Notisi ya kuanzisha Mikoa na Wilaya

Wakuu wapya wa mikoa 4, wakuu wa wilaya 19. Mashangingi 23, Kujenga majengo mapya ya ofisi na nyumba za watumishi, n.k. jamani kulikoni? Ukiongezea na mawaziri wa wizara na mawaziri wadogo! Tutafika kweli. NAPING KWA NGUVU ZOTE.
<br />
<br />
Bila kusahau mashangingi ya ma RAC, RPC etc!
 
Zoezi limechelewa .lilipaswa kufanyika kabla ya uchaguzi mkuu mwaka jana.. Sababu gani?? Itafurahisha kusikia kutoka kwa kiranja wa tawala za mikoa!!!
 
cna tatzo na kuanzisaha wilaya na mikoa mipya ila nicjeckia kuwa, mkuu wilaya hana umeme oficn, au mara mkuu wilaya anakaa majengo ya shule ya kata nk.
 
Fadhila nyingi za kulipa....
Sijui ni vigezo gani vinatumika kugawa hizo wilaya! Ukiangalia wilaya inayoitwa SERENGETI mkoani Mara, attention yote inaelekezwa mbugani tu. Ni wilaya inayosifika kwa ajili ya utalii. Na hata baadhi ya wakuu wetu wa nchi wanakimbizana huko kujenga mahoteli. Lakini ukiangalia kata zote za Tarafa ya Ngoreme kwa mfano, ambayo inahesabiwa kuwa sehemu ya wilaya ya Serengeti utadhani haipo katika ramani ya Tanzania. Vijiji vingi vimesahauliwa na macho yote yanaelekezwa mbugani tu.

Ifike wakati sasa Eneo lote la Tarafa ya ngoreme na baadhi ya vijiji vya wilaya ya Musoma vijijini vinavyopakana na tarafa hii vipewe hadhi ya wilaya. Maisha ya watu huko yanasikitisha na kuhuzunisha. Na kwa sababu ya kusahaulika, vijana wengi wanakimbilia mijini. Na kila wakati wazo hili linapotolewa, utasikia wanasiasa wanasema kuwa wilaya ya Serengeti ni mbuga tupu na idadi ya watu ni ndogo. Iwapo kweli Serikali hii inawajali wananchi wote bila ubaguzi, iwafikirie upya wananchi wa maeneo ya mbali na mbuga na hasa wa tarafa ya Ngoreme na vijiji vilivyo kandokando yake!
 
Mie nilitegemea mdau utakuja na orodha ya wakuu wa mikoa wapya walioteuliwa maana tetesi zilizopo ni kwamba JK anatarajia kuwatangaza wateule hao wapya jioni ya leo!

Ni kweli ametangaza wakuu wa mikoa lakini ukiangalia kwa undani kilichofanyika ni kuongezea watu ulaji tu kwani haingii akilini mtu ni DC wa wilaya fulani wakati huo huo unamteua kuwa mkuu wa mkoa mwingine tena mbali na wilaya anayo simamia. Ama mtu ni mbunge wa kuteuliwa halafu unamwongezea na ukuu wa mkoa, hiii ni aibu kwa viongozi wetu kwani inaonekana dhahiri kuwa aidha hawajui wajibu wao kwa jamii ama nafasi hizo hazina umuhimu wowote kwa maendeleo ya Taifa. Mfano mkuu wa mkoa wa Lindi alikuwa anakaimu ukuu wa mkoa wa DSM kwa muda mrefu sana na haiingii akilini kuwa alikuwa anawezaje kufanya kazi katika mikoa hiyo miwili kwa wakati mmoja.

Kubwa katika hilo naona hajateua wakuu wa mikoa mipya iliyoanzishwa hivyo bado nafasi ipo ya kupaza sauti na kutoa maoni na hisia zetu.
 
jamhuri ya muungano wa tanzania
ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa
taarifa kwa umma


notisi ya kuanzisha mikoa na wilayarais wa jamhuri ya muungano wa tanzania kwa mamlaka aliyopewa chini ya ibara ya 2(2) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania anaweza kuigawa jamhuri ya muungano katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na bunge.katika kutekeleza mamlaka hayo, rais ametoa notisi ya kusudio la kuanzisha mikoa minne (4) na wilaya kumi na tisa (19). Notisi hizo ambazo zimetolewa chini ya kifungu cha 4 cha sheria ya uanzishaji wa mikoa na wilaya sura 397 ya toleo la 2002 ni tangazo la serikali na. 285 la tarehe 9 septemba, 2011 kwa ajili ya uanzishaji wa mikoa na tangazo la serikali na. 287 la tarehe 9 septemba, 2011 kwa ajili ya uanzishaji wa wilaya.madhumuni ya notisi hizi ni kuzialika taasisi na mtu mwingine yeyote ambaye ataathirika na uanzishaji huo kutoa maoni, mapendekezo au pingamizi iwapo yatakuwepo katika kipindi cha siku 21 kwa mikoa mipya na siku 30 kwa wilaya mpya kuanzia tarehe ya notisi hizi.baada ya muda uliowekwa kupita, rais atachambua maoni, mapendekezo na pingamizi zilizotolewa na kuzitolea uamuzi kabla ya kuanzisha rasmi mikoa na wilaya hizo kwa kadri atakavyoona inafaa.mikoa mipya inayoanzishwa na makao makuu yake ni kama ifuatavyo: -
mkoawilaya zakemkoa zinakotokamakao makuu
1.geitageitamwanzageita
nyang’hwale(mpya)mwanza
chatokagera
bukombeshinyanga
mpya/mbogweshinyanga
2.simiyubariadishinyangabariadi
itilima (mpya)shinyanga
maswashinyanga
meatushinyanga
busega (mpya)mwanza
3.njombenjombeiringanjombe
wanging’ombe(mpya)iringa
ludewairinga
makete iringa
4.katavimpandarukwampanda
mlele(mpya) rukwa


wilaya mpya zinazoanzishwa na makao makuu yake ni kama ifuatavyo: -
wilaya mpyawilaya mamamkoamakao makuu
1. buhigwekasulukigomabuhigwe
2. busegamagu mwanzaigalukilo
3. butiamamusomamaranyamisisi
4. chembakondoadodomachemba
5. gairokilosa morogorogairo
6. ikungisingidasingidaikungi
7. itilima bariadishinyangaitilima
8. kakonkokibondokigomakakonko
9. kalambosumbwangarukwakalambo
10. kaliuaurambotaborakalua
11. kyerwakaragwekagerarubwera
12. mbogwebukombeshinyangambogwe
13. mkalamairambasingidanduguti
14. mlelempanda rukwainyonga
15. mombambozimbeyandalambo
16nyang’hwalegeitamwanzanyang’hwale
17. nyasambinga ruvumambamba bay
18. uvinzakigomakigomalugufu
19. wanging’ombenjombeiringawaging’ombe


kwa taarifa hii, wananchi wote wanaalikwa kutumia haki yao ya kisheria kutoa kwa maandishi maoni, mapendekezo na pingamizi kama zipo kwa kuzingatia utaratibu uliwekwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa maeneo husika na maslahi ya taifa kwa ujumla. Maoni, pingamizi au mapendekezo hayo yatumwe kwa kutumia anuani ifuatayo: -
katibu mkuu,
ofisi ya waziri mkuu,
tawala za mikoa na serikali za mitaa,
s. L. P 1923,
dodoma.

e-mail hakattanga@yahoo.com
fax- 026-2322116
imetolewa na: -
katibu mkuu,
ofisi ya waziri mkuu,
tawala za mikoa na serikali za mitaa.


9 septemba, 2011

*************************************************
wakuu kwa kuangalia hali halisi ya uchumi wa tanzania kwa sasa na jinsi taifa letu linavyokabiliwa na matatizo mengi ya kiuchumi pamoja na kijamii; ni sahihi kwa wakati huu kuanzisha mikoa mipya na wilaya mpya tena kwa idadi kubwa kama hiyo (mikoa minne na wilaya kumi na tisa).

Lipi jambo la muhimu kwa sasa, kuanzisha wilaya na mikoa mipya ama kuangalia namna ya kutatua matatizo yanayolikabili taifa kwa sasa?

Swali la kujiuliza, mbona wakati wa utawala wa awamu ya kwanza hadi ya tatu marais wa vipindi hivyo hawakuongeza mikoa na wilaya kwa idadi kubwa kama hiyo? Iweje wakati wa awamu ya jk ndiyo tunashuhudia kila kitu kikiongezwa kama baraza la mawaziri, uteuzi wa majaji, na hata mikoa pamoja na wilaya mpya.

Kwa wale wenye kuliona jambo hili na madhara yake naomba tupaze sauti kukemea na kulikataa mapema.

Source: PMORALG - Home -


asante sana ccm naona mmeendeleza kuongeza ajira kama mlivyoahidi..mungu bariki ccm mungu bariki tanzania
 
Nipo kuwa mkuu wa mkoa au Wilaya nitajua hizi nafasi ni za kulipa fadhila..kwa watu fulani

mimi naona ni kuongeza matumizi yasiyo na tija kwani wilaya na mikoa iliyopo haina maendeleo yeyote so kuongeza mingine ni ufisadi
 
mimi naona ni kuongeza matumizi yasiyo na tija kwani wilaya na mikoa iliyopo haina maendeleo yeyote so kuongeza mingine ni ufisadi

Kuna dhana kwamba pale ambako makao makuu ya Mikoa, Wilaya viko mbali, shughuri za maendeleo hazipelekwi/zinapelekwa kwa kasi ndogo. Hii inapasw kuwa sababu kweli?.

Majimbo ya nchi ya Marekani yameainishwa kwenye katiba. Si kila anayechukua madaraka anaruhusiwa kuongeza majimbo kwa matakwa yake au wasaidizi wake. Hili halizuii kupeleka shughuri za maendeleo kwenye maeneo yaliyo mbali na makao makuu ya majimbo/miji.

Hapa kwetu shughuri za maendeleo (barabara,hosp nk) zinaweza kufanyika ipasavyo maeneo mbali na makao makuu kama kuna utashi wa kisiasa. Sasa hivi inakuwa kana kwamba walengwa wa maendeleo ni wale wanaokuwa wameteuliwa!!

Kuna tatizo gani kujenga barabara,hosp,umeme, mashule eneo fulani na kuimarisha ofisi za tarafa kwa kuwezesha watumishi ngazi hizo pasipo kuongeza utitiri wa Mikoa,Wilaya ambazo zina matumizi makubwa sana ya uendeshaji/utawala, matumizi ambayo yangeongeza huduma za kijamii maenehayo?


Je tutaongeza Mikoa,Wilaya hadi lini? Kigezo cha kikomo ni nini? Kama kigezo ni Idadi ya watu CHINA na INDIA wana mikoa mingapi?
 
MAJIMBO MAPYA YA UCHAGUZI

1. Buhigwe-Kigoma

2. Uvinza - Kigoma

3. Kakonko-Kigoma

4. Butiama-Mara

5. Chemba- Dodoma

6. Ikungi- Singida

7. Itumila- Simiyu

8. Kaliua- Tabora

9. Mbogwe-Geita

10. Mkalama-Singida

11. Mlele- Katavi

12. Momba- Mbeya

13. Nyang'hwale- Geita

14. Nyasa- Ruvuma

15. Wanging'ombe-Njombe

====================================

Wednesday, September 14, 2011
Serikali yatangaza mikoa mipya

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

TAARIFA KWA UMMA

NOTISI YA KUANZISHA MIKOA NA WILAYA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mamlaka aliyopewa chini ya Ibara ya 2(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria au kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.

Katika kutekeleza Mamlaka hayo, Rais ametoa notisi ya kusudio la kuanzisha Mikoa minne (4) na Wilaya kumi na tisa (19). Notisi hizo ambazo zimetolewa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Uanzishaji wa Mikoa na Wilaya Sura 397 ya Toleo la 2002 ni Tangazo la Serikali Na. 285 la tarehe 9 Septemba, 2011 kwa ajili ya uanzishaji wa Mikoa na Tangazo la Serikali Na. 287 la tarehe 9 Septemba, 2011 kwa ajili ya uanzishaji wa Wilaya.

Madhumuni ya Notisi hizi ni kuzialika Taasisi na mtu mwingine yeyote ambaye ataathirika na uanzishaji huo kutoa maoni, mapendekezo au pingamizi iwapo yatakuwepo katika kipindi cha siku 21 kwa Mikoa mipya na siku 30 kwa Wilaya mpya kuanzia tarehe ya Notisi hizi.

Baada ya muda uliowekwa kupita, Rais atachambua maoni, mapendekezo na pingamizi zilizotolewa na kuzitolea uamuzi kabla ya kuanzisha rasmi Mikoa na Wilaya hizo kwa kadri atakavyoona inafaa.

Mikoa mipya inayoanzishwa na Makao Makuu yake ni kama ifuatavyo: -

MKOA WILAYA ZAKE MKOA ZINAKOTOKA MAKAO MAKUU
1. Geita Geita Mwanza Geita

Nyang'hwale(Mpya) Mwanza

Chato Kagera

Bukombe Shinyanga

Mpya/Mbogwe Shinyanga

2. Simiyu Bariadi Shinyanga Bariadi

Itilima (Mpya) Shinyanga

Maswa Shinyanga

Meatu Shinyanga

Busega (Mpya) Mwanza

3. Njombe Njombe Iringa Njombe

Wanging'ombe(Mpya) Iringa

Ludewa Iringa

Makete Iringa

4. Katavi Mpanda Rukwa Mpanda

Mlele(Mpya) Rukwa

Wilaya mpya zinazoanzishwa na Makao Makuu yake ni kama ifuatavyo: -

WILAYA MPYA WILAYA MAMA MKOA MAKAO MAKUU

1. Buhigwe Kasulu Kigoma Buhigwe

2. Busega Magu Mwanza Igalukilo

3. Butiama Musoma Mara Nyamisisi

4. Chemba Kondoa Dodoma Chemba

5. Gairo Kilosa Morogoro Gairo

6. Ikungi Singida Singida Ikungi

7. Itilima Bariadi Shinyanga Itilima

8. Kakonko Kibondo Kigoma Kakonko

9. Kalambo Sumbwanga Rukwa Kalambo

10. Kaliua Urambo Tabora Kalua

11. Kyerwa Karagwe Kagera Rubwera

12. Mbogwe Bukombe Shinyanga Mbogwe

13. Mkalama Iramba Singida Nduguti

14. Mlele Mpanda Rukwa Inyonga

15. Momba Mbozi Mbeya Ndalambo

16 Nyang'hwale Geita Mwanza Nyang'hwale

17. Nyasa Mbinga Ruvuma Mbamba Bay

18. Uvinza Kigoma Kigoma Lugufu

19. Wanging'ombe Njombe Iringa Waging'ombe

Kwa taarifa hii, Wananchi wote wanaalikwa kutumia haki yao ya kisheria kutoa kwa maandishi maoni, mapendekezo na pingamizi kama zipo kwa kuzingatia utaratibu uliwekwa kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi wa maeneo husika na maslahi ya Taifa kwa ujumla. Maoni, pingamizi au mapendekezo hayo yatumwe kwa kutumia anuani ifuatayo: -


Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
S. L. P 1923,
DODOMA.

E-mail hakattanga@yahoo.com
Fax- 026-2322116


Imetolewa na: -

Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

9 Septemba, 2011
 
Majimbo yote ya Kigoma na Geita na jimbo la Momba, Wanging'ombe na Butiama yanaenda upinzani
 
CCM mbona mnatuongezea mzigo wa walipa kodi tena!!!waliokuwepo tu ni kasheshe kuwahudumia na hawafanyi kazi pale bungeni&#8230;hao watahitaji ma VX, mishahara isiyokatwa kodi,kutibiwa ulaya nk&#8230;
Kwa nini msiongeze mahospitali mazuri na shule nzuri???
 
Nina hoja binafsi hapa ,jimbo la Bukoba vijiji ni kubwa na watu wameongezeka tunataka majimbo mawili kabisa
 
  • Thanks
Reactions: EMK
ugawaji majimbo mapya ni mbinu ya watawala waliopo kuongeza wabunge toka maeneo ambayo chama tawala kina ushawishi, lakini ni kuwabebesha mzigo wananchi, kama ni uwakilishi mbona hata waliopo bungeni hawaingii, zaidi ya kula mishahara?
 
Back
Top Bottom