NSSF na fao la kujitoa

NSSF na fao la kujitoa

Nenda tu ofisi yoyote iliyo karibu nawe. Hata hawana usumbufu siku hz na unachukulia hela yako popote tu ulipo, sio lazima urudi ulipokuwa unafanyia kazi.
Na hata fomu zao siku hizi zimeboreshwa sana, hazina mambo mengi ya kujaza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yeah hata pale Ilala boma wanatoa! Mm nachukua changu kila mwezi sema ni 33.3% ya mshahara wako wa mwisho. Hii ni kwa kazi za taaluma zote!
 
Kwa sasa nimejipanga nimpeleke mtumishi mmoja au wawili takukuru maana nimeona wanatengeneza mazingira ya rushwa toka mwaka jana mwezi 11wananizungusha tu.
 
Wanalipa ila sio kwa haraka, wasumbufu sana, unatakiwa kukaza ikiwezekana na mikwara juu!
Ngoja uzirudishe ndiyo utajua kiini cha mjadala huu. Hao NSSF ni mumiani kabisa wanang'ang'ania hela zetu kama zao vile.
 
Upo my aim high mate?
Bado upo diamond region Mimi still napambana huku makinikiani kabla acacia na barrick hawajagawana fito na GoTz
Mi navyojua lipo, kwsbb nilienda wiki iliyopita siku ya jtano nikapewa fomu na sasa nimezituma kwa mwajiri ajaze na kuweka mhuri kisha nirudishe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo my aim high mate?
Bado upo diamond region Mimi still napambana huku makinikiani kabla acacia na barrick hawajagawana fito na GoTz
Nipo nipo mpenzi, hlf yaan ngoja nije inbox kwanza maana nahisi nilikufaham kitambo kupitia kwa mpuuzi flani hv.
 
Acheni uwongo nyie Rais alisema ntu apewe akifie mbele lkn ss hv ukienda unaambia ww km proffesional katafute kaz ss huwa nashindwa kuelewa Rais alituongopea kutwambie tukachukie chetu?


Mkuu na utu uzima wako ukamwamini jiwe?
You can’t be serious
 
Wakuu nimeweza kupewa fao la kujitoa kwa sababu ya matatizo ya mwanangu.Nikutoa vielelezo na pia kuongea vizuri na mameneja wa Nssf,hapa sizungumzii rushwa nazungumzia kauli nzuri nakujieleza.
 
1 - Tangu Rais aseme wafanyakazi wapate FAO LA KUJITOA, bado hii haki kupatikana..Sekta binafsi ni kilio kila uchao, NSSF wameshindikana na waziri jenister mhagama ni kama ameipotezea kauli ya Rais ya kuifuta sheria mpya hadi 2023- Kwa nini wizara isipeleke marekebisho bungeni kufuta sheria kandamizi? ---Serikali Ya Kibeberu kukandamiza wanyonge.

2.Yaani wafanyakazi sekta binafsi wanafanya kazi katika mazingira magumu sana, bado mshahara ni kdg sana...halafu na kupoteza kazi ni any time....Bado Mabeberu wanakaba na kale ka Akiba
 
Kinacho zungmziwa cha 2023 ni kikokotoo cha zamani kuendelea kutumika, kikokotoo sio fao la kujitoa kikokotoo ni kwa ajili ya mtu anaepata malipo ya mkupuo na anastahili pensheni. Fao la kujitoa sasa ni kama hakuna kwasababu ni wenye ajira za mkataba tu na wageni ndo wanapewa fao la kujitoa wengine wote utapewa fao la kukosa kazi tena lazima umeachiswa kazi sio wewe kuacha. Kujibu swali lako kama ajira yako ni ya mktaba utapewa fao la kujitoa na hapo lazima mkataba uwe umesitiswa na muajiri sio umeacha kazi makusudi.
 
Lets say nina umri wa miaka 35, nimefanya kazi katika kampuni ya kigeni - kampuni imefungwa wanaondoka wanarudi makwao. Fao langu kwa miaka 7 niliyofanya nao kazi ni zaidi ya 45m. Serikali inaniambia ati nitafute kazi nyingine ili niendelee kuchangia.....nimetafuta kazi mwaka wa pili sasa sijapata naishi kwa kuombaomba... chakula shida, pa kulala ni shida - Nahangaika hivi wakati nina 45m zipo NSSF - Je hii ni HAKI.

FAO la kujitoa HOJA nzito mno ....wafanyakazi tuchague chama kinachokuja na SERA bora hasa kwenye FAO hili.
 
Turudishieni FAO LA KUJITOA..Tunaishi maisha magumu jamani vipesa vyetu imevishikilia huku mitaani twafa njaa...

Yaani unashindwa hata kujiajiri, hivi kwanini mliamua kututungia hii sheria kandamizi jamani...Wengine since 2017 sijapata changu hata hilo fao la kukosa ajira ni USANII tu...Tuhurumieni jaman enyi miungu watu
 
Sheria ya mifuko ilitungwa na serikali ili kumuwekea mfanyakazi kinga dhidi ya ukosefu wa kipato pindi AKISTAAFU(SYO KUKOSA KAZI)
Ndo maana walilazimisha waajiri wachangie 10%.
Sasa uko tayari hyo 10% ya mwaajiri ambayo syo haki yako ktk emolument yako uikose kwa aidha kurejeshewa mwajiri au serikali izichukue na wewe ubaki na 10% uliyochangia?

Lets say nina umri wa miaka 35, nimefanya kazi katika kampuni ya kigeni - kampuni imefungwa wanaondoka wanarudi makwao. Fao langu kwa miaka 7 niliyofanya nao kazi ni zaidi ya 45m. Serikali inaniambia ati nitafute kazi nyingine ili niendelee kuchangia.....nimetafuta kazi mwaka wa pili sasa sijapata naishi kwa kuombaomba... chakula shida, pa kulala ni shida - Nahangaika hivi wakati nina 45m zipo NSSF - Je hii ni HAKI.

FAO la kujitoa HOJA nzito mno ....wafanyakazi tuchague chama kinachokuja na SERA bora hasa kwenye FAO hili.
 
Back
Top Bottom