NSSF watolea ufafanuzi ufadhili wa Clouds Media Group (Harusi ya Billnas na Nandy)

Ameeleza kwa kirefu lakini sielewi au yeye haeleweki.
Aseme kwa kifupi kwamba walipeleka matangazo CMG.Kama siyo hivyo basi kuna halufu siyo nzuri
 
Kuna muda hizi taasisi zinareact kwenye ujinga..... kibiashara hii ni ishu ya kawaida katika kutangaza huduma yao sioni wanajitetea nini hapa na ilikua ni sehemu sahihi kutangaza huduma.... licha ya aina ya watu walohudhuria ila pia matangazo yalikua live.
Yaani siku zooote hatangazi huduma, ila baada ya kusikia flani anaoa, basi ghalfla bon vuu ndio akili ya kutangaza huduma inakuja, au sio?
 
Nimekutana nayo toka mitandao ya kijamii
9d43ccab-1a3c-4ae0-8a67-22d2bc0379c9.jpg

87e45f39-6933-4472-be9c-22589ecff77e.jpg
 
Nimekutana nayo toka mitandao ya kijamiiView attachment 2294853
View attachment 2294854
Gharama yote hiyo NSSF iliyoingia kwa ajili ya bando la wavuka daraja la Kigamboni au na wakazi wa mikoa yote Tanzania? Yaani mkazi wa wilaya ya Tanganyika anaweza kununua bando hiyo na akawa anavuka daraja la Kigamboni? This must be Black Magic, sasa tunaruka kwa ungo.

Nawashauri muweke kanusho jingine kulikanusha kanusho hili ambalo bado halijajibu maswali mengi, ingekuwa bando za mitandao ya simu huenda kanusho lingekidhi lakini hili la kununua bando pale darajani kama zile za mwendokasi na kivuko cha magogoni mnafanya udhamini badala ya tangazo!

Acheni hizo, mmechukulia watanzania ni wajinga wa kila kitu lakini si wajinga kiasi hicho, rudisheni pesa za wanachama wa NSSF maana sasa mnadhamini mpaka kutembelea nyumba mnazojenga huku mkiwaacha wanachama hoi kwa malipo hafifu!
 
Huyu lulu anavyotapatapa.

Hivi wewe lulu Jana jumapili ulikwenda ofisini?

Au hilo libandiko umelitype ukiwa sebuleni kwako na kulirusha hewani sidhani kama lina ridhaa ya management ya NSSF.

Acha kutapatapa Kwa hili umemuingiza chaka DG wako
 
Unatumia pesa kusimamia harusi za hao mnaowaita mastar brand ...upuz huuuu

Ova
 
Back
Top Bottom