Wagonjwa mbona wanateseka hata leo hii ambapo hakuna mgomo na walikuwa wakiteseka hata kabla ya Dr.Uli kutekwa!
Kwa sasa DCI Manumba yuko ICU anateseka kwa kupumlia mashine huku akiwa na vijidudu 500 vya Malaria! Nani wa kulaumiwa?Je, Dr.Uli na watumishi wengine wa afya wanahusikanaje hapa????
Hoja yangu ni kwamba mgomo wa Madaktari haukuhusika na mateso ya wagonjwa baali kile kilichokuwa kikipiganiwa na hao Madaktari ndiyo kingeliondoa mateso kwa wagonjwa. Bila vitendea kazi bora na muhimu afya ya Mtanzania siku zote iko rehani. Kama hakuna maabara zenye kupima ugonjwa husika kwa uhakika ni kazi bure. Kama hakuna CT-scan, hakuna X-rays machine, hakuna Ultra Sound, hakuna Stesoscape, hakuna Madawa muhimu ni upuuzi kumlaumu daktari! Bado kuna dada zetu na mama zetu wanajifungulia kwenye sakafu za hospitali na zahanati kwa kukosa vitanda au wanalala mzungu wa nne! Kila mtu analijua hili lakini kwa vile kuna watanzania wahuni na washenzi wanajifanya kuwa vipofu na kuamua kugandamiza haki za sekta muhimu kama hii!!Shame on them. naamini siku ya kiyama watajibu mbele za Muumba kwanini walisababisha vifo vya wagonjwa kwa maksudi!!!
Serikali ndiyo inayosababisha mateso kwa wagonjwa na ilikosea sana kutaka kuzima mgogoro huo wa Madaktari kwa nguvu ilhali Madaktari walikuwa na hoja za msingi.
Tafakari.
We unajua madokta wangapi sasa wanapiga part time kwenye hospital binafsi? Hivi wangelipwa mshahara wanaotaka unadhani isinge washawishi kutumika katika hosp za serikali mwanzo mwisho?
Chukulia mfano wewe kama Nape hajakupa posho yako leo utakubali?
Hawezi kukubali ila ndo hivyo yuko kabaruani anawajibika.
Serkali haiwezi kukwepa jukumu lake la msingi kwa W atanzania la kutoa hata Primary Health Care lakini upande mwingine vijana wengi sasa hivi wanasomeshwa na serkali udaktari cha kushangaza Maktaktari ktk Chuo Kikuu cha Umma wamegoma kufundisha Clinical subjects Hospitalini wakidai posho kisa tu imechelewa kuletwa kwa muda na lazima walipwe,nauliza uko wapi uzalendo wetu vijana, hili halihitaji propaganda za wana siasa, wazazi wetu, ndugu zetu watoto wetu na Watanzania tuwe na hofu ya Mungu kama Uzalendo ni shida,
NAUNGANA NA WOTE WENYE MAPENZI MEMA KULAANI YALIYOMPATA DR. ULIMBOKA, MUNGU AMPATIA MAISHA MEMA KILA MTU AWJIBIKE NA SIYO KISASI.
Osama hufai kabisa je unajua ni watu wangapi wamekufa leo kwa kukosa panadol na akina mama kukosa cloves za kujifungulia na vifaa vingine.
Waitaka mishahara minono kama ya wabunge ambao hata wakigoma hats sisimizi hafi?wale walikuwa wanadai mishahara minono, mengine ilikuwa ni kuwadanganya watanzania. shame on you and them
wakati mwingine ,haki haipatikani ila kwa ncha ya upanga, katika kudai haki lazima damu/ roho za watu zipotee, usitegemee ccm itaondoka hivihivi MADARAKANI ,kwa sababu Hao tayari ni watenda maovu kwa HIYO hawataondoka hivihivi 4get ittujadili na wagonjwa walioteseka kwa kukosa matibabu wakati madaktari wamegoma
mishahara ya 3.5ml/= huku watanzania wanateseka kwa kukosa panadol,hata huruma hatuna
Mbona Manumba amewaacha Muhimbili amekwenda Agakhan? Bado mgomo unaendelea?Umesoma kwa kodi za watanzania maskini unalipwa mshahara kwa kodi za watanzania maskini unagoma kuwatibu watanzania maskini, huu sio ubinadam hata kidogo
mishahara ya 3.5ml/= huku watanzania wanateseka kwa kukosa panadol,hata huruma hatuna
wagonjwa zaidi ya mia tatu 300 walikufa kwa kukosa huduma za madaktari waliokuwa ktk mgomo wa kijinga
mishahara ya 3.5ml/= huku watanzania wanateseka kwa kukosa panadol,hata huruma hatuna
kwa kuchangia hoja hii JF si ajabu ikafungiwa kama gazeti la mwana halisi"Nathibitisha kwamba Ramadhan Ighondu alitambulishwa kwetu kwa jina la Abeid. Binafsi ninamfahamu sana bwana huyu kwa sababu alikuwa akitumwa mara kwa mara kuja kukutana na mimi na tumekutana mara kadhaa kabla ya tukio lile," lilisomeka tamko hilo na kuongeza: "Nakumbuka kuwa Abeid alitambulishwa kwetu na kigogo mmoja, nikiwa pamoja na wawakilishi wengine wa madaktari kuwa yeye (Ramadhan Ighondu) ndiye atayehusika katika kuchukua madai na hoja za madaktari katika mgogoro kati ya madaktari na serikali.
"Nathibitisha kwamba mfanyakazi huyu wa Ikulu, ndiye aliyenipigia simu na kuniita kwenye kikao ambako muda mfupi baadaye nilitekwa. Katika mawasiliano hayo, Abeid alikuwa anatumia simu Na. 0713 760473," alisongeza Dk. Ulimboka kupitia tamko hilo.
Wana JF naomba tuijadili nukuu hii kwa fikra mbadala.Karibuni.
Source:Tanzania Daima 18/1/2013.