwa sana na kisukari na pressure. Aliugua, alizidiwa, akalazwa, lakini hakuna aliyekuwa karibu yake zaidi ya familia yake. Si watangazaji wenzie maarufu aliokuwa nao enzi hizo, au waajiri wake aliowatumikia kwa uaminifu.

Hata aliporipotiwa kuzidiwa na kwamba hali yake ilikuwa "serious" hakuna aliyejali. Alihangaika na mkewe na wanae huku akipewa support "kidogo" na Mzee Abood.

Licha kuzidiwa na maradhi lakini alilazwa "zahanati" ya Mazimbu, inayodaiwa kuwa Hospitali. Na bila shaka kutokana na kutopata huduma alizostahili kwa maradhi yake akafariki dunia.

Lakini mi nadhani Nyaisanga alihitaji matibabu bora zaidi ya yale ya Mazimbu. Alihitaji hospitali kubwa zaidi ya ile dispensary inayodaiwa kuwa hospitali pale Mazimbu. Pengine asingefariki ikiwa angepata huduma "standard" kidogo kwenye hospitali ya kueleweka.

Haikuwa lazima apelekwe Muhimbimbi kwenye VIP wodi, kama aliyopo Ufoo Saro. Nyaisanga hakuhitaji wodi yenye TV set, flat screen kama aliyopo Ufoo.. Alihitaji wodi ya kawaida yenye madaktari wataalamu ambao wangeweza kutatua shida yake.

Lakini ndio hivyo uwezo wake haukuruhusu kufika huko. Akaishia Mazimbu. Akaugua, akateseka, akalazwa. Peke yake. Hata wandishi wenzake hawakuandika habari za mwenzao kuugua.

However hata hawakumtembelea japo tu kumjulia hali hata kama walikuwa hawataki kuandika. Nani angemtembelea na wote walikuwa busy na risasi za Ufoo Saro..???

Aliugua, akateseka, akapita katika bonde la uvuli wa mauti. Licha ya kuwa alikuwa peke yake lakini hakuogopa, maaana "gongo na filmbo" yake BWANA vilimfariji.

Hatimaye akafariki usiku wa kuamkia October 20. Na hapo hasa ndipo ulipoonekana USALITI na Unafiki. Kila mtu alijifanya kumfahamu. Kila mtu alijifanya rafiki yake. Hata wale rafiki zake ambao pengine tangu waachane Radio One hawakuwahi hata kumpigia simu wakajifanya kuomboleza.

Viongozi wa serikali nao kama kawaida yao wakajitokeza na kudai wamepokea KWA MSHTUKO MKUBWA kifo cha Nyaisanga. Salamu za rambirambi zikatolewa kuanzia kwa Mh.Rais Kikwete hadi kwa MaDJs wa Radio Mbao. Wakapiga na nyimbo za kumuenzi mwenzao..

Lahaulah..!! Walikuwa wapi siku zote? Heshima zote hizi kwanini hawakumpa Nyaisanga angali hai, hadi wasubiri kuja kuipa maiti heshima?? Au ndo wanafikisha ujumbe kuwa WANAOKUDHARAU SIKU MOJA WATAKUSALIMIA KWA HESHIMA??

Lakini yote tisa, kumi ni vioja vilivyofanywa na waandishi wenzie. Aliokuwa nao RTD, wengine akaenda nao Radio One, wengine BBC, DW, Sauti ya Amerika etc. Watangazaji maarufu, wenye majina makubwa...wengine huwezi kuwaita majina yao kabla hujatanguliza neno "papaa" kwa sababu wana vitambi vikubwa, cha Idd Amin hakioni ndani..!! Wamekuwa mastar wa mjini..!!

Watangazaji hawa mapedeshee, ambao wengi walidai ni marafiki zake waliingia na mbwembwe Morogoro. Wakabadilisha kila kitu walichokikuta. Wakabadili ratiba ya mazishi na kuweka yao. Wakafuta kamati ya mazishi waliyoikuta Moro na kuunda yao..

Harakaharaka wakaweka na ratiba ya mwili wa Nyaisanga kuagwa Dar, tofauti na kamati ya Morogoro ambayo ilidhani kumuaga Morogoro peke yake ingetosha.

Mapedeshee wakasema lazima mwili wa Nyaisanga uletwe Dar. Watawezaje kuonesha mbwembwe zao mwili ukiagwa Moro?? Magari yao ya Vorgue, Discovery, Lexus hayawezi kwenda Moro. Suti zao kali za Dubai na Hong Kong haziwezi kuchafuka vumbi hadi Moro. Nyaisanga aletwe Dar.!

Waliposhauriwa kuwa mwili wa Nyaisanga ukitolewa Moro, upelekwe Dar kisha upelekwe Musoma kwa kupitia Morogoro utaharibika, hivyo ni bora waage kwa pamoja Moro kisha wapeleke mwili Musoma kwa maziko.. Haraka wakajibu "kama hofu ni mwili kuharibika tutakodi ndege, (Private Jet) itakayopeleka mwili hadi Musoma"

Kwa kauli hiyo Mjane wa marehemu hakuwa na pingamizi. Mapedeshee nao kufika Dar wakatangaza kwa haraka kuwa mwili wa Nyaisanga utaagwa Leaders kisha utasafirishwa kwenda Musoma kwa ndege. Kwa waliomfahamu Nyaisanga na alivyoteseka atleast hii ikawapa faraja kidogo.!

