NSSF: Kurudishiwa michango ya uanachama/withdraw benefit

NSSF: Kurudishiwa michango ya uanachama/withdraw benefit

HIZO TARATIBU KILA MTU ANAZO PALE ANAPOENDA KUDAI MAFAO YAKE.

KERO KUBWA NI KWA NINI LONGO LONGO ZIWE KIBAO?

NINGALIFURAHI KAMA UNGEWEKA BAYANA KUWA WENYE KUJITOA WANAPATA HELA ZAO HATA BAADA YA SIKU 3 NA SIO VINGINEVYO.
 
Mizengwe bado ipo, ukienda unapewa fomu unajaza na unapewa barua ya kufungua madai kisha unaambiwa utapigiwa simu uende kwa ajili ya kujaza fomu za madai usubiri kupigiwa tena simu ukachukue cheque
Hii info ya muda Kitambo enzi zile, inatakiwa current ambayo official
 
Afadhari sasa, nadhani na siye wa sekta binafsi huku kunaweza kua na utulivu sasa; ukweli sielewagi kabisa kwanini SSRA wanao ishi kwa fadhila za hiyo mifuko ya jamii wanatupa shida sana wafanyakazi; wafanyakazi hatuna mkataba na SSRA, tuna mkataba na mifuko ya jamii kama NSSF, PPF, PSPF nk. Binafsi sioni umuhimu wowote wa shirika hilo, lipo kwa ajili ya kutengeneza matumizi tu na sio ku generate pesa. Nipo tayari kukosolewa kwa hilo, na ningekutana na mhe rais kwangu mimi hilo ndio lingekua wazo langu la kwanza kumpa. Hakuna mantiki yoyote ya kuanzisha shirika linalo tafuna tu pesa kwa TIJA ambayo wala haipo.
 
Halijawahi kufutwa ila walibadili utaratibu ule wa mwanzo ilikuwa ikitolewa ndani ya mwezi tu tangu kuacha Kazi ila sasa wamerudisha utaratibu wa mwanzo wa miezi 6 kusubiri.

Kwanini usubiri miezi 6.

Wanaoweka huu utaratibu ni watu gani hasa?

Hii nchi inatia hasira sana.
 
Lilifutwa na badala yake likawekwa fao la bima ya afya

Bima ya afya gani? NSSF ni kama wanatapeli wanachama wao. Nimekuwa karibu na wanachama wao na hata nimebahatika kuona kwa karibu suala lao la Bima za Afya. Ni utapeli mkubwa tu. Wamechagua vijihospitali vya chini chini visivyokuwa na huduma za kiwango cha juu. Hii ni kukwepa gharama. Bima ya afya NSSF ni janga ndugu zangu. Mkitegemea hiyo bima mtapoteza maisha.
 
Kwanini usubiri miezi 6.

Wanaoweka huu utaratibu ni watu gani hasa?

Hii nchi inatia hasira sana.

Serikali ina influence kubwa sana kwenye hii mifuko.

Na ndio inayofanya inavyotaka yenyewe juu ya hii mifuko.

Hela zetu zimewekezwa kila kona ila return kwa sisi ambao ndio tuna Capital hakuna.

Tumefanywa mabwege na hela ni zetu.
 
Hawa NSSF washatengeneza uasi kwenye mioyo ya wanachama na familia zao..
Ni suala la muda tu
 
Back
Top Bottom