Nôtre dame de Paris inateketea kwa moto

Inauma kwa kweli kuona historia inateketea hivi
Nakumbuka tukio kama hili nilikuwa London wakati Windsor castle linawaka moto, lakini bahati halikuteketea lote na walitengeneza upya na sasa lipo kama zamani
Ila hili kanisa ndio kwaheri
Naona viongozi wengi duniani wana tweet
Na wenye uoendo na historia

Lakini ninapoona heritage site zinaharibika hivi kama daesh walivyovunja sites za makumbusho huko Syria na Iraq duuu inauma kwa kweli
Kila nikakotembelea dunia ni lazima niende kwenye majengo ya kihistoria
So sad

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
Acha lijiungulie zake tu, kwani unadhani halina akili? Limeshaona kuwa limegeuzwa kituko cha kutembelewa kama Makumbusho ya kihistoria huku waumini wakizidi kupungua kwa kasi ya ajabu. So limeamua kujipiga kibiriti tu.
 
Unaacha kulilia ndugu zako albino wanachinjwa huku Bongo,watoto wanatekwa na kuuwawa huko njombe unakuja kulilia jengo wa wafaransa,ajabu sana.


Sent from my iPhone using JamiiForums
Ni swala la kuchagua tu, siyo la kufundushana au la kulazimishana. Yeye kachagua cha kukililia hao wabongo walilie wewe.
 
As a Christian nililia lile kanisa ni muhimu sana kiimani kwa sisi wakristo.Taji ya miiba aliyovalishwa Yesu imehifadhiwa hapo,kipande cha msalaba alosulubiwa Yesu kimehifadhiwa hapo,Jiwe lililotoka mahali aliposulubiwa Yesu limehifadhiwa hapo.
Kwa iyo vyote vimeungua ?
 
Usisemee wakristo wote lina historia yenu wakatoliki tu siyo wakristo wote
Mimi siyo mkatoliki. Lile kanisa lilikuwa linagifadhi taji ya miiba alovishwa Yesu,msumari mmoja ulotoka kwenye msalaba wa Yesu. Kipande kilichotoka kwenye msalaba wa Yesu Sisi wakristo tunaamini Yesu. Vitu vilivyokuwa kwenye hilo hekalu ni muhimu sana katika imani Yetu ya Ukristo.
 
So far almost $1 billion has been pledged by billionaires and every day people to rebuild that beautiful church which also use to attract 13 millions tourists each year.

April 15, 2019
Paris, France

Historia ya Notre-Dame Cathedral na umuhimu wake katika historia ya taifa la Ufaransa

Muonekano wa Kanisa Kuu wa Notre-Dame jijini Paris, France linalohusishwa na Bikira Mariamu lilianza kujengwa mwaka 1163 AD baada ya jiwe la msingi kuwekwa na Pope Alexander III . Maana ya Notre-Dame ni Our Lady katika Kiswahili twaweza sema 'Mama Yetu' na ni utamaduni waWafaransa kufananisha jengo la kanisa kubwa kwa mahaba makubwa kama Mama Yetu . Ujenzi wa Notre-Dame ulimalizika 1345 A.D hivyo kuchukua miaka 180 kukamilisha mradi huu pekee wa jengo maarufu la kanisa la Notre-Dame.

Kuna Kengele kadhaa lakini ile kubwa kabisa yenye uzito wa tani 13 iliyopewa jina Emmanuel ambayo hutumika maalum wakati wa sikukuu kubwa za Pasaka, Christmas na hafla zingine kubwa . Kengele zingine ndogo tano husikika kuashiria muda wa saa kila siku katika jiji la Paris. Kanisa hili limeshehene kazi maarufu na za ustadi mkubwa wa Sanaa ya uchoroaji zikielezea hadithi na historia mbalimbali za kiimani.

Kuna sanamu mbalimbali zilizowekwa nje ya jengo la kanisa la Notre-Dame zikiashiria masuala mbalimbali ikiwemo kulilinda kanisa hilo na mabalaa mbalimbali ya kishetani. Kuna sanamu ya Charles The Great kuashiria mchango wake kwa Kanisa katika bara la ulaya, picha za Napolean Bonaparte akitawazwa na za mtiririko wa picha adhimu kuhusu matukio na historia ya Ufaransa na Kanisa. Kuna alama ya Point Zero ikimaanisha hapo ndipo kitovu cha katikati ya jiji la Paris likionesha kilomita sifuri (Kilometre zero Paris 48°51′12″N 2°20′56″E ).

Point Zero mbele ya Kanisa la Notre-Dame ndipo ramani na kiashiria cha mpango mjni ya jiji la Paris Ufaransa karne nyingi zilizopita kabla ya teknolojia ya GPS na satellite kuanzishwa. Hivyo tuauona umuhimu wa jengo hili kwa Wafaransakatika masuala ya Imani, utamaduni, kuenzi chao na utalii kwa ujumla. Kanisa hili limekuwa alama muhimu iliyosimama kwa miaka zaidi ya 850 kuelezea historia ya Ufaransa na pia jiji la Paris na aina ya ujenzi-wa-kuigwa katika cathedral zilizotapaka nchini Ufaransa za Amiens,Chartres na Rheims.

 
Mimi siyo mkatoliki. Lile kanisa lilikuwa linagifadhi taji ya miiba alovishwa Yesu,msumari mmoja ulotoka kwenye msalaba wa Yesu. Kipande kilichotoka kwenye msalaba wa Yesu Sisi wakristo tunaamini Yesu. Vitu vilivyokuwa kwenye hilo hekalu ni muhimu sana katika imani Yetu ya Ukristo.
Vinasaidia nini hivyo vitu katka ukristo wako?
 
Majengo meng huko mbeleni yana damu za mababu zetu, je hilo jengo lililoungua halina chembechembe hizo? Unaweza kukuta ndio malipo yenyewe hayo.
 
So far almost $1 billion has been pledged by billionaires and every day people to rebuild that beautiful church which also use to attract 13 millions tourists each year.
Umeahidi kiasi gani bilionea wanguuu... miss u
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom