pilipili kichaa
JF-Expert Member
- Sep 3, 2013
- 19,030
- 15,232
Wakuu hizi fedha zinatumika ktk matumizi mengine ndugu. ndio maana mafao yako ya hovyo sana na hayana tija kwa mstaafu
Niliachishwa kazi Ila ni miezi kadhaa sasa sijapata ela yangu kutoka mfuko na fomu nilijaza mda sana .Je nichukue hatua gani? Mana nimechoka kufuatilia au nipate direct contact ya muheshimiwa ndo watanipa.Kinacho zungmziwa cha 2023 ni kikokotoo cha zamani kuendelea kutumika, kikokotoo sio fao la kujitoa kikokotoo ni kwa ajili ya mtu anaepata malipo ya mkupuo na anastahili pensheni. Fao la kujitoa sasa ni kama hakuna kwasababu ni wenye ajira za mkataba tu na wageni ndo wanapewa fao la kujitoa wengine wote utapewa fao la kukosa kazi tena lazima umeachiswa kazi sio wewe kuacha. Kujibu swali lako kama ajira yako ni ya mktaba utapewa fao la kujitoa na hapo lazima mkataba uwe umesitiswa na muajiri sio umeacha kazi makusudi.
1 - Tangu Rais aseme wafanyakazi wapate FAO LA KUJITOA, bado hii haki kupatikana..Sekta binafsi ni kilio kila uchao, NSSF wameshindikana na waziri jenister mhagama ni kama ameipotezea kauli ya Rais ya kuifuta sheria mpya hadi 2023- Kwa nini wizara isipeleke marekebisho bungeni kufuta sheria kandamizi? ---Serikali Ya Kibeberu kukandamiza wanyonge.
2.Yaani wafanyakazi sekta binafsi wanafanya kazi katika mazingira magumu sana, bado mshahara ni kdg sana...halafu na kupoteza kazi ni any time....Bado Mabeberu wanakaba na kale ka Akiba
Halipo na 55yrs hujitoi, bali unastaafu.Habari wakuu
Naomba msaada mwenye kujua kama fao la kujitoa nssf lipo au ndo mpaka unitimize miaka 55....
Mtaani kugumu kama lipo tukachukue hizo hela tufanye hata biashara.
Rais hajafuta kikokotoo kipya, bali amesitisha kisitumike mpaka mwezi wa tatu mwakani.Naona kila mwana CCM analikwepa suala la FAO LA kujitoa kama vile ni Jambo dogo. Bwana Humprey Polepole ameongea na waandishi wa habari Mara 2..hii hoja ameiruka.
Mtu amefukuzwa kazi au mkataba umeisha, NSSF (Fao la kukosa Ajira) wanasema ulipwe 33.3 % ya Mshahara kwa miezi 6...baada ya hapo kaa miezi 18 ...ndio ulipwe.
Sheria mpya ya 2018, Raisi Magufuli alisaini, lakini baadae akaja kufuta kikokotoo cha wastaafu pekee...Sasa wafanyakazi wanaofukuzwa kazi sekta binafsi kabla ya umri wa kustaafu wanataabika. Wenye kuona hili wamshauri Magufuli haraka sana na arekebishe maana Katiba imempa mamlaka.
Raisi Magufuli, rudisha FAO LA kujitoaa. watu walipwe pesa zao kwa mkupuo bila masharti ... Hiki ni kipindi cha Kampeni...Kura za Wafanyakazi sekta binafsi ni mamilioni...
Ndugu Bashiru na Pole pole...FAO LA Kujitoa..
Rais hajafuta kikokotoo kipya, bali amesitisha kisitumike mpaka mwezi wa tatu mwakani.