Lakini hawakutimiza ahadi hiyo ya kumpeleka kwa ndege zaidi ya kutafuta umaarufu tu pale Leaders. Baada ya kuaga, kila mmoja akadisappear na kuachia familia mzigo wa kusafisha maiti kwa gari hadi Musoma. What a shame..!! Kumbe wakati wanajinadi kupeleka mwili kwa ndege akili zao zilikuwa Mabwepande au??.

Kwa nini basi, waliamua kuuleta mwili Dar? Je, kulikuwa na shinikizo la nani? Au walikuwa wanatafuta umaarufu? Hii ni dharau..

Nani aliwalazimisha waandishi kuleta maiti Dar na kuja kuitelekeza Leaders?? Kama walishindwa kumheshimu Nyaisanga akiwa hai, kwanini hawakuheshimu hata maiti yake?? Enyi Waaandishi na Watangazaji wa Tanzania, nani aliyewaloga??

Pili, kamati hii ya watangazaji na wandishi iliyoleta msiba Dar waliidharau kamati ya mazishi ya Morogoro kwa kubadilisha jeneza na kumweka katika jeneza lingine. Kamati iliyokuwa inaratibu mazishi Morogoro ilimuweka kwenye jeneza alilokuja nalo hadi hospitali ya Muhimbili.

Lakini Kamati ya "Waandishi" wakaenda na jeneza jingine Muhimbili na kumbadilisha Nyaisanga. Mwanakamati mmoja alipohojiwa kuhusu kukataa jeneza la Morogoro alijibu hivi "Lile lililotoka na mwili Morogoro lilionekana kukosa ubora halafu lilitengenezwa ‘chapchap' ndiyo ikaamriwa linunuliwe jingine zuri zaidi." (Risasi, 26,October 2013).

Kwa upande wangu this is illogical statement ever made. Ubora uliokuwa unazungumzwa ni nupi? Jeneza lisilo bora lingewezaje kumleta kutoka Morogoro hadi Dar.?? kama ubora walimaanisha nakshi na marembo, ya kazi gani hayo?? Kwanini hizo hela zisingesaidia mjane na watoto walioachwa badala ya kutafuta sifa za kijinga??

Jeneza la gharama ili iweje? Ili tuone kuwa Nyaisanga alikuwa na maisha ya kifahari kumbe sivyo??

Prof.Lipumba aliwahi kusema Watanzania hatuwezi kuendelea kiuchumi kwa sababu tumeendekeza maisha ya bandia. Hatutaki kuishi maisha yetu halisi.. Hatutaki kujikubali.

Mtu anasoma BAED lakini ukimuuliza atakuambia LLB. Hajikubali, atafanikiwaje?? Mtu analipwa Laki 5 kwa mwezi lakini anataka kudrive after two months. Hajikubali.. hataki kukubali kuwa hali yake ni duni na anatakiwa kustrive ili kufanikiwa.

Sasa Nyaisanga amekufa bila msaada wa maana kutoka kwa waandishi wenzie, leo mnamnunulia jeneza la Milioni na ushee, upuuzi..!!

Lakini kama kweli kamati hii ya waandishi walikuwa na uchungu na Julius na hawakutaka awekwe kwenye jeneza cheap, kwanini hawakuungana na kamati ya mazishi ya Morogoro na kuangalia upungufu uliopo na kuurekebisha. Bila shaka wangeweza kuwashauri wenzao wa Morogoro aina ya jeneza la kununua ili wasipoteze hela mara mbilimbili.

Lakini maziko ya Wakristo hufanywa na jeneza moja tu. Jeneza linalotumika kubebea mwili wa marehemu ndilo hilohilo huingizwa kaburini na marehemu akiwemo ndani, tofauti na Waislamu ambao jeneza hurudi msikitini.

Sasa jeneza la Nyaisanga lililokataliwa na Kamati ya Dar litaenda wapi? Mwanakamati mmoja alipoulizwa alijibu kwa kujiamini "Lile tuliliacha Muhimbili ,ndugu watajua cha kufanyia" (Risasi 26, October 2013).

Kwangu mimi hii ni kauli ya dharau. Ndugu watajua cha kufanyia?? What does it mean? Kwamba ndugu walipeleke jeneza nyumbani kujiandaa na msiba mwingine au?

Mi nadhani kamati iliyoundwa Moro ingeachwa ifanye kazi yake bila kuingiliwa kila kitu kingekamilika. Hii kamati iliyoundwa Dar ilikuwa ya kisiasa au kutaka umaarufu. kila mtu anajidai kuwa ndugu, rafiki na wa kumuonea huruma. Mlikuwa wapi Nyaisanga alipokuwa mgonjwa?

Lakini hii si mara ya kwanza mambo haya kutokea kwenye tasnia ya habari nchini. Wapo waandishi wameugua muda mrefu, wameteseka na wengine wamekufa vifo vya mateso, lakini ni nadra kusikia wandishi wenzake wakiripoti habari hizo.

Adam Mwaibabile alifungwa bila hatia, hakuna mwandishi aliyekuwa na habari nae. Hata aliposhinda kesi baada ya kukaa gerezani mwaka mmoja, waandishi wenzie hawakuona ile ni story. Walikuwa busy na story za wanasiasa maana ndio zinamake "headlines"

Hata Mwaibabile alipotoka gerezani na kuandika kitabu chake kuelezea aliyokutana nayo huko jela na namna alivyofungwa kwa uionevu wa RC wa Lindi, hakuna Mwandishi aliyempa suport hata ya kukipa promo kitabu chake.

Hakuna hata gazeti lililodiriki kumpa free space atangaze kitabu chake. Alikuwa akihangaika mwenyewe kama tiara kutafuta market ya kitabu chake.

Hakuna mwandishi aliyemfanyia interview.. Hakuna mwandishi aliyekuwa na muda nae..

Kwani yeye amepigwa risasi na jamaa kutoka Sudan?? kwani yeye amemwagiwa tindikali? Kwani yeye alinyofolewa jicho na kupelekwa S.Africa??

However hata wangedeal nae Mwaibabile hakuwa na 10% ya kuwapa kama waliyozoea kupewa na Wanasiasa kwenye bahasha za khaki..

Wenyewe wanasema si rushwa, bali ni posho tu inaitwa "brown envelop" Huwa wanapewa wakiripoti habari za Vyama vimegoma kukaguliwa fedha za ruzuku, au wakiripoti Mabilioni yaliyofichwa Uswisi..!

Hata hivyo licha ya kuteseka kote huko Mwaibabile akaja kufariki kifo chenye utata na ilidaiwa ameuawa lakini kwa waandishi wenzie ile haikuwa habari kubwa kama ya kukamatwa kwa "Masamaki ya Magufuli"

Waandishi hawakuthamini maisha ya mwenzao kisa Vibua na Pereje za Magufuli ndio ilikuwa "habari ya mjini".

Hadi leo hakuna mwandishi aliyewahi kudevelop story au makala kujaribu kureflect maisha ya Mwaibabile na kifo chake cha utata...

MY TAKE..!!
Waandishi hatuthaminiani.. Hatujaliani.. Hatupendani.. Tumebaki kuchumia matumbo na kutafuta umaarufu wa kijinga mjini. Tupo busy kuripoti habari za wanasiasa na kupiga ramli za kutabiri wagombea urais 2015.

Ifike mahali tujijali na kujipenda. Tujithamini..Tuache uzandiki huu wa kuithamani maiti na kutomjali mtu wakati akiwa anaumwa.

Tusipojijali sisi hata hao wanasiasa tunaowatetemekea hawawezi kututhamini. wataendelea tu kututumia kama "BIG G" ambayo utamu ukiisha hutupwa, hata aliyekuwa anaitafuna asijue alipoitupa.

MSIBA HUU WA NYAISANGA UWE FUNDISHO KWA WANAHABARI WOTE WA TANZANIA.. (mimi nikiwemo). Tutengeneze image itakayotufanya tukumbukwe hata tutakapoondoka hapa duniani.

Mwanaharakati Che Guevara aliwahi kusema "Im not afraid of death. Because i know when my Heart will beat no more, I wont die. I will continue living in the heart of other people for the Principles, Rules and Beliefs that I lived for..."

Chanzo
Maisha Times: INASIKITISHA: Julius Nyaisanga alisalitiwa na wenzie!

Ni kweli kabisa, I 100% support your observations!!! RIP Uncle J, sisi sote njia yetu ni hiyo hiyo.....
 
Tatizo sio waandishi wa habari, tatizo usanii ndo tabia ya watanzania wengi. Tumesikia na kuona pia juzjuzi vituko vya watumishi wa mungu kwe msiba wa askofu kulola. Hii hatari sana kwa ustawi wa jamii yetu kama watanzania.
 
wanahabari wamepakatwa na wanasiasa na mapedeshee so hawawezi kuthaminiana wao kwa wao
 
Bwana pascal mayalla, mimi naongea kutoka jikoni niko hapa DW huyo jamaa alifukuzwa alishindwa kazi alikuwa mzigo alitegemea kuishi kwa majungu majungu.....na hiyo picha nadhani ni adobe tu hiyo
Rihana, naomba tusaidiane kwenye hili!, DW trial ni miezi 6, ukishindwa unarudishwa!. Abou kakaa hapo miaka 4!, mktaba ukaisha akarudi home!. Aliyempokea ni Grace Kabogo, grace alipokuja likizo Tanzania, ni Abou aliitwa tena kumshikia kwa mwezi mmoja!, mtu aliyeshindwa kazi angevumiliwaje miaka 4?. Mtu aliyefukuzwa kazi, angeitwaje kumshikia mtu?!. Picha ya photoshop for what?!.
For Godness sake, tumwache Uncle Apumzike kwa amani!. Please!.
Pasco.
 
lakini hili la kusafirishwa na gari kutoka Dar hadi musoma ni la kweli ama kuna kuongezea chumvi??
 
Sijui ni wakina nani walikuwa wanakamati ya mazishi hiyo ya pili iliyoharibu? RIP Uncle J

Hivi kwa nn wabongo tunapenda sana unafiki????kumtaja mtu jina huwa inakua issue...mwenyekiti wa kamati ya mazishi alikua Aboubakar Liongo na mmoja wa wanakamati alikua Misanya Bingi na nafikiri Teddy Mapunda.watu huko bongo wanawajua wote kwa majina sema unafiki mwingi.kwenye blog ya michuzi alionekana Abouu akimkaribisha Mzee Mengi Leaders akiwa kama mwenyekiti wa kamati ya mazishi.
source: michuzi blog
 
