NSSF yazidi kuweka Historia: Inajenga Sports Academy imeingia ubia na Klabu ya Real Madrid

Nawapa hongera sana NSSF kwa uchapakazi wao, endeleeni kufanya mazuri roho za husda uwa azikosi.
 
Mnawekeza lakini wanachama wenu hawapati riba ya kile mnachokifanya

Umenena mkuu, hapo ndipo wizi wa macho makavu ulipo; haya mashirika ya pensheni hawaangalii thamani ya pesa ya mwanachama.

Hata wasingefanya hayo yote wanayojivunia, wange recover tu thamani ya pesa za wanachama mimi ningeridhika.
 
Excellent.
hata hivyo kuna malalamiko mengi sana juu ya watendaji wenu huku chini. wamulikeni kwani wanawaharibia sifa yenu nzuri.
 
Uwekezaji mzuri, lakini huwa najiuliza iwapo mnafahamu shida wanazozipata wanachama wenu. Nina mifano mingi ya wafanyakazi ambao ni wanachama na wanachangia kila mwezi. Cha kushangaza wanapofika katika kuulizia statement ya Michango yao takwimu hazieleweki. Kama unabisha ndugu yangu waulize wenzako wa tawi la Mwanza. Tatizo jingine lipo kwa wastaafu. Baba yangu alistaafu mwaka jana akiwa mwanachama wa NSSF, shida aliyoipata kwakweli ni ajabu. 'Njoo kesho' hazihesabiki hadi pressure ilipanda na alitamkiwa waziwazi atoe rushwa ndio mafao yake yashughulikiwe. Wenzake walitoa rushwa na haikuchukua muda wakapata mafao yao. Yeye nilimkataza asitoe kwani nilimuambia haiwezekani anunue haki/mafao yake, wakaamua kumkomoa. Lakini pia mzazi wangu huyo alikuwa akikumbana na lugha zisizofaa zilizojaa kejeli na matusi ya waziwazi. NSSF MSIVAE SUTI BILA YA SOKSI NA VIATU TENA MIGUU YENU IKIWA MICHAFU. Haya si ya kutunga, nime experience.
 
NSSF kabla ya Dau ulikuwa ni uozo kama mashirika mengine ya umma, lakini leo ni Shirika la mfano Tanzania na Afrika.
 
MrNSSF wapi naweza pata balance sheet ya NSSF ? Kama ni document ya siri iko kabatini kwa Dau au zimefukiwa chini kama hati ya muungano nijulishe mkuu manake za NSSF kenya na Uganda ziko online they are just a click away .
 
NSSF kabla ya Dau ulikuwa ni uozo kama mashirika mengine ya umma, lakini leo ni Shirika la mfano Tanzania na Afrika.

Tupia financial statements za past three years tuone kama uozo umeondoka. Unaweza kuwa victim wa window dressing.
 
Mimi ntafurahi sana hii mifuko ya hifadhi ikiacha kua ya kulazimishana kama kodi. Kama mfanyakazi nataka kujihifadhi mwenyewe kwanini ninyanyaswe na kushurutishwa?
 
acha unafiki wewe uhafidhina umekujaa

Hilo ni wazi kabisa wala halina utata.

Roho zinawauma, kwanini huyu na si sisi. Nyie na wazee wenu mmeiba sana mali za umma lakini mpaka leo hamna maendeleo hata chembe. Si yenu si ya nchi. Sasa wanaemeeshe makaburu tu kwa kunywa sana na wao wanawatengeneze tu, kila aina yapobe muwanemeeshe vizuri, mna akili zaidi ya kulewa?

Tazama Dau mambo aliyoyafanya na anayoyafanya kila kukicha, NSSF imekuwa shirika la kuigwa Afrika nzima kwa muda mfupi tu aliokuwapo Dau, mbona hatukuyaona kwa wajomba zenu walipokuwepo hapo?
 
Hilo ni wazi kabisa wala halina utata.

Roho ziwauma, kwanini huyu na si sisi. Nyie na wazee wenu mmeiba sana mali za umma lakini mpaka leo hamna maendeleo hata chembe.

ImageUploadedByJamiiForums1422625164.133134.jpg

Sawa jioni njema
 
Nikiwa mwanachama wa NSSF mwaka 20 sasa bado sijaona faida ya fedha zangu zinazokatwa bila ridhaa yangu kibaya zaidi ni huyu Dr Dau anavyochezea fedha zetu bila udhibiti wowote.

Ujenzi wa daraja sijui kituo cha michezo kinanisaidia vipi mimi mwanachama ?.Ni kwanini hakuna uwakilishi madhubuti wa wafanyakazi katika bodi ya NSSF kila siku serekali inachota fedha kibao kwaajili ya kuendesha shughuli zake za kawaidi badala ya kutegemea kodi inayotozwa na TRA.Mfenyakazi Tanzania ni majanga matupu.
 
Back
Top Bottom