Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 242
Noti mpya zazua balaa
Ubora wa noti mpya zilizoanza kutumika mwanzoni mwa mwaka huu unatia shaka, baada ya kubainika kuwa baadhi yake zinachuja na kuacha rangi zikilowa maji au jasho.
Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumapili umebaini kuwa noti hizo hasa za Sh 5,000 na 10,000 zikikandamizwa au kusuguliwa kwenye karatasi nyeupe hata bila ya kuloweshwa maji au jasho, huacha rangi.
Hali hii imesababisha baadhi ya watu kutilia shaka ubora wake huku wasomi wakitaka serikalki kuwa makini kwa kuwa inaweza kupata hasara kubwa….
…….Ili kuthibitisa malalmiko hayo, Mwananchi Jumapili ilichukuwa noti ya Sh 5,000 na kuisugua kwenye karatasi nyeupe ikaacha rangi ya bluu…..
Habari zaidi katika Mwananchi Jumapili.
Noti mpya zazua balaa
Ubora wa noti mpya zilizoanza kutumika mwanzoni mwa mwaka huu unatia shaka, baada ya kubainika kuwa baadhi yake zinachuja na kuacha rangi zikilowa maji au jasho.
Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumapili umebaini kuwa noti hizo hasa za Sh 5,000 na 10,000 zikikandamizwa au kusuguliwa kwenye karatasi nyeupe hata bila ya kuloweshwa maji au jasho, huacha rangi.
Hali hii imesababisha baadhi ya watu kutilia shaka ubora wake huku wasomi wakitaka serikalki kuwa makini kwa kuwa inaweza kupata hasara kubwa .
.Ili kuthibitisa malalmiko hayo, Mwananchi Jumapili ilichukuwa noti ya Sh 5,000 na kuisugua kwenye karatasi nyeupe ikaacha rangi ya bluu ..
Habari zaidi katika Mwananchi Jumapili.
Mkuu Nguli, nasikia zinachanika kirahisi sana pia; nini kifanyike sasa? Serikali izuie mzunguko wa noti hizi mapema?
Hivi hakuna testing kabla ya kupeleka kwenye mzunguko? Wanadhani watanzania ni vilaza kutoangalia ubora wa kitu walicholetewa na wamekilipia hela nyingi kufikia kinaingizwa sokoni?
Nani wanatakiwa kubebeshwa lawama hizi? BoT? Hazina? Serikali kuu?
Bongo tambarare!
Hata TBS hawakutumika jamani?
Zinaacha rangi kwa mfano ukivaa shati jeupe ukaiweka kwenye mfuko wa shati ukiitoa inaacha rangi kwenye shati, yena na hivi kuna joto sasa hivi ndio usiseme kabisaa
Na hutasikia mtu kawajibishwa.... Wanajua wabongo mchana wanasema usiku wanalala! Kwisha!! Wizi MTUPU!!
hakuzisugua??
au kuna ulaji mwingine wamejitengenezea?? si ni shamba la bibi
Tahadhari!!
Ukilipwa noti mpya zikague vizuri.....
Kwa macho yangu nimeshuhudia juzi Ijumaa mtu kalipwa noti hizo za 10,000 mojawapo ikiwa fake!!
yaani wameshazitengeneza wakati hazijamaliza hata mwezi katika mzunguko!!