NYENJENKURU
JF-Expert Member
- Feb 11, 2011
- 1,063
- 288
Lakini gharama kwa serikali si zinazidi kuongezeka?AU..Simeulewi JK
Sasa menejimenti ifanyeje watoto wazuri wanazidi kumaliza vyuo na hakuna pa kuwapachika. Refer Ukuu wa wilaya ManyyoniKuna watu wanaandaliwa ukuu wa wilaya na ukuu wa mkoa kulipa fadhila
<br />Hongera jk, wacha wapinzani wa maendeleo waseme au wabeze, kusogeza mamlaka jirani zaidi na wananchi ni muhimu sana. Hata hivyo tangu lini? Wapinzani wakapongeza kazi ya serikali iliopo itakuwa ajabu.
Lol! Sikujua, na Iringa je?Morogoro na Mbeya ni Mikoa Mikubwa sana... naona hawawezi kuigawanya sababu ya Ardhi wamegawana hao wakubwa wa CCM
Wanaimaliza Mwanza sababu ya Upinzani, Wanaigawa gawa - vipi Majimbo yamekufa kabisa?
Mkuu unataka kusema zitakuwa zimepunguwa maana kwa sasa idadi hiyo imeshavuka sanaDu hii mikoa mingine,mfano kamkoa ka Pinda kana wilaya mbili tu,haiingii akilini,kupoteza hela ya walipa kodi kwa ajili ya kuanzisha mkoa wenye wilaya 2 tu heti tu kwasababu waziri mkuu anatoka mkoa huo,huo ni utumiaji mbaya wa madaraka,kama kila atakaye pata uwaziri mkuu atataka tarafa yake iwe wilaya na wilaya yake iwe mkoa ili wapate fungu kubwa basi kufikia 2050 Tanzania itakuwa na wilaya kama 130
Du hii mikoa mingine,mfano kamkoa ka Pinda kana wilaya mbili tu,haiingii akilini,kupoteza hela ya walipa kodi kwa ajili ya kuanzisha mkoa wenye wilaya 2 tu heti tu kwasababu waziri mkuu anatoka mkoa huo,huo ni utumiaji mbaya wa madaraka,kama kila atakaye pata uwaziri mkuu atataka tarafa yake iwe wilaya na wilaya yake iwe mkoa ili wapate fungu kubwa basi kufikia 2050 Tanzania itakuwa na wilaya kama 130
Hapo sasa mkuu wangu na sidhani kama kuna kiongozi wetu yeyote anafahamu kwa nini Italy wamefanya hivyo!Tanzania raha sana. Wakati Italy, moja kati ya nchi nane tajiri zaidi ulimwenguni inapunguza mikoa, wilaya na mabaraza ya miji ili kupunguza matumizi, [Gonga hapa: The adjustment plan Italian provinces and municipalities deleted to fit the budgets of 2013 | Economics Newspaper], Tanzania ambayo inaingia katika nchi kumi masikini zaidi duniani, ndio kwana inaongeza utitiri wa wilaya na mikoa ili kuongeza matumizi. Moyo unaniuma sana.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
TAARIFA KWA UMMA
NOTISI YA KUANZISHA MIKOA NA WILAYARais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mamlaka aliyopewa chini ya Ibara ya 2(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria au kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.Katika kutekeleza Mamlaka hayo, Rais ametoa notisi ya kusudio la kuanzisha Mikoa minne (4) na Wilaya kumi na tisa (19). Notisi hizo ambazo zimetolewa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Uanzishaji wa Mikoa na Wilaya Sura 397 ya Toleo la 2002 ni Tangazo la Serikali Na. 285 la tarehe 9 Septemba, 2011 kwa ajili ya uanzishaji wa Mikoa na Tangazo la Serikali Na. 287 la tarehe 9 Septemba, 2011 kwa ajili ya uanzishaji wa Wilaya.Madhumuni ya Notisi hizi ni kuzialika Taasisi na mtu mwingine yeyote ambaye ataathirika na uanzishaji huo kutoa maoni, mapendekezo au pingamizi iwapo yatakuwepo katika kipindi cha siku 21 kwa Mikoa mipya na siku 30 kwa Wilaya mpya kuanzia tarehe ya Notisi hizi.Baada ya muda uliowekwa kupita, Rais atachambua maoni, mapendekezo na pingamizi zilizotolewa na kuzitolea uamuzi kabla ya kuanzisha rasmi Mikoa na Wilaya hizo kwa kadri atakavyoona inafaa.Mikoa mipya inayoanzishwa na Makao Makuu yake ni kama ifuatavyo: -
MKOA WILAYA ZAKE MKOA ZINAKOTOKA MAKAO MAKUU 1. Geita Geita Mwanza Geita Nyang'hwale(Mpya) Mwanza Chato Kagera Bukombe Shinyanga Mpya/Mbogwe Shinyanga 2. Simiyu Bariadi Shinyanga Bariadi Itilima (Mpya) Shinyanga Maswa Shinyanga Meatu Shinyanga Busega (Mpya) Mwanza 3. Njombe Njombe Iringa Njombe Wanging'ombe(Mpya) Iringa Ludewa Iringa Makete Iringa 4. Katavi Mpanda Rukwa Mpanda Mlele(Mpya) Rukwa
Wilaya mpya zinazoanzishwa na Makao Makuu yake ni kama ifuatavyo: -
WILAYA MPYA WILAYA MAMA MKOA MAKAO MAKUU 1. Buhigwe Kasulu Kigoma Buhigwe 2. Busega Magu Mwanza Igalukilo 3. Butiama Musoma Mara Nyamisisi 4. Chemba Kondoa Dodoma Chemba 5. Gairo Kilosa Morogoro Gairo 6. Ikungi Singida Singida Ikungi 7. Itilima Bariadi Shinyanga Itilima 8. Kakonko Kibondo Kigoma Kakonko 9. Kalambo Sumbwanga Rukwa Kalambo 10. Kaliua Urambo Tabora Kalua 11. Kyerwa Karagwe Kagera Rubwera 12. Mbogwe Bukombe Shinyanga Mbogwe 13. Mkalama Iramba Singida Nduguti 14. Mlele Mpanda Rukwa Inyonga 15. Momba Mbozi Mbeya Ndalambo 16 Nyang'hwale Geita Mwanza Nyang'hwale 17. Nyasa Mbinga Ruvuma Mbamba Bay 18. Uvinza Kigoma Kigoma Lugufu 19. Wanging'ombe Njombe Iringa Waging'ombe
Kwa taarifa hii, Wananchi wote wanaalikwa kutumia haki yao ya kisheria kutoa kwa maandishi maoni, mapendekezo na pingamizi kama zipo kwa kuzingatia utaratibu uliwekwa kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi wa maeneo husika na maslahi ya Taifa kwa ujumla. Maoni, pingamizi au mapendekezo hayo yatumwe kwa kutumia anuani ifuatayo: -
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
S. L. P 1923,
DODOMA.
E-mail hakattanga@yahoo.com
Fax- 026-2322116
Imetolewa na: -
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
9 Septemba, 2011
*************************************************
Wakuu kwa kuangalia hali halisi ya uchumi wa Tanzania kwa sasa na jinsi Taifa letu linavyokabiliwa na matatizo mengi ya kiuchumi pamoja na kijamii; ni sahihi kwa wakati huu kuanzisha mikoa mipya na wilaya mpya tena kwa idadi kubwa kama hiyo (Mikoa MINNE na Wilaya KUMI NA TISA).
Lipi jambo la muhimu kwa sasa, kuanzisha wilaya na mikoa mipya ama kuangalia namna ya kutatua matatizo yanayolikabili Taifa kwa sasa?
Swali la kujiuliza, Mbona wakati wa utawala wa awamu ya kwanza hadi ya tatu Marais wa vipindi hivyo hawakuongeza mikoa na wilaya kwa idadi kubwa kama hiyo? Iweje wakati wa awamu ya JK ndiyo tunashuhudia kila kitu kikiongezwa kama Baraza la Mawaziri, Uteuzi wa majaji, na hata Mikoa pamoja na Wilaya Mpya.
Kwa wale wenye kuliona jambo hili na madhara yake naomba tupaze sauti kukemea na kulikataa mapema.
Source: PMORALG - Home -
4. | Katavi | Mpanda | Rukwa | Mpanda |
Mlele(Mpya) | Rukwa |