Novel writer gani ni best kwako?

Jack & Jill - James Patterson

Sidney Sheldon

If Tomorrow Comes

Nothing Lasts Forever

Tell Me Your Dreams
The Other Side of Midnight

na wengine wengi
 
Nawakumbuka sana waandishi hao na nawashukuru sana wazazi wangu hasa Mama angu kwa kunijengea utamaduni wa kupenda kusoma vitabu tangu nikiwa mdogo na hapa nitaorodhesha novels zote nilizosoma ninazoweza kuzikumbuka ili waJF muijue hazina hiyo na kwa wale waliosahau na ambao hawajasoma watafute.Riwaya za Tanzania nyingine nilizisoma katika magazeti na majarida hakuna toleo lililonipita.Vile vile namshukuru rafiki yangu mmoja alinisaidia pia katka kuvipata na kuvisoma anaitwa MOPAO.

ARISTABLIS ELVIS MUSIBA(MAREHEMU)

1.KIKOMO-

Willy Gamba alitumwa kufuatilia wizi mkubwa na wa kushangaza wa almasi uliokuwa ukifanyika Mwadui.Safari yake ilimpitisha Shinyanga,Maganzo, Mwanza,humu utakutana na Chifu,Maselina,ELUNGATA,PWEKE,TAUSI,Makungu Majula na wahusika wengine wengi.Ni riwaya tamu sana ambae hajaisoma aitafute.
2.KUFA NA KUPONA-
Willy Gamba anafanya kazi inayompeleka mpaka Nairobi Kenya.Lengo kuu ni kupambana kulinda usalama wa taifa la Tanzania.
3.NJAMA-
Willy Gamba anakwenda Sierra Leone huko anakutana na mrembo VERONICA AMADA na wapelelezi wengine.Meli yenye shehena ya silaha za wapigania uhuru kusini mwa Afrika katika bandari ya Dar es Salaam inaibiwa shehena yote.Kazi ilikuwa ngumu Willy anamwokoa binti aitwae BINTI TANZANIA,vile vile alifanikiwa kuwawezesha wapigania uhuru kuzipata silaha zao.
4.KIKOSI CHA KISASI-
Riwaya hii inahusiana na mtandao wa BOSS wa makaburu wa Afrika Kusini kama JEAN mwenye GAD garage,PAPA mwenye Gereji PAPADIMITROU,MUTEBA mwenye gereji BANINGA na wengine waliokuwa wamejikita Kinshasa Zaire (Congo DRC) wakifanya kazi maalumu ya kuwaua wapiganiaji uhuru.Utakutana na wapelelezi akina KOFI,OZU,ROBERT.Utasikia hotel za Memling,Continental na ziwa Nsele.Humo kuna akina MWADI ,TETE,MAX.Ni riwaya tamu mwanzo hadi mwisho ikipitia Tanzania,Zambia na Zaire.
BEN RAMADHAN MTOBWA(MAREHEMU)
1.DAR ES SALAAM USIKU-
Rukia msichana mrembo na maisha yake ya kiajabu ajabu katika jiji la Dar es Salaam.
2.PESA ZAKO ZINANUKA
3.NAJISIKIA KUUA TENA
4.TUTARUDI NA ROHO ZETU?-
Joram Kiango alitumwa Afrika Kusini kupambana na majahili waliotaka kuilipua Afrika kwa kutumia satellite.Alikuwa bega kwa bega na mrembo NURU.
5.SALAMU KUTOKA KUZIMU-
Joram na Nuru tena ikiwa ni mwendelezo wa Tutarudi na Roho Zetu.
6.ROHO YA PAKA-
Inspekta KOMBORA alitumiwa ujumbe wa hatari pamoja na mzoga wa paka,kisome uone Joram Kiango alivyofanikiwa kuwazidi akili mtandao wa maadui wa taifa wakiongozwa na jamaa wawili vituko.
7.ZAWADI YA USHINDI
Riwaya nzuri iliyowahi kuchaguliwa kujibia mtihani wa Kiswahili kidato cha nne kwa miaka kadhaa.Ni hadithi ya SIKAMONA aliyeenda kupigana vita vya Kagera kumng’oa nduli Iddi Amini Dada wa Uganda.
ZAINABU K. MWANGA
1. KIU YA HAKI-
Mzee Toboa Siri alipenda siku zote haki zitendeke na sheria ichukue mkondo wake,kisome uone masahibu makubwa yaliyomkuta.Kilitumiwa kujibia mitihani ya taifa ya Kiswahili nchini Tanzania.
2. HIBA YA WIVU-
Riwaya nzuri ya mapenzi na tamaa katika ndoa yenye matukio ya kusisimua.Kilitumiwa kwenye mitihani pia.
3. WIVU WA MUMEO-
Mwendelezo wa riwaya ya Hiba ya Wivu ambapo katika hii IHUCHA anamkosea mkewe.

