Nyaisangah hakutendewa haki hata kidogo

Nyaisangah hakutendewa haki hata kidogo

Ni kweli kabisa Mkuu. Famila inatakiwa ijengwe katika misingi imara ili hata siku ukiwa haupo haitayumbishwakuanzia kwenye msiba mpaka maisha baada ya mazishi.

Ni changamoto inayowezekana mkuu tukikubali kuwa hapa tunapita basi tuandae good grounds kwa watakaobaki!!!!!
 
Hivi umefiwa wewe wanakuja marafiki wa marehemu ndugu yako na kukuambia tunaomba sijui tupeleke mwili sabasaba sijui heshima.imefanyaje na unakubali????!!!!!! THIS SIGNIFIES NOTHING BUT A WEAK FAMILY!!!!!!!

TUKIWA HAI TUJENGE FAMILIA ZETU JAMANI

Kuna watu wanapenda misiba we acha tu, ndo humo wanamo pigia mihela kwa kula cha juu
 
Mkuu napingana na ww hapo kua marafiki hawakumsaidia uncle J kwenda nje...hivi kweli uncle J kwa umahiri wa utangazaji na miaka yote aliofanya RTD na radio one alikua ni mtu wa kusaidiwa kweli???au ilitakiwa yy tu afanye juhudi binafsi kufika huko kama walivyofanya wenzake akina mzee wa macharanga...tufike pahali watu wakubali kuwa responsible na maisha yao sio kurusha lawama za kijinga kwa marafiki wakati muda na nafasi vilikuwepo...lazima tukubali kuwa ukipanda bange tegemea kuvuna bange na sio mahindi...nawakilisha!!

Unakusudia Nyaisana alipanda bange? Lakini mbona umejibu hoja moja tu yakwenda nje? Tunangoja ya kubadili Jeneza ahadi yakutoa ndege na kutosadiwa wakat wa ugonjwa
 
Unakusudia Nyaisana alipanda bange? Lakini mbona umejibu hoja moja tu yakwenda nje? Tunangoja ya kubadili Jeneza ahadi yakutoa ndege na kutosadiwa wakat wa ugonjwa


Mkuu ya kubadili jeneza hilo kwa kweli naweza sema hata mm cjalielewa ilikuwaje..but uncle J alishaenda Deutche Welle kujaribu bahati yake sasa sijui ilikuwaje huko akashindwa..kingine sio kila mtu anapenda kuishi ughaibuni kuna wengine wanapenda maisha ya bongo ya uvivu uvivu, pombe na
wanawake kwa sana.
 
mwacheni kumjadili ameshakufa na tayari kazikwa, mlikuwa na nafasi nzuri kuelezea haya wakati mwili ukiwa MOROGORO au DAR, kwann msubiri azikwe, wewe kipi ulichokifanya kwenye huo msiba? familiya imekutuma uje ukaiongelee? marehemu hayo ndo maandalizi aliyoyafanya juu ya familiya yake kwa kadri ya uwezo wake, wewe nawe jiandae kwa kadri ya uwezo wako. Kama kuna mtu kapata hela kupitia msiba huo zitaisha na bado naye ipo siku atakufa, mwacheni ndugu yetu apumzike kamaliza kazi yake hapa duniani na si wakati wa kumjadili.
 
Nimefurahi kukubali kwamba Uncle J alikuwa na uwezo mkubwa wa kuweza kwenda nje, je, umejiuliza kwa nini hakupata nafasi hiyo hadi kwenda kufia Morogoro badala ya Uingereza ua Ujerumani? Kuna wengi hawakuwa na uwezo wa kufanya kazi kama Uncle J lakini walibebwa na kupewa fursa hizo. Naamini kuwa Uncle J alikuwa na marafiki wengi na wengine wanafanya kazi nje ya nchi,jiulize nani aliyekwenda hata kumpa ushauri wa mawazo kwamba asiende Morogoro na kumshauri kwenda nje?

Sote tunajua uwezo wa Uncle J, lakini je yeye binafsi alikuwa na ndoto/nia ya kutaka kufanya kazi nje ya Tanzania?

Pili, kwani huyo bwana akiwa hai kuna juhudi zozote alizozifanya za kujaribu bahati yake kufanya kazi mashirika ya habari ya kimataifa?

Kama alijaribu na kushindwa, je ni kuna watu waliomkwamisha? Ni kina nani hao?

Je hao waliomkwamisha mafanikio yake ndio hao walioshadadia shughuli nzima ya msiba wake?
 
Basi waswazi wataanza kumsema charles hillary kwa nn hajaja kuxika. hovyoooo
 
Nimefurahi kukubali kwamba Uncle J alikuwa na uwezo mkubwa wa kuweza kwenda nje, je, umejiuliza kwa nini hakupata nafasi hiyo hadi kwenda kufia Morogoro badala ya Uingereza ua Ujerumani? Kuna wengi hawakuwa na uwezo wa kufanya kazi kama Uncle J lakini walibebwa na kupewa fursa hizo. Naamini kuwa Uncle J alikuwa na marafiki wengi na wengine wanafanya kazi nje ya nchi,jiulize nani aliyekwenda hata kumpa ushauri wa mawazo kwamba asiende Morogoro na kumshauri kwenda nje?

