NSSF yambambikia F. Mbowe deni, hii haikubaliki

Swali ambalo wa-bongo wote tunabidi kujiuliza ni hili: hivi hii mifuko ya jamii ina sera za kukopesha watu au tasisi pesa? Mbona hiyo ni kazi ya ma-bank. Au kwa sababu wana hela zetu nyingi wanafikiri wanaweza kutoa mikopo ovyo ovyo. Ndio maana wa CCM wanachukua huko, hawakopi.
 
Tatizo la baadhi ya wana JF kila kitu wanaleta ushabiki wa vyama na kuondoa kabisa uwezo wa kutafakari kwa kukubali majibu mepesi, ni kweli Mbowe ana deni kubwa NSSF hilo halina ubishi nina uhakika si bahatishi na kuna kipindi NSSF ilikuwa inataka kukamata kiwanja chake cha pale moshi mjini. Ki ukweli ni mapugufu kwa mtu yeyote kuchuka pesa hovyo kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii bila ya kuzirudisha kwani ni pesa za wanachama.

Usipanic,

Ni kweli Mbowe alikopa NSSF, na kwasababu ni mfanyabiashara anaweza kuwa alikopa sehemu nyingi tu sana kwasababau nyingi mno.

Pili ni kweli alilipa deni, je lilikwisha hilo anajua yeye na mdeni wake. Tatu ni kweli hadaiwi billioni kama inavyosemwa na wanasiasa.

mada inajikita kwenye hoja ya msingi, je ni kweli anadaiwa na anatafutwa kama mawaziri walivyosema ? Je hana haki ya kuwa mfanyabiashara, soma mada ya msingi nini amejibu. Je NSSF si wapo waje au wafanyakazi wa nssf waseme ni kiasi gani anadaiwa kama msingi na kiasi gani riba, na je deni liko active au collections?

Na waweke wazi ni wanasiasa wangapi wanadaiwa na nssf na madeni ya muda gani, je wanasiasa wangapi walitumia collateral ili tuweze kupata fedha zetu ?

Mbowe anaandamwa kwasababu tu ni mwanasiasa mpinzani. Kama kuna kosa limetokea liwekwe wazi, kama kavunja sheria iwekwe wazi, sio kumsakama tu.

Wabunge wa ccm wameomba fedha zisizozao na kwasababu ya ubabe wao wamechukua fedha zangu nilizochangia NSSF kwa kugawa rushwa kwenye majimbo yao hii inaniuma sana. Mbowe kakopa na karudisha na riba ili mimi na wewe tuweze kulipwa mafao yetu, kama bado tunamdai tunadai faida. Ila hawa wa lumumba wamechukua principle ya fedha yangu ninayokatwa kila mshahara kuchangia.
 
kwani NSSF wanakopesha? Mi ni mwanachama na siku zote sikuona mkopo!
 
Kama Mbowe alikopa 15M anadaiwa 1.2B je Sumaye tunamdai ngapi alikopa 50M. mhh inawezekana 200Bilioni.
 
kama anadaiwa si wachukue hatua za kisheria? Hii inshu imekaa kisiasa na mi naona ni propaganda chafu tu dhidi yake baada ya kuona ccm imezidiwa kila kona.
 
naomba ukweli, balanced report always is good for me. Itendee nchi yako haki. Tiririka ......

Tiririka wewe uliyesema kabambikiwa.

Hivi NSSF yote mijitu iliyobobea na mi CPA iwe miongo na msema kweli na ajuae mahesabu ni Mbowe, school failure?

Mbowe huyuhuyu aliyeundanganya umma kuwa hataki shangingi? akalirudisha mlango wa mbele akaenda kuhukuwa lingine mlango wa nyuma?

Hoja zingine ni ujinga mtupu.

Akalipe deni au aombe msamaha.
 
Acheni kudanganyana mbowe alikopa 500ml. Enzi hizo akakataa kulipa deni kwani ilikuwa linaongezeka siku adi siku, wakampeleka mahakamani nssf wakashinda kesi n akatakiwa kulipa jamaa akawa hana pesa kilichofatia nssf wakapewa kibali cha kumkamata, serikal ikasema subirn kwanza hii ishu ndio itakuwa njia ya kufanikiwa kisiasa....so ndiomana unaona mbowe anakujaga juu na serikali ikimkumbusha liledeni mbowe anachanganyikiwa, mwisho wa siku anakuwa mpole
 
Tiririka wewe uliyesema kabambikiwa.

Hivi NSSF yote mijitu iliyobobea na mi CPA iwe miongo na msema kweli na ajuae mahesabu ni Mbowe, school failure?

Mbowe huyuhuyu aliyeundanganya umma kuwa hataki shangingi? akalirudisha mlango wa mbele akaenda kuhukuwa lingine mlango wa nyuma?

Hoja zingine ni ujinga mtupu.

Akalipe deni au aombe msamaha.

Fox aombe msamaha wa nini ? hapa ni deni ama kulipa ama deni limebambikwa ndio hoja.

Mawaziri wa JK wamesema anatafutwa kwa kudaiwa billions na NSSF. Ubambikiaji ni huu hizi tarakimu. Yeye mwenyewe kasema alikopa 15M na kalipa 80M 65M ikiwa ni riba.

Sasa Je hizo billions alizosema Ghasia na mwenzeka jina unalo wamezitoa wapi? Je NSSF wanasemaje?

Kumbuka NSSF wanamichango yangu mingi sana nategemea kula mafao yangu hivi karibuni.

Hivyo ningependa waache kabisa kugawa sadaka kwa wanasiasa. Mbowe yeye kakopa kalipa kama hajamaliza najua alitupatia dhamana tutakula, ila kwa hali ilivyo everything have been paid. Kama kuna ushahidi wa mabilioni ya ghasia tuwekeeni.
 
Acheni kudanganyana mbowe alikopa 500ml. Enzi hizo akakataa kulipa deni kwani ilikuwa linaongezeka siku adi siku, wakampeleka mahakamani nssf wakashinda kesi n akatakiwa kulipa jamaa akawa hana pesa kilichofatia nssf wakapewa kibali cha kumkamata, serikal ikasema subirn kwanza hii ishu ndio itakuwa njia ya kufanikiwa kisiasa....so ndiomana unaona mbowe anakujaga juu na serikali ikimkumbusha liledeni mbowe anachanganyikiwa, mwisho wa siku anakuwa mpole

mhhh loading!

Hivi ukidaiwa billions, ukakamatwa ukapelekwa jela unakaa miaka mingapi deni liishe??? Sina uhakika kama sheria inasema mdaiwa ambaye amekopa na akahitajika kuweka dhamana mali akishindwa kulipa kuna swala la kuwekana jela ama ni kufilisi mali alizoweka dhama.

Naomba kama kuna wanasheria wanisaidie sheria za tanzania zinasemaje kuhusu madeni na kukupa hasa NSSF kwani naona taratibu zake zinaongelewa tofauti na mabank mengi.

Wapo wadaiwa sugu wengi Tanzania kama sheria zinasema kufungwa mbona sijasikia akifungwa mtu kwa kushindwa kulipa deni? Nimeshuhudia minada mingi mmoja wapo wa nyumba ya memose cheyo.
 
Kwahiyo deni limegeuka fimbo ya kumnyoosha na hawana haraka ya kumdai kwa nguvu mpaka wakati mwafaka.
Mi naona wanachadema wamchangie deni liishe,vinginevyo mambo hayataenda.
 
Kwahiyo deni limegeuka fimbo ya kumnyoosha na hawana haraka ya kumdai kwa nguvu mpaka wakati mwafaka.
Mi naona wanachadema wamchangie deni liishe,vinginevyo mambo hayataenda.
Mkuu umenena ni vyema makamanda wakachanga au kuchukua pesa za ruzuku na kumlipia mwenye kiti deni.

Kamanda Mungi na Crashwise mnaonaje hili wazo la kumaliza mzozo?
Au makamanda tupitishe makapu tukiongozwa na Godbless J Lema huko kwenye mikutano hili kumaliza huu mzozo.

Tumshirikishe Lipumba hili swala na Ukawa.
 
Last edited by a moderator:
mnabishana na mpiga disco?

Real!

Ni kwa vile majina yenyewe hapa kitalani.

Kwani kupiga disco kuna ubaya gani? Kila mtu anaweza kupiga disco? Unafikiri ni kazi rahisi? Ni wangapi walikuwa na kumbi za disco leo ni magofu? He is smart and intelligent hilo halina ubishi.

mafanikio ndio yanapina kiwango cha akili na werevu wa mtu. Kila mtu anaweza kupata degree, masters, na phd. Hizi elimu za darani zina formula moja tu kusoma vitabu vilivyoandaliwa, period. Ukivisoma vingi huku unalishwa na umetulia unatunukiwa vyeti, hakuna kitu unatakiwa kufanya zaidi ya kuigiza nini wenzako wameshafanya.

Ila ukiachwa porini bila fedha ama na fedha unatakiwa ujue utaziongeza vipi hapa hakuna kukariri inahitajika akili, ubunifu, maarifa na kufikiri out of the box. Yes he did it more tha 20 years na dico and he does very well.

Kwa hiyo unaweza kumuita Bakheresa muuza lamba lamba kwasabu tu hana lundo la vyeti vya darasani, wangapi wameshindwa kuwa yeye.

Ukisoma masoma masomao mengi duniani ni historia za wale waliofanya bila vitabu, Dr Isaac Newton, Gallileo, Dell, Bill gates, nk

Kina Mbowe ndio sababu ya vitabu vya biashara kuandikwa. TZ ingekuwa nchi inayotukuza kazi, ubunifu ufanyaji kazi na kujituma leo tunekuw ana vitabu vya maisha na mafanikio na kushindwa akina Salum Bakheresa, Kiswele, Ngorika, Mengi, Maburuki, Makosa -iringa, nk.

Tungesoma ni vipi mtu ambaye hajamaliza darasa la saba aliweza kuwa tajiri ungewa activate wote wanaoona bila shule kubwa kubwa hawezi kitu, tungesoma vitabu vya maprofessa vipi walifanikiwa wale wenye uwezo wa kukariri vitabu vingi wangejifunza baada ya kukariri kitabu inakupasa kufikiri nje ya kitabu ili kufanikiwa.

Badala ya kutumia hasira za umasikini kulaumu waliofanikiwa kwa kuwarushia maneno ya kashfa na kuonyesha usongo wa mawazo wengi waliokuwa nayo.

Ni kwanini basi wakija nchini watu kama JZ, kanye west, hayati Luck dube, Dell, Bill gates, Wacheza movies wa holl wood wenye fedha nyingi bila elimu msiwaone hawafai? Mbona vitabu vingi mnavyosoma ni maisha ya watu wasio na formal education bali uwezo mkubwa wa kufikiri na kutenda.

One day will understand. .... loading.
 
hivi kweli hana 1.2bn? si asme wamlipie! huu ni ukorofi tu, zile pesa alouza mafuso siangelipa deni!
 
Back
Top Bottom