Rihana, naomba tusaidiane kwenye hili!, DW trial ni miezi 6, ukishindwa unarudishwa!. Abou kakaa hapo miaka 4!, mktaba ukaisha akarudi home!. Aliyempokea ni Grace Kabogo, grace alipokuja likizo Tanzania, ni Abou aliitwa tena kumshikia kwa mwezi mmoja!, mtu aliyeshindwa kazi angevumiliwaje miaka 4?. Mtu aliyefukuzwa kazi, angeitwaje kumshikia mtu?!. Picha ya photoshop for what?!.
For Godness sake, tumwache Uncle Apumzike kwa amani!. Please!.
Pasco.[/QUOT
Pasco, achana kubishana na huyu jamaa,yeye anafikiri ajira za ughaibuni ni za ujanja ujanja kama bongo...mtu kama Abouu sio wa kufukuzwa kazi baada ya kufanya DW kwa miaka 4....swali dogo tu hivi hapo bongo kwa sasa ni mtangazaji gani anaweza kusimama na Aboubakar Liongo??/yamejaa makanjanja kibao ...anyway sio kosa lake kwani wabongo hawako serious na kitu chochote wanapenda uzushi kama huu.
 
Si vyema kukumbushia habari zao waliolala mauti. Waacheni wafu wazike wafu wao, ndivyo maandiko yanavyosema. Lakini katika hili la Nyaisanga tuna la kujifunza hasa kwa sisi wenye taaluma ya habari..

Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya familia zinadai kuwa wakati Nyaisanga alipokuwa mgonjwa, hakuna hata mwanahabari mmoja aliyekuwa akijali afy
a yake.

Alisumbuliwa na kisukari kwa zaidi ya miaka 20 lakini hakuna aliyejali. Si waajiri wake (ambao Nyaisanga aliwaingizia mamilioni ya fedha kwa umahiri wake wa kazi), si wanahabari wenzie, wala marafiki zake.

Licha ya kusumbuliwa na maradhi muda mrefu na licha ya wenzie kutoonesha support lakini, hakujali, aliendelea na kazi zake.

Wakati Radio One inaanzishwa alikubali kujitoa sadaka na kuacha kazi RTD ili kuhakikisha Radio One inaanzishwa na inasimama imara. Wakati ule na kina Charless Hilary, Mickdady Mahmood, Flora Nducha, Abdalah Majura na wengine.

Mtangazaji mararufu wa BBC, Aboubakar Liongo anadai ni Julius aliyemshawishi kuingia kwenye taaluma ya habari. Ni yeye aliyempeleka Radio One kufanya majaribio yake ya kwanza kama Radio Presenter. Hata baba yake Liongo alipoonesha wasiwasi Nyaisanga ndiye aliyemtoa wasiwasi huo kwa kumhakikishia usalama wa mwanae.

Hata baadae iliporipotiwa amesimamishwa kazi Radio One licha ya kuitumikia kwa takribani miaka 15, hakukata tamaa, aliendelea kupambana. Hatimaye akapata ajira Abood Media Morogoro.

Alipokuwa Morogoro bado aliendelea kusumbuliwa sana na kisukari na pressure. Aliugua, alizidiwa, akalazwa, lakini hakuna aliyekuwa karibu yake zaidi ya familia yake. Si watangazaji wenzie maarufu aliokuwa nao enzi hizo, au waajiri wake aliowatumikia kwa uaminifu.

Hata aliporipotiwa kuzidiwa na kwamba hali yake ilikuwa "serious" hakuna aliyejali. Alihangaika na mkewe na wanae huku akipewa support "kidogo" na Mzee Abood.

Licha kuzidiwa na maradhi lakini alilazwa "zahanati" ya Mazimbu, inayodaiwa kuwa Hospitali. Na bila shaka kutokana na kutopata huduma alizostahili kwa maradhi yake akafariki dunia.

Lakini mi nadhani Nyaisanga alihitaji matibabu bora zaidi ya yale ya Mazimbu. Alihitaji hospitali kubwa zaidi ya ile dispensary inayodaiwa kuwa hospitali pale Mazimbu. Pengine asingefariki ikiwa angepata huduma "standard" kidogo kwenye hospitali ya kueleweka.

Haikuwa lazima apelekwe Muhimbimbi kwenye VIP wodi, kama aliyopo Ufoo Saro. Nyaisanga hakuhitaji wodi yenye TV set, flat screen kama aliyopo Ufoo.. Alihitaji wodi ya kawaida yenye madaktari wataalamu ambao wangeweza kutatua shida yake.

Lakini ndio hivyo uwezo wake haukuruhusu kufika huko. Akaishia Mazimbu. Akaugua, akateseka, akalazwa. Peke yake. Hata wandishi wenzake hawakuandika habari za mwenzao kuugua.

However hata hawakumtembelea japo tu kumjulia hali hata kama walikuwa hawataki kuandika. Nani angemtembelea na wote walikuwa busy na risasi za Ufoo Saro..???

Aliugua, akateseka, akapita katika bonde la uvuli wa mauti. Licha ya kuwa alikuwa peke yake lakini hakuogopa, maaana "gongo na filmbo" yake BWANA vilimfariji.

Hatimaye akafariki usiku wa kuamkia October 20. Na hapo hasa ndipo ulipoonekana USALITI na Unafiki. Kila mtu alijifanya kumfahamu. Kila mtu alijifanya rafiki yake. Hata wale rafiki zake ambao pengine tangu waachane Radio One hawakuwahi hata kumpigia simu wakajifanya kuomboleza.

Viongozi wa serikali nao kama kawaida yao wakajitokeza na kudai wamepokea KWA MSHTUKO MKUBWA kifo cha Nyaisanga. Salamu za rambirambi zikatolewa kuanzia kwa Mh.Rais Kikwete hadi kwa MaDJs wa Radio Mbao. Wakapiga na nyimbo za kumuenzi mwenzao..