Si tunaambiwa alikuwa mgonjwa muda mrefu yaani muathirika na navyojua mimi makampuni mengi ya nje ni lazima wakupime afya . Nisaidieni mnaojua zaidi
 
Si tunaambiwa alikuwa mgonjwa muda mrefu yaani muathirika na navyojua mimi makampuni mengi ya nje ni lazima wakupime afya . Nisaidieni mnaojua zaidi

Mmmmmh......!!
 
Wakati alipokuwa akiumwa, Mtangazaji mahiri hapa nchini, Julius Nyaisangah hakuna hata mwanahabari mmoja aliyekuwa akijali afya yake, wanahabari wa Dar es Salaam hawakuona umuhimu wa kuchangishana na kumhudumia mwenzao lakini alipofariki dunia waliamua kuuteka msiba na kuuleta Dar es es Salaam. Wakatoa ahadi ya kuupeleka kwa ndege mwili wake hadi kijiji kwake alikozaliwa huko Mara.

Hata hivyo, hawakutimiza ahadi hiyo ya kumpeleka kwa ndege baada ya kutafuta umaarufu pale Leaders Club na kisha mwili ukasafirishwa kwa gari hadi huko kwao. Kwa nini basi, waliamua kuuleta mwili Dar? Je, kulikuwa na shinikizo la nani?

Pili, kwa nini waliidharau kamati ya mazishi ya Morogoro kwa kubadilisha jeneza la kumbebea mwili wake na kumweka katika jeneza lingine? Kama kweli walikuwa na uchungu na Julius kwanini hawakujikusanya na kwenda Morogoro kuungana na kamati ya mazishi ya kule na kuangalia upungufu uliopo na kuukamilisha.

Naamini kabisa kwamba Abood alikuwa amejiandaa vyema kuusafirisha mwili wa Nyaisangah hadi kijijini kwake na kila kitu kilikuwa kimekamilika, je kamati iliyoundwa Dar ilikuwa ya kisiasa au kutaka umaarufu.

Ikumbukwe kuwa Nyaisangah alikuwa amefanya kazi Redio Tanzania na Redio One na kikatokea cha kutokea na kuacha kazi, alikuwa na marafiki wengi ambao hawakuweza kumsadia na kumfanya kuwa mmoja wa watangazaji ambao wengeweza kwenda kutangaza katika vyombo vya kimataifa ( vye nje) lakini marafiki hao hawakuwa na msaada wowote kwake, baada ya kufariki ndiyo kila mtu anajidai kuwa ndugu, rafiki na wa kumuonea huruma.

Watz, tuache uzandiki huu wa kuithamani maiti na kutomjali mtu wakati akiwa anaumwa. Binafsi nisingependa kuona hiki kitu kikijirudia kwa mtu mwingine.

Kibaya zaidi wakawadanganya wafiwa waliokuwa wamebaki Morogoro ambao ilikuwa wasafiri na msiba kwenda Musoma, kuwa walishawaandalia usafiri wa kutangulia Musoma wakati mwili ukija kuagwa dar. Matokeo yake waombolezaji wale wakatelekezwa pasipo kujua wafanyeje, ikabidi wausubiri mwili utoke dar ndipo waanze safari ya pamoja kuelekea Musoma. Hili pia halikupendeza!
 
Jifunze jambo moja!!!!

Ukiwa hai imarisha sana familia yako na kuijengea misingi imara ya kusimamia mambo yao bila kushirikisha watu wa mbali na vikundi shirikishi!!!!

Rafiki zako ni rafiki zako wewe once haupo hawana dhamana ya kusimamia uliyoyaacha kama mlikutana.bar ili mnywe na wewe ushakufa na huwezi kunywa you are good for nothing!!!!!Mke au mume ndio mpango mzima ukitoka hapo ni wadogo au wakubwa zako na spouse kwa umoja,hao marafiki ni kama wataamua kushiriki hawafungwi popote!!!!!

Hivi umefiwa wewe wanakuja marafiki wa marehemu ndugu yako na kukuambia tunaomba sijui tupeleke mwili sabasaba sijui heshima.imefanyaje na unakubali????!!!!!! THIS SIGNIFIES NOTHING BUT A WEAK FAMILY!!!!!!!

TUKIWA HAI TUJENGE FAMILIA ZETU JAMANI

hapo ndipo palipo na logic. kwa uelewa wangu waombolezaji ndio hua wanaufata msiba na sio msiba kuwafata waombolezaji
 
waandishi wa habari wa tanzania hawana umoja kabisa , hiyo ndiyo taasisi mbovu kuliko zote , japo wanapenda sana sifa ! Ni heri hata umoja wa waendesha bodaboda wa Yombo vituka !
 
Back
Top Bottom