Wafanyakazi wote wa KIRIBO LTD mafao yetu hayaonekani kwa miaka 4, NSSF mlikuwa wapi?

mkurya org.

JF-Expert Member
Sep 25, 2014
1,571
1,691
Wanajukwaa poleni Sana na Majukumu,

Mimi hapa ni miongoni mwa wafanyakazi wa kampuni ya Kiribo Ltd iliyopo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara.

Kwa taarifa rasmi kuhusiana na kampuni yetu tulisimama kazi tangia mwaka Jana mwezi wa saba ila tangia tulivyosimama kazi hatujawahi pewa haki zetu au malipo yetu yoyote Yale yanayohusiana na malipo ya wafanyakazi Kama Sheria ya wafanyakazi inavyosema.

Tumepita ngazi zote zinazohusika Kama vile kwa mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa na hata kwa Naibu waziri wa kazi mh.Katambi alishataarifiwa ila bado hatujapewa mrejesho wowote kuhusiana na Jambo hili.

Na kwa upande wa NSSF tulivyosimamishwa kazi Kuna baadhi yetu tulienda kuangalia salio tukapewa statement zetu.

Kuangalia Tukakuta ndani ya miaka minne yote tuliyofanya kazi kampuni ya Kiribo Ltd mwajili wetu hajawahi weka Ela yoyote zaidi ya mwezi mmoja tu kama statement inavyoonesha hapo chini na wengine hawana kabisa pesa yoyote kwenye account zao.

Na tulivyowauliza kwann hamna salio kwenye account zetu na huku Sheria inawataka wao ndo waweze kufatilia Mafao yetu hawakuwa na majibu yoyote tuliyopewa zaidi ya kutuambia sisi ndo turudi kwa mwajiri tukamweleze na tukirudi kwa mwajiri wetu hataki kutupatia Barua zetu za kuachishwa kazi.

NSSF shida ipo wapi mbona kampuni zingine zinachangia michango ya wafanyakazi wao vizuri na kwann hii kampuni ya Kiribo kwa miaka yote minne wafanyakazi hawana pesa zao kwenye account?

Hii hapa chini ndo account statement yangu niliyopewa na wafanyakazi karibia wote ipo hivyo na wengine hawajawahi wekewa hata huo mwezi mmoja.

IMG_20210425_141849.jpg
 
Back
Top Bottom