Elections 2010 [NOT CONFIRMED]: Prof. Mlambiti (wa Uchumi SUA) naye ashinda Ulanga

Matokeo yatakayotangazwa ulanga magh. Ni ushindi kwa tabibu hadji hussein mponda dhidi ya profesa mlambiti. Ni matokeo yasiyo na ridhaa ya wana ulanga magharibi lakini inatubidi sote kama wanafunzi wa demokrasia turudi ktk mstari wa kukubali na kuheshimu matokeo hayo.

Udiwani umekaa hivi kule ulanga magharibi. Ni kweli kuna wards 15 au 16 ila nina hakika na hizi zifuatazo.
kata za ulanga magharibi ni hizi hapa
1. kivukoni-chadema
2. mavimba/minepa-ccm
3. lupiro-chadema
4. kichangani-ccm
5. iragua-ccm
6. itete-chadema
7. njiwa-chadema
8. mtimbira/madira-ccm
9. mtimbira-usangule-ccm
10. sofi-tlp
11. malinyi-chadema
12. igawa-ccm
13. biro-ccm
14. ngoheranga-ccm
15. kilosa kwa mpepo-ccm
ukweli ndio huo na ni mtindo uliomuondoa dkt ngasongwa ktk kura za maoni chini ya uratibu wa celina kombani,ccm wilaya na mkoa ndio umetumika kumtoa roho profesa mlambiti.

amini usiamini mtimbira hawana vote za kumshindisha mgombea yeyote katika hali ya namna hiyo. Tafakarini wana ulanga na tupatieni majibu 2015.

mbunge mpya apewe ushirikiano ktk agenda hizi na siyo vinginevyo
  • wilaya mpya ya malinyi pasipo kuporwa mipaka ya sasa ya ulanga magharib
  • umeme
  • songea road
  • elimubora
  • elimu ya uraia kwa kila mwananchi
  • afya na huduma zingine za jamii
ikiwa mgombea anatumia milioni 50-100 kupata ubunge kwanini basi mtu huyu akishaapishwa akwepe jukumu la kuwa kinara wa maendeleo kwa hali na mali, daima utu haununuliwi.
ninawapongeza kwa kuthubutu kuleta mabadiliko, daima safari ni hatua nanyi mko safarini.........

ninawasilisha
 
Mkuu FDR, Jr asante sana kwa details. Hii detail itasaidia sana hata kwa Chadema wajipange wakati mwingine wafahamu fika majimbo ambayo ni jina la mtu linachaguliwa na si chama na pale ambapo ni chama kinachaguliwa na i jina la mtu. Kwa upande wa CCM wanachagu chama zidi kuliko jina la mgombea!! i.e sifa zake. Mifano mingi ipo kama kule kwa EDO, Chenge, Rostam Azizi, etc. Ni Rombo kwa Mamba wameamua tu kufanya mabadiliko na kwa vile wachagga wameiva sana kisiasa.
 
FDR Jr Inaelekea una taarifa nyingi, tujipange baada ya uchaguzi, tudai ile wilaya ya malinyi
 
Msongoru, FDRjr vipi hakuna habari mpya, mlambiti vipi jamani? nasikiliza bongo radio lakini sisikii chochote kuhusu ulanga magharibi
 
Ni taarifa za kusikitisha, huko Morogoro vijijini jimbo la Ulanga hali si shwali, matokeo hayatangazwi hali ya uchakachuaji ndio imetawala.

Baada ya kuona hivyo mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA Mh Prof Mlambiti awasili mjini Morogoro kuungana na familia yake baada ya kukosa tumaini ili hali anaongoza katika majimbo mengi ya huko jimboni Ulanga.
 
haileti maana hapo!! atawaachiaje wachakachue? au unapiga gumzo tu!
 
Ni taarifa za kusikitisha, huko Morogoro vijijini jimbo la Ulanga hali si shwali, matokeo hayatangazwi hali ya uchakachuaji ndio imetawala.

Baada ya kuona hivyo mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA Mh Prof Mlambiti awasili mjini Morogoro kuungana na familia yake baada ya kukosa tumaini ili hali anaongoza katika majimbo mengi ya huko jimboni Ulanga.

Acha propaganda mnajiandaa kuchakachua??
 
Ni taarifa za kusikitisha, uko morogoro vijijini jimbo la Ulanga hali si shwali, matokeo hayatangazwi hali ya uchakachuaji ndio imetawala, baada ya kuona ivo mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA Mh Prof Mlambiti awasili mjini Morogoro kuungana na familia yake baada ya kukosa tumaini ili hali anaongoza katika majimbo meni ya iuko jimboni Ulanga.

Tinno Chaz | Facebook
 
nilisikia kwenye taarifa za uchaguzi ch10 japo ilikuwa almost 2400. Kama ni kweli basi prof Kahigi wa Bukombe na Mlambiti wakiwa BUNGENI naamini japo pengo la SLAA ni gumu kuzibika lakini NEW ÅND PROMISSING REVOLUTION IS BEFORE US.