EDDIE GANZEL(MAREHEMU)
MWANDISHI HUYU NDIO NAMBA MOJA YANGU KWA TANZANIA (JAMES HADLEY CHASE WA TANZANIA) ALIKUWA AKITUMIA AKILI NYINGI NA STAILI KALI ZA MANENO NA UTUNZI KATIKA RIWAYA ZAKE.ALIFARIKI MOROGORO .
1. KISIWA CHA SILKI
Ni riwaya ya miaka ya 70 ambayo inahusu ugonjwa, mwandishi alitunga na ikaonekana kama aliutabiri ugonjwa wa UKIMWI.
2. MAUAJI YA KISHENZI-
Inspekta wa polisi alimchukua msichana akaenda nae kwake, kabla hawajafanya chochote alipigiwa simu kituoni kwake akaenda kuwapa silaha askari.Aliporudi kwake alikuta binti ameuawa,alichanganyikiwa akaamua kutuliza akili ili ajiokoe.Alichukua Landrover ya Polisi na kwenda kuutupa mwili katika uwanja wa mpira usiku ule ule mvua ikiwa inanyesha ili apate muda wa kutosha kufanya upelelezi ili ajinasue.Mwishoe kwa shida huku akiwa amekata tamaa aligundua bosi wake alifanya mauaji yale.Ni riwaya nzuri ya mtindo kama wa JAMES HADLEY CHASE.
3. MSAKO WA HAYAWANI-
Komando DENNIS MAKETE anamtafuta hayawani aliyejaribu kumuua Baba aliyemlea Daktari MAKETE.Muuaji ni KASSIM HASHIR baba ake mzazi Dennis.Utakutana na mrembo Inspekta BESSY.
4. ZUBAA UZIKWE-ILICHAPISHWA KATIKA MAJARIDA KADHAA YA BONGO chini ya SABBI MASANJA mchoraji FORTUNATUS NDILLA
Majambazi wanne CHENJE na wenzie waliiba wakakamatwa watatu tu yule wa nne aliponea uraiani.Aliyebaki alijenga hotel kubwa na nzuri ya ZE BAMBUSH,wenzie walikuwa karibu kuachiwa na walitaka wagawane zile mali sawa bin haki.Soma riwaya hii ufaidi simulizi nzuri tena za kufikirisha za marehemu Eddie Ganzel.
5.ZAWADI YA *****-
Tajiri mwenye asili ya kiasia tena kiongozi alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi mrembo LIZA.Liza alipata mimba akauawa kwa hila na jamaa aliyetumwa na tajiri yule ili atoe mimba kumbe alipewa sumu.Kaka ake Inspekta aliyesomea Marekani aliahidi kufanya juu na chini kuwapata wauaji,akawa anatishiwa kupewa zawadi ya ***** iliyochongwa kwa mbao za mti wa mninga yaani JENEZA.Mheshiwa Premji alikiri na mwishowe alikufa.Humu utamkuta SHANGAZI mmiliki wa gesti au kijiwe cha MKUNGUNI.Vile vile binti wa kiarabu RAHMA aliyemshawishi Liza kuwa na mahusiano na Waziri kwa juhudi nyingi hadi akafanikiwa.
6.MSAKO WA MR. X-
Riwaya nzuri kuhusu mfungwa aliyetaka kutoroka jela,nje matajiri watatu waliwekeana dau kama kijana yule atatoroka ulinzi mkali wa askari ambao uliongezwa maradufu siku ya kupelekwa mahakamani kwenye kesi yake na siku hiyo hiyo ndiyo aliyoahidi kutoroka.Mr. X ni Lord wa madawa ya kulevya asiyejulikana hata kwa anaowatuma kupeleka mihadarati hiyo sokoni,huwa amebadili sura na sauti na hutoa mzigo baharini kenye kisiwa.Mbinu ilifanywa na Polisi kumtoa selo kipenzi cha Mr. X ili aweze kupatikana.Ajabu yake ni kuwa kati ya wale wafanyabiashara watatu ambaye huwezi kudhania mmoja wao ndiye Mr. X!!
7. DUNIA GUNIA-
Riwaya yake ya mwisho kabla ya kifo cha Eddie,ni kisa cha msichana aliyetoroka kwao akajikuta ameolewa na mtoto wa tajiri.Utata mkubwa ulitokea,tafuta riwaya hii ufaidi zaidi.

8.KWA MUNGU MBALI-NA REY GANZEL (BINTI WA EDDIE GANZEL)
Binti alikuwa bwawani akiogelea na mchumba wake,huko mchumba wake aliuawa na yeye kubakwa na vijana watatu.Alipopona aliona hukumu hiyo kutolewa na Mungu itakuwa mbali.Alilipiza kisasi kwa kuua mwanaume mmoja baada ya mwingine katika mashindano ya piki piki,na mazingira mengine bila kuacha clues zozote.Ni riwaya kali pia.