Lahaulah..!! Walikuwa wapi siku zote? Heshima zote hizi kwanini hawakumpa Nyaisanga angali hai, hadi wasubiri kuja kuipa maiti heshima?? Au ndo wanafikisha ujumbe kuwa WANAOKUDHARAU SIKU MOJA WATAKUSALIMIA KWA HESHIMA??

Lakini yote tisa, kumi ni vioja vilivyofanywa na waandishi wenzie. Aliokuwa nao RTD, wengine akaenda nao Radio One, wengine BBC, DW, Sauti ya Amerika etc. Watangazaji maarufu, wenye majina makubwa...wengine huwezi kuwaita majina yao kabla hujatanguliza neno "papaa" kwa sababu wana vitambi vikubwa, cha Idd Amin hakioni ndani..!! Wamekuwa mastar wa mjini..!!

Watangazaji hawa mapedeshee, ambao wengi walidai ni marafiki zake waliingia na mbwembwe Morogoro. Wakabadilisha kila kitu walichokikuta. Wakabadili ratiba ya mazishi na kuweka yao. Wakafuta kamati ya mazishi waliyoikuta Moro na kuunda yao..

Harakaharaka wakaweka na ratiba ya mwili wa Nyaisanga kuagwa Dar, tofauti na kamati ya Morogoro ambayo ilidhani kumuaga Morogoro peke yake ingetosha.

Mapedeshee wakasema lazima mwili wa Nyaisanga uletwe Dar. Watawezaje kuonesha mbwembwe zao mwili ukiagwa Moro?? Magari yao ya Vorgue, Discovery, Lexus hayawezi kwenda Moro. Suti zao kali za Dubai na Hong Kong haziwezi kuchafuka vumbi hadi Moro. Nyaisanga aletwe Dar.!

Waliposhauriwa kuwa mwili wa Nyaisanga ukitolewa Moro, upelekwe Dar kisha upelekwe Musoma kwa kupitia Morogoro utaharibika, hivyo ni bora waage kwa pamoja Moro kisha wapeleke mwili Musoma kwa maziko.. Haraka wakajibu "kama hofu ni mwili kuharibika tutakodi ndege, (Private Jet) itakayopeleka mwili hadi Musoma"

Kwa kauli hiyo Mjane wa marehemu hakuwa na pingamizi. Mapedeshee nao kufika Dar wakatangaza kwa haraka kuwa mwili wa Nyaisanga utaagwa Leaders kisha utasafirishwa kwenda Musoma kwa ndege. Kwa waliomfahamu Nyaisanga na alivyoteseka atleast hii ikawapa faraja kidogo.!

Lakini hawakutimiza ahadi hiyo ya kumpeleka kwa ndege zaidi ya kutafuta umaarufu tu pale Leaders. Baada ya kuaga, kila mmoja akadisappear na kuachia familia mzigo wa kusafisha maiti kwa gari hadi Musoma. What a shame..!! Kumbe wakati wanajinadi kupeleka mwili kwa ndege akili zao zilikuwa Mabwepande au??.

Kwa nini basi, waliamua kuuleta mwili Dar? Je, kulikuwa na shinikizo la nani? Au walikuwa wanatafuta umaarufu? Hii ni dharau..

Nani aliwalazimisha waandishi kuleta maiti Dar na kuja kuitelekeza Leaders?? Kama walishindwa kumheshimu Nyaisanga akiwa hai, kwanini hawakuheshimu hata maiti yake?? Enyi Waaandishi na Watangazaji wa Tanzania, nani aliyewaloga??

Pili, kamati hii ya watangazaji na wandishi iliyoleta msiba Dar waliidharau kamati ya mazishi ya Morogoro kwa kubadilisha jeneza na kumweka katika jeneza lingine. Kamati iliyokuwa inaratibu mazishi Morogoro ilimuweka kwenye jeneza alilokuja nalo hadi hospitali ya Muhimbili.

Lakini Kamati ya "Waandishi" wakaenda na jeneza jingine Muhimbili na kumbadilisha Nyaisanga. Mwanakamati mmoja alipohojiwa kuhusu kukataa jeneza la Morogoro alijibu hivi "Lile lililotoka na mwili Morogoro lilionekana kukosa ubora halafu lilitengenezwa ‘chapchap' ndiyo ikaamriwa linunuliwe jingine zuri zaidi." (Risasi, 26,October 2013).

Kwa upande wangu this is illogical statement ever made. Ubora uliokuwa unazungumzwa ni nupi? Jeneza lisilo bora lingewezaje kumleta kutoka Morogoro hadi Dar.?? kama ubora walimaanisha nakshi na marembo, ya kazi gani hayo?? Kwanini hizo hela zisingesaidia mjane na watoto walioachwa badala ya kutafuta sifa za kijinga??

Jeneza la gharama ili iweje? Ili tuone kuwa Nyaisanga alikuwa na maisha ya kifahari kumbe sivyo??

Prof.Lipumba aliwahi kusema Watanzania hatuwezi kuendelea kiuchumi kwa sababu tumeendekeza maisha ya bandia. Hatutaki kuishi maisha yetu halisi.. Hatutaki kujikubali.

Mtu anasoma BAED lakini ukimuuliza atakuambia LLB. Hajikubali, atafanikiwaje?? Mtu analipwa Laki 5 kwa mwezi lakini anataka kudrive after two months. Hajikubali.. hataki kukubali kuwa hali yake ni duni na anatakiwa kustrive ili kufanikiwa.

Sasa Nyaisanga amekufa bila msaada wa maana kutoka kwa waandishi wenzie, leo mnamnunulia jeneza la Milioni na ushee, upuuzi..!!

Lakini kama kweli kamati hii ya waandishi walikuwa na uchungu na Julius na hawakutaka awekwe kwenye jeneza cheap, kwanini hawakuungana na kamati ya mazishi ya Morogoro na kuangalia upungufu uliopo na kuurekebisha. Bila shaka wangeweza kuwashauri wenzao wa Morogoro aina ya jeneza la kununua ili wasipoteze hela mara mbilimbili.

Lakini maziko ya Wakristo hufanywa na jeneza moja tu. Jeneza linalotumika kubebea mwili wa marehemu ndilo hilohilo huingizwa kaburini na marehemu akiwemo ndani, tofauti na Waislamu ambao jeneza hurudi msikitini.

Sasa jeneza la Nyaisanga lililokataliwa na Kamati ya Dar litaenda wapi? Mwanakamati mmoja alipoulizwa alijibu kwa kujiamini "Lile tuliliacha Muhimbili ,ndugu watajua cha kufanyia" (Risasi 26, October 2013).

Kwangu mimi hii ni kauli ya dharau. Ndugu watajua cha kufanyia?? What does it mean? Kwamba ndugu walipeleke jeneza nyumbani kujiandaa na msiba mwingine au?

Mi nadhani kamati iliyoundwa Moro ingeachwa ifanye kazi yake bila kuingiliwa kila kitu kingekamilika. Hii kamati iliyoundwa Dar ilikuwa ya kisiasa au kutaka umaarufu. kila mtu anajidai kuwa ndugu, rafiki na wa kumuonea huruma. Mlikuwa wapi Nyaisanga alipokuwa mgonjwa?

Lakini hii si mara ya kwanza mambo haya kutokea kwenye tasnia ya habari nchini. Wapo waandishi wameugua muda mrefu, wameteseka na wengine wamekufa vifo vya mateso, lakini ni nadra kusikia wandishi wenzake wakiripoti habari hizo.

Adam Mwaibabile alifungwa bila hatia, hakuna mwandishi aliyekuwa na habari nae. Hata aliposhinda kesi baada ya kukaa gerezani mwaka mmoja, waandishi wenzie hawakuona ile ni story. Walikuwa busy na story za wanasiasa maana ndio zinamake "headlines"

Hata Mwaibabile alipotoka gerezani na kuandika kitabu chake kuelezea aliyokutana nayo huko jela na namna alivyofungwa kwa uionevu wa RC wa Lindi, hakuna Mwandishi aliyempa suport hata ya kukipa promo kitabu chake.

Hakuna hata gazeti lililodiriki kumpa free space atangaze kitabu chake. Alikuwa akihangaika mwenyewe kama tiara kutafuta market ya kitabu chake.

Hakuna mwandishi aliyemfanyia interview.. Hakuna mwandishi aliyekuwa na muda nae..

Kwani yeye amepigwa risasi na jamaa kutoka Sudan?? kwani yeye amemwagiwa tindikali? Kwani yeye alinyofolewa jicho na kupelekwa S.Africa??

However hata wangedeal nae Mwaibabile hakuwa na 10% ya kuwapa kama waliyozoea kupewa na Wanasiasa kwenye bahasha za khaki..

Wenyewe wanasema si rushwa, bali ni posho tu inaitwa "brown envelop" Huwa wanapewa wakiripoti habari za Vyama vimegoma kukaguliwa fedha za ruzuku, au wakiripoti Mabilioni yaliyofichwa Uswisi..!

Hata hivyo licha ya kuteseka kote huko Mwaibabile akaja kufariki kifo chenye utata na ilidaiwa ameuawa lakini kwa waandishi wenzie ile haikuwa habari kubwa kama ya kukamatwa kwa "Masamaki ya Magufuli"

Waandishi hawakuthamini maisha ya mwenzao kisa Vibua na Pereje za Magufuli ndio ilikuwa "habari ya mjini".

Hadi leo hakuna mwandishi aliyewahi kudevelop story au makala kujaribu kureflect maisha ya Mwaibabile na kifo chake cha utata...

MY TAKE..!!
Waandishi hatuthaminiani.. Hatujaliani.. Hatupendani.. Tumebaki kuchumia matumbo na kutafuta umaarufu wa kijinga mjini. Tupo busy kuripoti habari za wanasiasa na kupiga ramli za kutabiri wagombea urais 2015.

Ifike mahali tujijali na kujipenda. Tujithamini..Tuache uzandiki huu wa kuithamani maiti na kutomjali mtu wakati akiwa anaumwa.

Tusipojijali sisi hata hao wanasiasa tunaowatetemekea hawawezi kututhamini. wataendelea tu kututumia kama "BIG G" ambayo utamu ukiisha hutupwa, hata aliyekuwa anaitafuna asijue alipoitupa.

MSIBA HUU WA NYAISANGA UWE FUNDISHO KWA WANAHABARI WOTE WA TANZANIA.. (mimi nikiwemo). Tutengeneze image itakayotufanya tukumbukwe hata tutakapoondoka hapa duniani.

Mwanaharakati Che Guevara aliwahi kusema "Im not afraid of death. Because i know when my Heart will beat no more, I wont die. I will continue living in the heart of other people for the Principles, Rules and Beliefs that I lived for..."

Chanzo
Maisha Times: INASIKITISHA: Julius Nyaisanga alisalitiwa na wenzie!

Hii habari imenisikitisha sana ,kweli marehemu Uncle J. hakutendewa haki .Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya Uncle J.Ili haki itendeke, vipi anayeshinda kesi kortini? Ila hilo la Mwaibabile limeandikwa sana na limetumika kwenye case kadhaa kama reference

Francis Chirwa

Toleo la 110
2 Dec 2009

KWAMBA haki za binadamu kwa binadamu huanzia tumboni mwa mama yake ni ujumbe ambao ulizama vyema vichwani mwa wahariri waliohudhuria warsha iliyofanyika wiki iliyopita mjini Dar es Salaam.
Mimba ikishatungwa, mtoto aliyeko tumboni huwa na haki ya kuishi ndiyo maana mama mzazi anapoitoa mimba bila ya sababu za msingi, Jamhuri inamfungulia shitaka. Japo ni mimba yake mwenyewe, Jamhuri haikuwapo wakati mwenyewe anaipata mimba hiyo kwa raha zake mwenyewe akiridhia.
Lakini kuujua ukweli huo ni jambo moja na utekelezaji wa ukweli huo ni jambo jingine. Ukweli ni kwamba kazi ya uandishi wa habari kimsingi ni kuhusu haki za biandamu. Waandishi wanaporipoti au kupiga picha maonevu yanayofanyika sehemu mbali mbali ya jamii, wanaripoti kuhusu kunyimwa kwa haki za msingi za wanaoonewa. Hivyo wanaporipoti mama aliyemtupa mtoto chooni baada ya kumzaa, wanafanya kazi hiyo hiyo ya kulidna haki za binadamu.
Hata wanaporipoti kuhusu ufujaji wa mali ya umma, wanawapigania jamii ambayo mali hizo zingewafaa kwa maendeleo yao kama ujenzi wa miundombinu, huduma za afya na mambo mengine mengi ya maslahi yao.
Hivi sasa kuna mjadala kuhusu hukumu ya kifo kama katika sheria za Tanzania ifutwe au iendelee kuwapo. Kila mmoja anasema lake na kila upande una sababu nzito ya kueleza kama adhabu hiyo ibaki kama ilivyo au la.
Si nia ya makala hii kujikita katika suala hilo. Lakini kuna suala moja ambalo linahitaji kutiliwa maanani tunapojadili suala zima la haki za binadamu. Suala hilo ni la fidia kwa ‘mkosaji' ambaye baadaye inathibitishwa kwamba hakuwa na kosa hata kidogo.
Inakuwaje kwa ‘mwizi,' ‘mbakaji,' ‘fisadi' au ‘mzinzi' ambaye ametumikia adhabu anapothibitishwa baadaye kwamba alionewa na tuhuma hizo? Anaachwa tu? Anaambiwa pole? Anaombwa radhi? Au jamii inajifanya suala lake halina umuhimu wowote?
Huyu ni mtu ambaye ametoka gerezani kwa kosa ambalo hakulifanya. Amepoteza wakati wake mwingi bure, amekosa kuihudumia familia yake na matokeo yake familia yake ilikwenda mrama. Alitoka gerezani na kujikuta amekimbiwa na mume au mke, mtoto au watoto wake wa kiume wamekuwa wezi, mtoto wa watoto wake wa kike wamezalishwa ovyo kwa sababu ya kujitafutia vijisenti baada ya kushindwa kusoma.
Mtu huyo anafidiwa vipi? Huyu ni mtu ambaye haki zake za binadamu zimekiukwa kwa kiasi kikubwa kuanzia pale aliposota rumanda baada ya kukamatwa, hadi mateso ya gerezani akitumikia kifungo.
Angalau huyo mtu aliyetumikia kifungo sasa tunaweza tukazungumzia suala la kulipwa fidia. Je, yule aliyehukumiwa kunyongwa na adhabu ikatekelezwa?
Itakapodhihirika kwamba ilikuwa ni ‘mistaken identity' (alikamatwa akidhaniwa ndiye kumbe siye), mnamfanya nini? Yule ambaye alikuwa sehemu mbaya kwa wakati mbaya kiasi cha na yeye kukumbwa' na balaa la mauaji atarudishiwa uhai baada ya kunnyongwa? Jibu ni kwamba hawezi kurudishiwa uhai hivyo, haki yake ya kuishi itakuwa imeondolewa kwake bila sababu.
Katika warsha hiyo ya wahariri iliyoandaliwa na Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora, Profesa Luitfried Mbunda wa Chuo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (zamani Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam), alizungumzia kesi ya Jamhuri dhidi ya Adam Mwaibabile ya mwaka 1996 kwamba ni mfano wa mojawapo wa kusikitisha wa ukiukwaji wa haki za binadamu ambao haukufidiwa.
Mwaibabile ambaye sasa ni marehemu Januari 7, 1996 alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kupatikana na nyaraka za siri za Serikali na kufikishwa mbele ya Mahakama ya Wilaya ya Songea.
Profesa Mbunda alisema kwamba Mwaibabile akiwa mwandishi wa habari wa kujitegemea na mfanyabiasha alikumbwa na balaa kutokana na kutoelewana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Nicodemus Banduka kwa sababu ya habari alizokuwa akiziandika kuhusu mkoa huo.
Inaelezwa kwamba Banduka alimwandikia barua Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea kutaka amnyime leseni ya biashara kwa mwaka wa fedha wa 1995/96 kwa vile alimwona ni ‘mchimvi mno' kwa hiyo mtu asiyefaa.
Kwa kufanya hivyo, mkuu huyo wa mkoa alikuwa anamnyima Mwaibabile haki yake ya kufanya biashara kupata kipato cha ziada kwa ajili yake na familia yake. Mwaibabile alipopata ‘kimemo' chenye kumkataza asifanye biashara na ‘kumwaga mtama huo kwenye kuku wengi' (kwa kuripoti), mkuu huyo alikasirika. Alifunguliwa shitaka la kupatikana na ‘nyaraka za siri za Serikali.'
Ingawa katika kesi hiyo nyaraka zenyewe za siri hazikuwasilishwa mahakamani kama ushahidi, Mwaibabile alipatikana na hatia na kufungwa jela mwaka mmoja.
"Vyombo vyua habari viliporipoti kesi hiyo kwa kina, tasnia ya sheria nchini ilishikwa na simanzi jinsi hakimu wa wilaya ambaye ni mwanasheria aliyefuzu taaluma yake alivyoishughulikia kesi hiyo. Hivyo hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa taifa na jumuiya ya kimataifa," alisema Profesa Mbunda katika mada yake.
"Wale waliolaani na kushutumu hukumu hiyo wakiongozwa na vyombo vya habari ni Chama cha Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari (AJM), Chama cha Waaandishi wa Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN) na Mwenyekiti wa chama upinzani cha siasa cha UDP, Mheshimiwa John Cheyo pamoja na makundi ya wanaharakati ya Tanzania na kimataifa," alisema Profesa Mbunda.
Kufuatia juhudi hizo, Machi 20, 1977, Mwaibabile alipewa dhamana na Mahakama Kuu wakati akisubiri kusikilizwa kwa rufani yake. "Jaji aliyesikiliza, Jaji Dan Mapigano (mstaafu) alisema ya kuwa alikuwa anatoa dhamana bila ya masharti yoyote kwa sababu rufani hiyo ilikuwa na nafasi kubwa ya kushinda," alisema Profesa Mbunda.
Na kweli, Aprili 29, 1977, mahakama hiyo hiyo ilifuta hukumu iliuyokuwa imetolewa na Mahakama ya Wilaya na kumwachia huru Mwaibabile. Mwaibabile alikuwa huru tena baada ya kukaa gerezani kwa siku mbili tu badala ya mwaka mzima.
Bahati hiyo ya mtende inawapata wachache sana katika dunia yetu. Kimemo cha mkuu wa mkoa kilitafsiriwa kuwa ni nyaraka nyeti ya Serikali. Kama si kelele nyingi zilizopigwa, Mwaibabile angesota jela mwaka mzima bila sababu yoyote.
Ni dhahiri asingefidiwa na familia yake ingekuwa taabani kwa mwaka mmoja, kisa? Kimemo. Huu basi ni wakati wa kuzungumzia fidia kwa wale wanaosota na na kufungwa kwa kupatikana na hatia kwa tuhuma za kufinyangwa.
Lakini katika hilo basi, mfumo wa sheria unapaswa kukaza buti kuhakikisha kwamba watuhumiwa wanashitakiwa kwa mashitaka halisi na si ya kukomoana. Ashitakiwe mtu kwa kuua kama kweli aliua na si kwa vile alikuwa sehemu ya mchakato uliosababisha mauaji. Kama alishiriki mchakato wa mauaji basi ashitakiwe kwa hilo pia asiachiwe atambe wakati ana mkono wake katika mauaji husika.
Hiyo ni changamoto kubwa kwa medani ya sheria na hasa kwa wanasheria. Si vibaya basi tukawa na mfumo wa kuwa na waendesha mashitaka huru ambao bila shaka watakuwa makini mno na kazi zao.
Chini ya mfumo uliopo, Polisi wana mambo mengi ya kufanya ndiyo maana katika kesi nyingine wanaonekana wanalipua katika kutimiza wajibu wao. Wakati mwignine wanakuwa kwenye njia panda wanapotakiwa kumshughulikia mwenzao.
Ni wao wenyewe polisi wanaotakiwa kukamata, kumpeleka mwenzao mahakamani na kujenga hoja ili apatikane na hatia ilhali ni jana tu walikuwa pamoja kwenye mesi yao.

- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/ili-haki-itendeke-vipi-anayeshinda-kesi-kortini#sthash.Q24bbIpp.dpuf
 
Daah Mungu atusaidie jamani, binadamu tuwe na utu na sio kuweka interest zetu mbele hata kwenye issue za misiba. Pumzika kwa amani uncle Jj

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Labda kije kizazi kingine kabisa cha waandishi si hawa tuwaonao leo! Hawajitambui!
 
Mbona hiyo ni kawaida tu kwa wabongo! Watajitolea kwa hali na mali kuhudumia mazishi yako na si vinginevyo.
 
Poleni sana wote mlioguswa na kupatwa na machungu ya msiba huu kisha kutendwa mlivyotendwa na Waandishi Waliotaka kujipatia umaarufu kwa Msiba wa Julius Nyaisangah kuletwa Leaders Club.
 
Ndiyo maana kuna mambo ya ajabu kwenye tasnia ya habari....! Halafu utawasikia wakisema tunataka...na sisi tutambulike...kama mwimili mwingine wa dola...! Shame on you who are sabotaging Journalism.
 
Back
Top Bottom