mbinguni
JF-Expert Member
- Jan 2, 2013
- 2,767
- 1,068
Nathibitisha kwamba Ramadhan Ighondu alitambulishwa kwetu kwa jina la Abeid. Binafsi ninamfahamu sana bwana huyu kwa sababu alikuwa akitumwa mara kwa mara kuja kukutana na mimi na tumekutana mara kadhaa kabla ya tukio lile, lilisomeka tamko hilo na kuongeza: Nakumbuka kuwa Abeid alitambulishwa kwetu na kigogo mmoja, nikiwa pamoja na wawakilishi wengine wa madaktari kuwa yeye (Ramadhan Ighondu) ndiye atayehusika katika kuchukua madai na hoja za madaktari katika mgogoro kati ya madaktari na serikali.
Nathibitisha kwamba mfanyakazi huyu wa Ikulu, ndiye aliyenipigia simu na kuniita kwenye kikao ambako muda mfupi baadaye nilitekwa. Katika mawasiliano hayo, Abeid alikuwa anatumia simu Na. 0713 760473, alisongeza Dk. Ulimboka kupitia tamko hilo.
Wana JF naomba tuijadili nukuu hii kwa fikra mbadala.Karibuni.
Source:Tanzania Daima 18/1/2013.