HAMMIE RAJABU(MAREHEMU)
1. SITAKI BADO SIJAVUNJA UNGO-
2. UKIMWONA MMALIZE-
Malik jambazi aliyekubuhu jijini Dar anapigwa risasi ya bega akiruka korongoni baada ya kusumbua sana wananchi jijini.
3. SANDA YA JAMBAZI-
Mwendelezo wa hadithi ya Malik alivyojikokota akafika kwa wakulima Baba KWEMBE na Mama Kwembe akamteka dereva wa Lori akaelekea Morogoro.Jambazi haachi ujambazi aliendelea.Mwishowe Inspekta SINDI alimchana risasi za kifua akaanguka kama puto lililopasuliwa.
4. ROHO MKONONI-
Mpelelezi wa Tanzania RAY SIBANDA alitumwa Nairobi Kenya kumtafuta mwanajeshi wa Tanzania aliyelazwa kwenye hospitali ya vichaa.Luteni yule alikuwa anajua siri ya mahali zilipo karatasi za siri kuu ambazo Iddi Amini pia alizihitaji.Katika mission hiyo anakutana na IDA YMANA binti mpelelezi kutoka Msumbiji na AL QUADIR mpelelezi kutoka Libya.Ni riwaya kali yenye ujanja mwingi na mbinu za kipekee.
5. KAMLETE AKIBISHA MLIPUE-
Ray Sibanda anatumwa nchini Nigeria kumtafuta mwanajeshi muasi aliyejaribu kupindua serikali ya Rais JK NYERERE.Mhaini huyo alikimbia akajichimbia Nigeria Ray alifika na kumlazimisha kurudi alipogoma ilibidi amlipue kama amri ilivyosema.
JOHN MSIMBE SIMBAMWENE (JOMMSI Publications)MWANDISHI HUYU ANA VITABU VINGI KULIKO WOTE VINAFIKA 36.WAHUSIKA WAKUU NI INSPEKTA FOG,SAJENTI SEFU,BAADHI YAKE NAVYOKUMBUKA NI VIFUATAVYO
1.FUNGUO ZA SIRI ZIMEIBIWA-Mama anayekula sana na muda wote MAMA KIZITO anamwibia Profesa Baraka aliyegundua dawa ya UKIMWI funguo zenye sefu lenye kanuni ya utengenezaji wa dawa hiyo
2 . MADHAMBI YA MWENYE NYUMBA.
3.OPERESHENI SUKUMA NAMBA NANE
4.ORODHA YA WATAKAOUAWA.
5.MAUAJI LOJINGI.
FARAJI H. KATALAMBULA (MAREHEMU)ALIMILIKI JARIDA LA MAPICHA LA PILI PILI PILI.
1.SIMU YA KIFO
SALUMU ABDULLA (MAREHEMU ) MTUNZI WA KUTOKEA ZANZIBAR.RIWAYA ZA KISHERLOCK HOLMES.WAHUSIKA WAKUU SPEKTA MUSSA NA RAFIKIE NAJUM.VILITUMIWA SANA KWENYE MITIHANI YA KISWAHILI MIAKA YA 1960 NA 1970.SITAVICHAMBUA MPAKA SIKU INGINE.
1.MZIMU WA WATU WA KALE.
2.DUNIANI KUNA WATU.
3.KISIMA CHA GININGI
4.SIRI YA SIFURI
Wana JF nawapenda sana orodha zaidi katika riwaya za Kiswahili na Kiingereza kama akina AGATHA CHRISTIE,CHARLES DICKENS,WILLIAM SHAKESPEARE na RENE BRABAZON yaani JAMES HADLEY CHASE mpaka siku ingine.










 
Jack & Jill - James Patterson

Sidney Sheldon

If Tomorrow Comes

Nothing Lasts Forever

Tell Me Your Dreams
The Other Side of Midnight

na wengine wengi
Dah kama umesoma the other side of the midnight tafuta muendelezo wake kwenye memories of the midnight huko the saga continues
 
ingekuwa vizuri kwa wale wenye soft copy ya novel yoyote wanayoitaja wakaiatacha ila na sisi tupate burudani ya hizo novel.
Mi nampenda beny carsol nimesoma kazi zake za gifted hand, think big, the big picture na take risk
 
Nilikuwa na soft copy ya novel za hawa watu, ila sijui nimeziweka wapi ntazitafuta niziweke hapa ili wanaozihitaji wazinyonye
  1. Sidney Sheldon
  2. Robert Ludlum
  3. Stephen King
  4. Fredrick Forsthy
  5. John Grisham
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom