Lole Gwakisa
JF-Expert Member
- Nov 5, 2008
- 4,734
- 2,265
Jana tumeshudia serikali ikisalimu amri kuwa itarudisha sheria gereji ili ifanyiwe marekebisho na kuafiki na kilio cha wachngiaji wamifuko ya hifadhi ya jamii juu ya fao la kujitoa. Nimeona tena nguvu ya umma ikishinda. Wachangiaji bila kujali itikadi, dini wadhifa na tofauti nyingine walijitokeza kupinga sheria hii na mwisho tumeshinda mpaka hatua hii na tunaamini hii ni mpaka watakaporidhia kufanya marekebisho tunayaoyataka.
Kumbe tukiamua tunaweza japo wako waliokosoa uelewa wetu wa dhana ya mifuko ya hifadhi ya jamii - tunawasamehe tunajua walikuwa wanaganga njaa kwa kutetea kila kilichopita kama sheria hata baada ya kuona hakifai. Tujifunze katika hili wenye sheria ni sisi na zipo kwa ajili yetu na siyo sisi kwa ajili ya sheria
Nawasilisha
Hata hivyo nimepata hii humuhu JF,sijui Zoma yuko wapi?