Chadema imeingiza vichwa vya ukweli yaani roho yangu imetakatika kabisa. Jamani tusimsahau na TUNDU LISU kile kichwa ni balaa sana. Mwaka huu hakuna majibu mepesi kwa maswali magumu. nakwambia ngumi zitapigwa bungeni lakin kwa maslahi ya Taifa
 
wakuu mimi nilihitimisha ktk thread yangu na kurudia msimamo huo ktk thread hii na ile breaking news, ukweli ni kwamba ccm na hasa wananchi wa mtimbira wamemuangusha prof. Mlambiti, mimi ni mwana ccm na ninakiri kuwa mtimbira walijiandaa hata kuua mtu aili mradi mbunge anatoka pale, niliwapinga sana njayagha na ngonyani simon kuwa wasiingie ktk kinyang'anyiro hiki 2010 na wamuache mzee wao amalizie msimu wa mwisho na ninawahakikishia kuwa prof. Mlambiti baada ya kushindwa na dkt. Ngasongwa kwa misimu mitatu 2005 alitamka hadharani kuwa sasa yeye na ngasongwa basi. Hii ilinifanya niamini kuwa prof. Mlambiti alikuwa na agenda binafsi na ngasongwa, sasa kilichotokea baada ya hawa jamaa ngonyani na njayagha kumharibia ngasongwa ktk ngome yake kule malinyi na ngoheranga binafsi nilijua wakiingia tarafa ya mtimbira hakuna wa kutoka na ikawa hivyo, mgawanyiko ulitokea lupiro lakini walikuwa washachelewa hatimaye hadji mponda akawashinda wote na kufuatiwa na njayagha na ngasongwa nafasi ya tatu.

baada ya matokeo hayao moyoni niliamini kuwa yamekwisha ghafla akajitokeza tena prof. Mlambiti kwa tiketi ya chadema, nilijiuliza sana kwanini hawa waliokuwa na hamu ya jimbo hili tangu 1995 na uhuru iweje wapingane??!! Ndipo nilipobaini na kutambua uhalisia wa prof.mlambiti kuwa kwake tatizo ni ccm na siye individuals, which is better for democracy.

nikajiuliza ikiwa 1995-2005 opposition ngome yake ni mtimbira kwangu tatizo likawa ni malinyi, sasa ghafla malinyi ikajivika hadhi ya upinzani na kumkarimu prof.mlambiti, mlambiti ameongoza ktk tarafa za malinyi na ngoheranga, mtimbira ameongoza mponda na kule lupiro taarifa ni kuwa prof aliongoza, figures ni hizi : Hadji mponda 18627- prof.mlambiti 15814 tofauti ni kura 2813 alizozipata mtimbira.

kuna taarifa kuwa kura za mtimbira zilijaa mizengwe na udanganyifu, professa mlambiti ameangushwa na ndugu zake kwa njaa zao. Maana kuna ushahidi wa wazi kwa wapiga kura kugawiwa shs elfu 10-20 toka mgombea wa ccm, hali hii imeonekana malinyi na mtimbira, kibaya zaidi mawakala wa chadema mtimbira ndio walionunuliwa na kumuuza mgombea wa chadema.

yamepita haya na tugange yajayo wana ulanga magharibi.
 
NI KWELI PROF AMESHINDWA KWA TOFAUTI YA KURA 2813, TAYARI MKURUGENZI WA ULANGA MZEE LUANDA AMEMSHAMTANGAZA HADJI MPONDA. DHULUMA INAUMA LAKINI MAISHA YANATUTAKA TUENDELEE, TUTAFUTE MAENDELEO YETU PALE TULIPO NA TUKUTANE 2015.

"Nikajiuliza ikiwa 1995-2005 opposition ngome yake ni mtimbira kwangu tatizo likawa ni malinyi, sasa ghafla malinyi ikajivika hadhi ya upinzani na kumkarimu prof.mlambiti, mlambiti ameongoza ktk tarafa za malinyi na ngoheranga, mtimbira ameongoza mponda na kule lupiro taarifa ni kuwa prof aliongoza, figures ni hizi : Hadji mponda 18627- prof.mlambiti 15814 tofauti ni kura 2813 alizozipata mtimbira"

Ninamuomba prof aendeleze legacy yake ktk mageuzi ya kisiasa, amepata madiwani sita, Chadema 3 na TLP 3 huo ni mtaji ambao anapaswa kuundeleza hata kama 2015 hatagombea. Chadema wanapswa warudi kule hususan Dr.Slaa mwenyewe na wakuu, elimu ya uraia bado yahitajika sana na pia msasa ufanywe kwa madiwani hawa wa upinzani ili waonyeshe tofauti ndani ya halmashauri na ktk wards, natoa pole kwa Professa, Regia lakini ninawashukuru kwa kuwaonyesha njia Ulanga Kilombero, dada Regia sasa aifanye Ulanga-kilombero ndio Mlimani city yake, tupo pamoja tutawafikia wananchi mpaka kieleweke.
Mungu ibariki Ulanga West-Kilombero
 
FDR Jr hebu fafanua , Regia unayemrefer ni nani?, harafu sielewi unaposema Ulanga west - Kilombero mimi najua Ulanga west na East
 
Back
Top Bottom