Nusu kilo ya Sukari utaigawa vipi mara TATU....!

Nusu kilo ya Sukari utaigawa vipi mara TATU....!

Baba_Enock

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
7,076
Reaction score
2,465
Sikonge....

"Nusu kilo ya Sukari utaigawa vipi mara TATU" Huu wimbo uliimbwa na Band Gani?

Una ujumbe mzito kwa wana MMU...!
 
Last edited by a moderator:
unagawa mara mbili nusu nusu, hivyo wakwanza anapata robo, wawili waliobaki wanapata kila mmoja 1/8.
Easy eeh!
 
anasema "..........ulituweka ndani sisi wanawake watatu, kanga na vitenge kwetu sisi ni haba, mchele wa kitumbo kwetu ... nusu kilo ya sukari utaigawa vipi mara tatu..........." ila sina comments kwa sasa.
 
...kwaheri mpenzi yooyo ninarudi kwa baba na mama walionilea,sio kama sikupendi bali ni NJAA inayonifanya nikimbie nyumba yako...

Vijana wajifunze,wanawake kila mtaa wakati uwezo haba!mwishowe majanga!
 
Ahh Baba Enock na wewe bana, google ipo Mkuu wangu.

Haya ngoja nikupakulie kutoka kwa wakali wengine wa miziki maana mie hapa nimeachwa Solemba 🙂

Baadaye Shabaan Dede alihamia Bima Lee Orchestra ambako alishirikiana na hayati Jerry Nashon 'Dudumizi' na Roy Bashekanako kuimba kibao cha 'Milionea wa mapenzi' ambapo aliimba uhusika wa mwanamke aliyeolewa ukewenza. Anaghani kwenye baadhi ya mashairi;
"Umetuweka ndani sisi wanawake watatu,
Kanga na vitenge kwetu sisi ni ndoto,
Mchele wa kitumbo kwetu sisi almasi,
Nusu kilo ya sukari utaigawa vipi mara tatu"

Ni hapo hapo Bima Lee Orchestra 'Wana Magnet Tingisha' ambapo Jerry Nashon 'Dudumizi' naye aliibuka na kibao juu ya mwanamke aliyetimuliwa na mumewe 'Baba Shani' ambapo anaimba;

"Mume wangu amenifukuza,
Na kuniumbua mbele za watoto,
Kanifukuza kisha kamleta mwanamke ee baba,
Kula taratibu baba usimalize yote,
Mali tumechuma wote ni haki ya watoto ee baba"


Hii nimeitowa:
http://www.raiamwema.co.tz/wako-wapi-waimbaji-wa-kike%C2%A0muziki-wa-dansi-nchini

Sikonge....

"Nusu kilo ya Sukari utaigawa vipi mara TATU" Huu wimbo uliimbwa na Band Gani?

Una ujumbe mzito kwa wana MMU...!
 
Back
Top Bottom